Kweli mtaji wa masikini ni nguvu zake?

Dec 5, 2019
62
99
Jamaa mmoja kutoka Ipinda Kyela alienda Chunya kwa lengo la kuchimba madini.

Baada ya kufika alifurahishwa na kuvutiwa sana na ukarimu wa watu wa kule kitu ambacho kilimfanya awe na amani as if ni mwenyeji.

Safari yake ya kwenda porini iliwadia akaingia kwenye hardware na kununua sululu, koleo (spedi), na buti. Kisha akaenda kuchonga mpini wa sululu vifaa vikawa tayari.

Kama alivyopokelewa na wenyeji wake waliojaa ukarimu wa hali ya juu, akapelekwa porini tayari kwa kuanza kazi.

Nanukuu,
"Tulienda pori moja linaitwa Godima tulizunguka sana kutafuta mchanga lakini kila tulipotoboa michanga haikuwepo"

Swali: Michanga ya nini sasa?

Jibu: Dhahabu hukaa kwenye mchanga na mawe madogo madogo.

Okey tuendelee,

Nanukuu,
"Ile siku tuliimaliza kwa kufanya poor survey na kutoa ardhi ili kupata mchanga'' siku ikaisha.

Kesho yake wakahamia sehemu nyingine ambayo wazungu waliwahi kupita na kuchimba kwa kutumia vifaa vyao bora.

Nanukuu,
"Tulienda sehemu nyingine waliyopita wazungu, nasi tukaanza kuchimba marudio, baada ya kuchimba mchanga wa kutosha tukasubiri wapimaji"

Swali: Wapimaji ni wakina nani na wanatoka wapi?

Jibu: Kuna watu wananunua vipimo na kupimisha kisha wanatakata 20% hadi 30% huwa wanafanya hivyo mahali wachimbaji wadogo wadogo wapo.

Baada ya wapimaji kupima jamaa akabahatika kupata gram 12 @ gram ilikuwa ni Tsh.50000/=

Yes, akaona neema ndiyo hiyo mambo ni safi mdogo mdogo.

Akarudi alipofikia na kula bata kidogo. Huku akiamini kesho atapata zaidi ya kile.

Kesho yake wakarudi na kufanya kazi kwa nguvu mpya na matumaini mengi kuja kupima hakuna chochote hata chenga.

Jamaa hakukata tamaa,
Kesho yake wakaendelea na kazi kama kawaida. Lakini pia hakupata kitu but wenzake walipata akapata faraja toka kwao, siku ikaisha.

Siku iliyofuata kazini kama kawaida. Baada ya kazi kupima hamna kitu tena. Ililiendelea vivyo hivyo siku, wiki, wik 2, wiki 3, mwezi hakuna hata gram 1.

Nanukuu,
"Tukahama pori na kuenda kuweka kambi kabisa huko huko porini, sehemu inaitwa matundas tulikaa porini tukichimba usiku na mchana wenzangu walikuwa wanapata lakini mimi hapana. Nilikaa porini wiki 3 bila kupata hata gram 1"

Swali: Sasa uliishije na kula nini?

Jibu: Jamaa tulipkuwa wote walikuwa wanapata siku nyingine walikuwa wananisaidia kiasi"

Jamaa anaendelea kufunguka,
Tulikaa kwenye pori hilo kwa miezi 2 bila kupata dhahabu yeyote. Hata wenzangu nao wakaanza kukosa kabsa.

Tukaamua kuhamisha kambi na kupeleka pori lingine. Ambako nako tulifanya kazi miezi 3 bila kupata dhahabu ya aina yeyote japo jamaa wakuwa wanapata ndogo ndogo.

Swali: Kwanini uliamua kuendelea kukaa porini huoni kama ulikuwa unapoteza muda badala ya kurudi nyumbani na kufanya mambo mengine?

Jibu: Hali ilikuwa mbaya mpaka nauli ya kurudia nyumbani nilikosa, pia jamaa walikuwa wananiomba nisikate tamaa tutakula kitakachopatikana.

