Kweli Mkapa kalidanganya taifa, ona hapa jinsi Vicent Nyerere alivyo mtoto wa ukoo wa Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Mkapa kalidanganya taifa, ona hapa jinsi Vicent Nyerere alivyo mtoto wa ukoo wa Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Mar 18, 2012.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  MWENYEKITI Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ni mmoja wa wana ukoo wa Nyerere Burito.
  Mkapa alipewa heshima hiyo mwanzoni mwa miaka ya 2000, baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Sherehe za kumtambua rasmi kama mwana ukoo zilifanyika nyumbani kwa marehemu Chifu Edward Wanzagi Nyerere, kijijini Butiama.

  Juzi, Mkapa amesikika akimshambulia Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), wakati akizindua kampeni za CCM za Uchaguzi Mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki. Mkapa akasema amefanya kazi na Mwalimu, amemzika, hajawahi kusikia Mwalimu Nyerere ana mtoto wake mwenye jina kama hilo. Akasema inawezekana huyo analitumia ajinufaishe kisiasa.

  Baada ya kumsikia Mkapa kwa makini, nimeamua kuzungumza na Vincent Nyerere. Naye akaonyesha mshangao wake. Akajiuliza inakuwaje mwana ukoo mwenzake (Mkapa) amshambulie kwa sababu tu ya jina. Tena nikajiuliza, ilikuwaje siku ile alipokaribishwa rasmi kwenye ukoo, hakuhoji, “mbona huyu Chifu anajitangaza kuwa mtoto wa Baba wa Taifa?” Najua hakuhoji kwa sababu anajua kuwa Chifu Edward Wanzagi, baba yake ndiye huyo huyo baba yake Kambarage, yaani Nyerere.

  Baada ya kutafakari, nimeona nijaribu kuweka sawa haya mambo. Kwanza nianze na ukoo huu wa Nyerere. Lakini haitakuwa vema kuuanza ukoo huu bila kumhusisha Mwalimu kwanza.

  Kwa ufupi ni kwamba jina la Baba wa Taifa ni Julius Kambarage Nyerere. Jina Julius ni la ubatizo. Jina Kambarage ni la asili lenye maana ya ‘mzimu wa mvua’. Jina Mwalimu lilitokana na kazi yake ya ualimu. Kama walivyo walimu wengi, alipenda kuitwa ‘Mwalimu’ badala ya ‘Mheshimiwa au Dokta’. Tena kwa wasiojua, jina la kwanza kabisa la Mwalimu Kambarage lilikuwa Mgendi, lenye maana ya ‘mtembezi’ kwa lugha ya Kizanaki. Kwa nini wazazi wake waliliondoa jina hilo na kumpa jina la Kambarage, huo ni mjadala mwingine ambao nikiombwa nitauzungumzia.

  Hivyo basi, mtiririko wa jina lake ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Burito Mazembe Wisigana Tandari. Hii ina maana kwamba Kambarage alizaliwa na Nyerere. Nyerere (Baba yake Mwalimu) alizaliwa na Burito. Burito alizaliwa na Mazembe. Mazembe alizaliwa na Tandari. Orodha ni ndefu.

  Hadi hapo, utaona kuwa Nyerere si jina la Mwalimu. Bali jina lake ni Kambarage Nyerere, ikiwa na maana kwamba Nyerere ni ndiye baba yake mzazi. Ni kama leo kuna kina ‘Mkapa’ wengi, hiyo haina maana kwamba wanaotumia jina hilo wanataka kujitanabahisha kuwa ni watoto wa Mkapa yule ambaye ni Rais Mstaafu. Unaweza kuuliza, iweje watoto wa Mwalimu waitwe majina kama Burito (Andrew) Nyerere, Anna (Watiku) Nyerere, Emil (Magige) Nyerere, Makongoro (Charles) Nyerere, John (Guido) Nyerere, Pauleta Nyerere, Madaraka (Godfrey) Nyerere au Rosemary Nyerere?

  Matumizi ya jina ‘Nyerere’ yamekuwa makubwa kwa sababu ni jina la ukoo. Ni jina kama yalivyo majina makubwa ya kina ‘Mkwawa’, ‘Makongoro’, na kadhalika. Hao watoto wa Mwalimu hawakutumia jina ‘Nyerere’ kama jina la baba yao, bali ni la babu yao, yaani Nyerere Burito. Unaweza kusema Nyerere alikuwa maarufu, lakini aliyelipa umaarufu zaidi ni Mwalimu Kambarage.

