Kweli Mkapa kalidanganya taifa, ona hapa jinsi Vicent Nyerere alivyo mtoto wa ukoo wa Nyerere

Umenena: Mkapa akasema amefanya kazi na Mwalimu, amemzika, hajawahi kusikia Mwalimu Nyerere ana mtoto wake mwenye jina kama hilo.

Inaonyesha Mkapa alimaanisha si BLOOD SON wa Kambarage ambavyo natumaini ni kweli ingawa Vincent ni mwana ukoo wa Nyerere.
 
This is excitement for no reason. Mkapa anategemewa vipi kuwakumbuka watu wote anaowapa hela? Mkapa ni mtu mkarimu,amewapa watu wengi hela. Hakumbuki kama alimpa ubani Vicent.
Nakumbuka siku moja,Mama Anna Mkapa alipokuwa First Lady,alikuwa anatoa zawadi katika hoteli fulani,deep into the night,mpaka akaanza kusinzia.
Nadhani complaint ya Vicent hapa ni kwamba kama ameitwa yeye siyo mtoto wa Nyerere basi yeye no mtoto wa nani? Kwa hiyo maneno ya Mkapa yamemfanya aonekane tapeli. Lakini hili ni jambo limefanyika bila kukusudia. Mkapa anweza kusema kwamba alikosea,lakini it would be too strong a word to call that an 'apology'
 
haya sisahngai kwa jibu lako..mimi nataka nikupe crediti zako wewe unapanic..ni wasi sio wewe nimeshapata jibu. asante kwa kuileta jamvini.

Pole pole mzee wa TISS aka usalama wa ccm, Usimkolimbe magamba 3
 
Mkapa atakuwa aliomba kujumuisshwa kwenye ukoo wa Nyerer kwa lengo la kujisafisha

Umewahi, mimi pia nilitaka kuandika hivi kwamba Mkapa aliomba kujumuishwa kwenye ukoo huo kwa ajili ya kujisafisha. Ikumbukwe ni wakati huo alipo wapromote watoto wawili wa Kambarage kuwa wabunge wa kuteuliwa.
 
Kutokana na nlichokipata hapo juu toka kwa mtoa mada ni kwamba Mkapa alisema hajawahi sikia kama kuna mtu anaitwa Vincent Nyerere kwenye familia ya Mwalimu Nyerere; kama ilikua hivyo na kulingana na ufafanuzi wa namna ukoo wa Nyerere ulivyo basi sioni kama Mkapa alikosea kwa kauli hiyo lkn kama angesema hajawahi sikia jina hilo kwenye ukoo au Familia ya Nyerere basi hapo mtu mzima angekua ameteleza; Kwa mantiki hiyo basi ukweli wabak kuwa Vincent Nyerere ni mtoto wa Nyerere na si mtoto wa Mwl.JKN
 

Asante sana. Sasa tunaomba utupe katiba ya ukoo wa kina nyerere mtu aliye na ukoo wa kupewa na sasa anaonekana ameuchoka ukoo kama huyu chinga tunamtosaje?
 
...Akumbuke kuwa Mwalimu akiwa hai alimweleza kuwa ukoo wa Burito ni mkubwa.
Kwa hiyo ukoo ni Burito au ni Nyerere? Unajichanganya.

Alichoamua kufanya ni kutumia jina la ubatizo na jina la kuzaliwa linalobeba jina lake na la ukoo, yaani la babu yake.
Kama jina la ukoo maana yake ni jina la babu then kila mtu ana babu yake, kwa hiyo Julius and Vincent being of different generations should never share a surname because they have different grandfathers! Kwa hiyo Vincent alijipachika jina la babu, sio la ukoo!