Maisha ya porini yakaendelea
Kwa bahati mbaya sehemu waliyoweka kambi ilikuwa ni mbali zaidi kuliko maeneo yote waliyopitia. Unga wa ugali ukawa umeisha kuenda mashineni mazishe zikawa zimeharibika.

Nanukuu,
"Jamaa ikabidi waende mjini kufuata mahitaji ilikuwa ni safari ya siku nzima kwenda tu.

Tulibaki wawili kambini njaa inauma ni hatari, basi kulikuwa na maharage lakini maji tuliishiwa maana kiza kilishakuwa kimeingia, Tulikaanga maharagwe na kuyala kama bisi (mahindi yaliyokaangwa)

Swali: Huko porini kulikuwa na mito ya maji?

Jibu: Dada yangu acha tu, chunya ni kukame sana hakuna mito, Tulikuwa tunakunywa maji ya mvua yaliyokuwa yanatuama kwenye madimbwi mbalimbali"

Jamaa anaendelea kufunguka,
Kesho ilipofika hata hatukuenda kuchimba mwili ulilegea kwa njaa, tukaenda kuyatafuta maji kwanza tukiwa njian tukakutana na mdudu,

Swali: Mdudu!!!, mdudu gani na ikawaje?

Jibu: Ndio dada yangu, tulikutana na nyoka aina ya cobra ilikuwa karibu na kichuguu alichokuwa kilichokuwa karibu na rafiki yangu.

Sitosahau ile siku, yule nyoka akaanza kutukimbiza tukatawanyika akalimfukuzia rafiki yangu na kumng'ata rafiki yangu nikiwa na namuona kwa mbali.

Mimi ni muoga sana wa nyoka nilikimbia sana huku niomba msaada bahati nzuri jirani kulikuwa na wasukuma wakichunga mifugo yao.

Tulienda kumsadia jamaa lakini tayari tulikuta ameshatangulia mbele za haki.

Swali: Daaah, kwani wale wenyewe hawaogopi na nyoka hakuwasikia ninyi maana ilikuwa ni muda mfupi kwa maelezo yako.

Jibu: Wasukuma wana dawa wao hawadhuriki wala mifugo yako, nami nilipewa ile dawa kama kinga wala nyoka hakurudi tena.

Basi jamaa wa mjini wakaja na kukunana na majonzi ya jamaa yetu. Marehemu alikuwa ni mtu wa Mbeya lakini alikuwa na wenyeji wake pale Chunya maeneo ya Sinjilili.

Baada ya kumaliza mazishi ya jamaa. Tukarudi porini na kuhama lile pori.

Maisha yaliendelea kama kawaida kesho yake mvua ilinyesha sana mashimo yote yalijaa maji na mifereji ikaanza kupitisha maji siku ile hatukuchimba.

Eneo hili kidogo lilikuwa na watu pia kulikuwa na udongo mzuri kwa kilimo. Nilikutana na mzee mmoja alikuwa analima lima maeneo yale mvua ikinyesha namkumbuka kwa jina la MZEE BEN SANGA. Yule mzee aliniambia maneno mengi na kunishauri pia.

Nanukuu,
"Mwanangu uchimbaji wa madini ni kama kamali kuna kupata na kukosa pia una mambo mengi.

Nakushauri sasa mvua zimenyesha haya maeneo yana rutuba waweza lima ni nguvu zako tu "

Nilimsikiliza mzee lakini nilishindwa nimjibu nini, nikaishia kusema "Asante mzee wangu kwa ushauri mzuri lakini saizi sijajipanga"

Yule mzee alicheka sana kusikia neno sijajipanga. Akaniuliza kijana una tatizo lolote la kiafya? Akili yako iko sawa? Nikajibu ndiyo niko sawa.

Kisha nikaondoka na kwenda kambini kuwasimulia jamaa zangu wakanicheka na kuniambia nikishindwa nirudi nyumbani lakini sio kilimo cha Chunya.

