Kweli Mwanaume na mwanamke wako sawa?

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,834
Mimi sio mwanasheria ila natakakujua kisheria kuwa Mwanaume na mwanamke wako sawa? na je wanahaki sawa?
Maana kwangu mimi imekuwa kero kubwa sana maana kila wakati nasikia haki sawa haki sawa na ukiangalia inakinzana na utamaduni wetu wa kitanzania na hataule wa kidini.

Jamani naomba elekezo ya kisheria
 
kwenye katiba.. wote ni sawa
kwenye sheria.. mwanamke anabebwa
kwenye dini.. mwanaume ni kinara
katika uhalisia.. mwanaume yupo juu ya mwanamke, ata ktk ngazi ndogo kbsa.. familia, baba ndo grand finale mwenyewe
 
Wewe muuliza swala lenyewe linajionesha kuwa hawako sawa.Tangu zama za Enzi ya bustani ya Eden na uasi wa mwanadamu mwanaume hajawahi kuwa sawa na mwanamke. Mungu alitoa majukumu ya mwanaume kwa kula kwa jasho lake na mwanamke kuzaa kwa uchungu.Ndugu yangu hapo usawa uko wapi?
Ukija kiasisa umewahi kusikia wanaume wakipendelewa kwenye elimu,viti maalum,umoja wa akina baba, wanaume wakiwezeshwa wanaweza, mikutano ya dunia ya wanaume watupu.Mpaka hapo huo usawa unautoa wapi.
 
Ndugu,

Inategemea unaongelea usawa katika nini. Mambo ya ki-binadamu na ki-mausiano ni mengi na yanayohitaji usawa lakini usawa huo hauji kwa kufikiria bali hali harisi. Anza na maumbile hatuko sawa, sheria/sera wanawake wanabebwa hasa katika kipindi hiki, Kwenye kazi ngumu wanaume mbele, Mahari wanalipa wanaume na mambo mengine mengi japo katika ya nchi na sheria nyingine hata za kimataifa zinasema watu wote ni sawa bila kufafanua katika lipi.
 
Back
Top Bottom