Matumizi ya jina ‘Nyerere’ yamekuwa makubwa kwa sababu ni jina la ukoo..... kwa sababu jina Nyerere ni la ukoo, na si la Mwalimu Kambarage. Mwalimu ni sehemu ya ukoo huo.
Well, kama kuna such thing as jina la ukoo na Nyerere ndio jina la ukoo, na kama kimila unaitwa jina lako na la ukoo basi baba yake mwalimu, yani Chifu Nyerere, alipozaliwa angeitwa Nyerere Nyerere, yani alilopewa na la ukoo. Lakini akaitwa Nyerere Burito, yani lake na la baba yake. Kama ambavyo Julius nae alipozaliwa akaitwa Kambarage Nyerere, yani lake na la baba yake. Kwa hiyo tuseme hao waliowatoga majina Julius na pia Chifu Nyerere walikuwa hawajui system za kutoga majina za kizanaki? Walikosea mara mbili?

Kwa hiyo Vincent sio mtoto wa Kambarage wala sio mtoto wa Nyerere, ni mtoto wa Kiboko.

Jina lake lilitakiwa liwe Vincent Kiboko, kama ambavyo mwalimu aliitwa Julius Nyerere, lake na la baba yake. Na kama ambavyo mwenyewe umekubali kwamba ingekuwa absolutely correct kwa Andrew kuitwa Andrew Kambarage.

Kwa nini umruke babaako mzazi ukajiite jina la babu mwanzisha ukoo ambae wengi wetu hatujui aliishi lini na wapi, alifanya nini maishani, kwa nini ana ujiko wa sisi kuchukua jina lake, yeye mwenyewe jina lake la ukoo ni nani, kwa nini tuanzie kwake, na kwa nini baba yangu aliyenifikisha hapa nilipo asahaulike?

Utaona mwalimu hakuitwa last name ya Burito ambayo ndio babu yake, kwa sababu alikuwa proudful na baba yake, akajiita Julius Nyerere. Kwa hiyo kuna sababu za wazi za kusadiki kwamba Vincent is shying away from "Kiboko" as his Surname.
 

wewe huna hoja...
Unajua kweli mana ya surname? Kanywe uji....
 
Kama jina la ukoo maana yake ni jina la babu then kila mtu ana babu yake, kwa hiyo Julius and Vincent being of different generations should never share a surname because they have different grandfathers
!


Kweli rafiki yangu aliwahi kunambia kuwa, hapa JF kuna washambuliaji na wachambuzi. Anhe User U'r the later. :hand:
 
@MAGAMBA MATATU: Kwanza naomba uniweke sawa, hivi karibuni ilisikika kuwa Mkapa alifanikiwa kuwa mwanaukoo kwa kuandika barua. Lakini katika post yako umesema/andika kuwa Mkapa mlimpa heshima ya kuwa mwana ukoo.

Sasa je ni utaratibu upi hasa mnautumia ili kumuhalalisha raia asiye mwanaukoo wenu kuwa mwana ukoo?





Pili naomba unifafanulie ni lini mlianza kutumia utararibu huo ? yaani utaratibu utakaokuwa umeeleza katika swali langu la kwanza hapo juu, na watu wangapi mmewahalalisha kuwa wana ukoo wenu? ikiwezekana wataje hata majina hao mliowahalalisha.
 
Kwa hiyo Vicent amelithi mikoba ya ujasiri, uadilifu, umahiri na vyote vya Baba wa taifa?
 