Kesho yake maji bado yalikuwa yamejaa kwenye mashimo.hivyo hatukuchimba tena. Nikaenda kwa yule mzee.

Nanukuu,
"Mzee shikamoo, samahani jana ulinicheka sana na uliniuliza maswali, naomba kujua kwanini ulifanya vile?"

Mzee anajibu,
Kijana mimi nina miaka 53 sasa, ujana wangu nilipoteza muda sana, sasa najuta na kuona thamani ya muda.

Kama hujajipanga vizuri kwenye uchimbaji wa madini acha fikiria kilimo ndiyo uti wa mgongo.

Mzee akaendelea kunisihi. Najua bado wewe ni kijana unga nguvu na unaweza kulima mimi nitakupa shamba na mbegu kuhusu mbolea huku hatutumii ardhi ina rutuba"

Sikumuelewa kabisa yule mzee,
Nikamwambia mzee nashukuru bora nirudi tu nyumbani. Nikarudi kambini na kuwafahamisha jamaa zangu kuwa nataka kujaribu kilimo walinicheka sana.

Basi nikaachana nao kisha nikaenda kwa mzee ben sanga, Mungu ambariki na kumrehem mahali alipo.

Yule mzee nakumbuka alikuwa ni msabato, akanipa hekari moja kama kianzio nikaanza kulima kwa mkono asubuhi, mchana na jioni.

Niliweza kufanikiwa kumaliza ile hekari, akaniongezea nyingine nikajitutumua hatimaye nayo nikamaliza muda wa kulima ukawa umeisha.

Alinipa mbegu nikapanda. Ardhi ya kule ilikuwa na rutuba sana walikuwa hawatumii mbolea mahindi yaliota vizuri sana.

Wakati huohuo mzee naye alikuwa anajishughulisha na uchimbaji wa madini lakini yeye alikuwa anaifanya hiyo kazi wakati amemaliza kazi za shamba na kurelax.

Akanifundisha kuchimba na kuosha ule mchanga ili kupata dhahabu maana uchimbaji wake ulikuwa ni tofauti na ule tuliouzoea.

Yaani yeye hata chenga alikuwa anapata ambazo zilikuwa zinaangukia kwenye point 6,7, hadi gram 1 zilitosha kutufuta machozi.

Mavuno ya mahindi yalivyowadia sikuamini nilichokiona. Kila hekari ilitoa gunia 32 zenye ujazo wa debe 7. Hivyo nilipata gunia 64.

Nilimshukuru sana MUNGU na yule MZEE BEN SANGA kwa ushauri mzuri na kunisaidia kama mtoto wake.

Niliona miujiza zaidi baada ya kuwa na soko zuri sana la mahindi kipindi kile yalipanda sana,

Nakumbuka debe ilikuwa ni Tsh 15000/=. Nikajikuta nakamata pesa ambayo tangu nizaliwe nilikuwa naiona kwenye video tu.

Kimahesabu ilikuwa
15000×7×60

Gunia 4 sikuziuza nilitoa shukrani kwa yule Mzee BEN SANGA.

Aliniambia haya maneno:
"KIJANA NGUVU ZAKO NDIYO MTAJI WAKO, USIOGOPE KUANZA NA KIDOGO JUHUDI YAKO KWENYE SEHEMU SAHIHI ITAKUFANYA NDOTO IWE"

Nilimshukuru sana yule mzee,
Hakuishia hapo kwa kuwa nilikuwa napenda kulima mpunga. Aliniunganisha na watu wa Kamsamba maisha yanaendelea sio haba.

USHAURI KWA VIJANA:
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na ardhi kubwa maeneo mengi ya porini unatumia nguvu zako tu kwani kuna sehemu ukiomba wanakupa wewe unafanya kazi ya kufyeka pori na kuanza kulima mdogo mdogo nguvu zenu ndio mtaji wako tuache kupoteza muda namba za umri hazigandi.

HABA NA HABA HUJAZA KIBABA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Story yako nimeipenda sana hakika nimejifunza kitu aisee ubalikiwe sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom