Kweli nimeamini tuna upungufu wa walimu wa sayansi na hisabati

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Nimeangalia orodha iliyotolewa na wizara ya elimu kwa watu waliotuma vyeti vyao na kukamilisha jumla nimekuta 2013 tu yani imenipa picha kuwa wahitimu wa sayansi na hisabati ni kidogo sana.

Vijana someni sayansi musikimbie.
 
Hakuna waalimu wa Sayansi wa kutosha halafu mtu anasema masomo ya Sayansi ni lazima kwa wanafunzi wote wa O-level.
Hapo nadhani walipania kuona mazero na ma F kwenye mitihani ya NECTA.

Pengine kuna waalimu wengi wa Sayansi ila kutokana na mizengwe wanayofanyiwa waalimu na serikali, wameamua kuweka vyeti vyao makabatini na kufanya shughuli nyingine zenye faida.
 
Wapeni mishshara mizuri watu watasoma saysnsi. Mishahara ya art=na sayansi
Hapa napo inabidi wapaangalie,

Mwalimu wa Sayansi anafundisha masomo mawili, practical na theory......iweje alipwe sawa na yule wa sanaa anayefundisha theory pekee?
 
No Inspiration, me ilisoma sayansi toka vidudu, nimekuja kugundua naingizwa chaka nilipomaliza first degree, nika kata corner nikaenda commercial, wenzangu waliobaki huko ni vilio kila uchao....
Btw hivi kuna haja gani ya kukomaa na ma thermodynamics, calculus, Zoology, organic chemistry na ma titration kibao ets alafu uje ulipwe laki tano..
Does it make sense to you?
 
Motisha hakuna,nani awe mwalimu,hao viongozi tu walikuwa waalimu,walikimbia nini .
Kazi ngumu,nyumba tabu,vifaa vya kufanyia kazi sifuri,lawama kibao,mshahara kidogo ,kodi na makato yanaongezeka.
Atake nani wakati vitu vingi kwa watu wa sayansi ni vingi vya kufanya.
Tutaendelea kusifia wenzetu tu.
 
Ina maana bado ulikuwa hujaamini?!

O-Level nilisoma private school yenye kila kitu including best laboratories na walimu wa kumwaga wa sayansi! However, out of mikondo 6 ambayo tulikuwa nayo pale shuleni, ni mikondo miwili tu ndio tulikuwa tunasoma sayansi! Na kati ya hiyo mikondo miwili, ni mmoja ndio ulikuwa serious na sayansi kwa sababu mkondo mwingine walikuwa wanasoma na history na hivyo wengi walikuwa wanaenda art.

So, ikiwa shule ambayo ilikuwa na kila kitu bado ilikuwa inashindwa kutoa wanafunzi wa sayansi; vipi zile shule zetu??!!

Tatizo la kusoma sayansi nchi hii ni zaidi ya kuwa na maabara na walimu...!!
 
Hakuna waalimu wa Sayansi wa kutosha halafu mtu anasema masomo ya Sayansi ni lazima kwa wanafunzi wote wa O-level.
Hapo nadhani walipania kuona mazero na ma F kwenye mitihani ya NECTA.

Pengine kuna waalimu wengi wa Sayansi ila kutokana na mizengwe wanayofanyiwa waalimu na serikali, wameamua kuweka vyeti vyao makabatini na kufanya shughuli nyingine zenye faida.
Hivi Tanzania kuna masomo ya Sayansi au?Maana nina wasi wasi na ili
 
Nimeangalia orodha iliyotolewa na wizara ya elimu kwa watu waliotuma vyeti vyao na kukamilisha jumla nimekuta 2013 tu yani imenipa picha kuwa wahitimu wa sayansi na hisabati ni kidogo sana vijana someni sayansi musikimbie

Mbona nimeona jumla ni1054
 
Watu wa naona mbali ndio maana waliwapeleka UDOM ili kufidia gap lkn alipokuja mjuaji akawaita vilaza. Tutaendelea na upungufu huo hadi mwisho kama hakuna mikakati
Kuna wengine kibao wamemaliza mwaka huu, vyeti hawajapata watapunguza udadi
 
Back
Top Bottom