utaratibu huu wa kutumia surname ulikuja wakati wa wakoloni, kabla ya hapo ndio hizo system ya mtu kuitwa jina la baba yake, na mtoto au mjukuu kupewa jina la babu yake, kama ulivyo sema mfano Emil kambarage, lakini hapo hapo Emil angeweza kupewa jana la Nyerere au Nyakigi nk kama hishima ya hao wakubwa wa Kambarage kama wajomba zake, Baba yake ambaye atakuwa ni Babu kwa Emil nk, sasa katika hiyo transition ya ku-adopt jina moja kuwa la ukoo kulitokea mchanganyiko huo wa jina la ukoo pia kupewa watu binafsi katika koo hizo hizo wakifuata mila na desturi zao za zamani, na hii si huko tu zanaki au musoma na kwingineko, hata wewe ukiuliza asili ya jina la ukoo wako utakuta kuna hitilifu hizo. sababu za kufuata mfumo huo wakoloni waliona wakati ule kutokana na kutukuweko kwa kumbukumbu watu wengi ndugu walipotezana, baada ya kuhama au kwenda vitani. leo chukulia mtu wa ukoo wa mkapa, tuseme walizaliwa watano, lakini kama ilivyo kuwa desturi za wakati huo kila moja akatukuza hilo jina la baba yake bila kuweka kina saba cha babu, halafu watu hao hao wakatoka machinga mwingine akaenda kilwa na labda huko akao, kama alikuwa mkristo kule kilwa akapata binti wa sheikh hivyo akabadili jina na wengine kwa heshima ya sheikh aliye mfungisha ndoa akawekeza na jina la sheikh , unafikiri baada ya muda watoto wake watawajua ndugu zao wa machinga, na hapo ni moja tu aliye kwenda kilwa, hapo hapo waweza kukuta dada kaolewa msumbiji, mwingine alikwenda malawi, mwingine alikwenda shinyanga kwenye machimbo au morogoro kama manamba, mwingine alikwenda burma kwenye vita kuu. je watu hawa baada ya muda wataunganika vipi? haya ndio yalikuwa nimatatizo yetu.
 

Mkapa alitenda hivyo akiwa amekusudia kwa 100% ili kumchafua Vicent. jiulize
1-Unadhani mkapa hakuwa anajua kuwa jina la nyerere ni la ukoo au ni la baba yake kambarage (mwl Juliusi)?
2-Unadhani alikuwa hajui kuwa baba yake kambarage yaani mzee nyerere alikuwa na watoto wengine kama akina Joseph na wajuu wengine kutoka kwa wana wengine wanaotumia jina lao la ukoo la nyerere?
3-Unadhani mkapa hakusema hivyo akijua kuwa watanzania ni mbumbumbu na hivyo watakubaliana na hila zake ili wamwone Vicent anajikomba kwa familia ya mwl Nyerere?
4-Au yeye benjamin mkapa amewazuia jamaa zake wa ukoo wake wasitumie jina la ukoo la mkapa, kwamba ni lake yeye na wazaliwa wake tu?

Sijawahi kusikia mtu anajiingiza kwenye ukoo mwingine tena wa kabila jingine kama alivyofanya mkapa kujiingiza kuwa mwana ukoo wa nyerere? phewwww....
 
utaratibu huu wa kutumia surname ulikuja wakati wa wakoloni, kabla ya hapo ndio hizo system ya mtu kuitwa jina la baba yake, na mtoto au mjukuu kupewa jina la babu yake,
Ngoja kwanza, haiwezekani kusema mtu anaitwa jina la baba yake na mtoto anapewa jina la babu yake, ina maana huyo "mtoto" wakati anazaliwa hakuwa "mtu"?

Mpaka hapo ushachemka vibaya sana, hueleweki.

Hoja yangu ilikuwa ni kwamba mtaalam wa majina ya kizanaki ameshindwa kueleza kwa nini Julius Nyerere alitumia last name ambayo ni jina la baba yake, na kwa nini baba yake Julius, yani Nyerere Burito, nae pia alitumia last name ambayo ni jina la baba yake, badala ya Nyerere, kama Nyerere ndio jina la ukoo.
 
Namkumbuka kiboko (josephat) nyerere alisumbua sana pale musoma mjini.

Yer aliwahi kuwekwa ndani gereza la Butimba (MZ) miaka ya themanini siku moja Bibi Mgaya akaja kumchukua. Mkuu wa mkoa alimpigia Mwalimu, akamwambia, 'sasa mie nifanyeje kama amekuja kuchukua mtoto wake, mpeni'. Kiboko alikuwa kiboko kweli!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…