  Ni sahihi Makongoro akaitwa Makongoro Kambarage, Burito Kambarage, Madaraka Kambarage, Rosemary Kambarage, Magige Kambarage, Nyerere Kambarage, na kadhalika. Nadhani hadi hapo tupo pamoja.

  Je, huyu Kambarage Nyerere hakuwa na ndugu wa tumbo moja? Alikuwa nao. Baadhi yao ni Nyangete Nyerere, Nyakahu Nyerere, Nyakigi Nyerere, Kizurira (Joseph) Nyerere na kitindamimba katika tumbo la Bibi Mgaya (Christina) Nyang’ombe (mama wa wote hawa) ni Kiboko (Josephat Nyerere). Kitindamimba huyu alifariki dunia miaka ya karibuni kabisa. Mkapa alihudhuria mazishi yake kijijini Butiama.

  Huyu huyu, Josephat Kiboko Nyerere (kitindamimba katika tumbo la Bibi Mgaya), naye kapata watoto wengi. Hapa siwezi kuwaorodhesha wote. Lakini miongoni mwao ni VINCENT NYERERE KIBOKO NYERERE.

  Wazanaki ni watu wanaoheshimu mila. Kurithishana majina ni moja ya mambo muhimu sana kwa Wazanaki. Ndiyo maana alipozaliwa huyu (mbunge), baba yake (yaani Kiboko Nyerere) aliamua kumpa jina la ‘Nyerere’ akiwa amempa heshima hiyo baba yake mzazi, yaani Mtemi Nyerere Burito aliyefariki dunia mwaka 1942. Alikuwa Mtemi wa Butiama. Kama mbunge huyu angeamua kutumia majina ya Kizanaki, angeitwa Nyerere Kiboko Nyerere. Alipoamua kutumia majina ya ubatizo, akaweka jina Vincent na akaongeza la kwake la kuzaliwa la ‘Nyerere’; hivyo jina lake likawa Vincent Nyerere. Angeweza kuweka kando jina la ubatizo akatumia jina la Nyerere J.K. Nyerere (Nyerere Josephat Kiboko Nyerere). Alichoamua kufanya ni kutumia jina la ubatizo na jina la kuzaliwa linalobeba jina lake na la ukoo, yaani la babu yake.


  Ni kwa sababu hiyo, mgeni yeyote anayefika Butiama anaweza kupigwa bumbuwazi kwa kusikia jina ‘Nyerere’ likitamkwa kama salamu. Hiyo ni kwa sababu jina Nyerere ni la ukoo, na si la Mwalimu Kambarage. Mwalimu ni sehemu ya ukoo huo.

  Lakini jina la Nyerere leo limefika mbali zaidi. Kuna waigizaji wanaitwa kina Steven Nyerere, kuna Nyerere wengi sana kila kona ya Tanzania. Afrika ina kina Nyerere wengi. Marekani ndo usiseme kabisa! Hii haina maana kwamba wanaoitwa ‘Nyerere’ wanataka kujitafutia umaarufu kwa kutumia jina la Mwalimu au wanataka wajulikane kuwa wamezaliwa na Mwalimu Kambarage. Hapana.

  Kwa ufafanuzi huu nadhani mwana ukoo Mkapa atakuwa ametambua kuwa huyu mbunge kuitwa Vincent Nyerere si kwa sababu ya kutaka kujikweza, bali hilo ndilo jina lake halisi. Endapo atajiita Vincent Kambarage Nyerere, hapo ndipo tunaweza kusema anataka kujitambulisha kama mtoto wa ‘Mwalimu’. Na ni kweli kwamba Mwalimu Kambarage ni baba yake mkubwa Vincent Nyerere. Hilo halina mjadala.

  Tunamkaribisha mwana ukoo Mkapa akutane na sisi wazee ndani ya ukoo ili tupate kumpa somo. Akumbuke kuwa Mwalimu akiwa hai alimweleza kuwa ukoo wa Burito ni mkubwa. Huo unajumuisha familia za Chifu Wanzagi, Kambarage, Jackton, Wisigana, Muhunda, Nyamboga, Daniel, Kizurira, Nyakigi, Nyabisenye na nyingine nyingi. Kwetu sisi, Vincent Nyerere ni mwana ukoo na mjukuu halisi wa Nyerere Burito Mazembe Wisigana Tandari. Hajawahi, na hatawahi kujinasibu kama mtoto wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ingawa ukweli ni kwamba kiongozi huyo ni baba yake mkubwa. Wazazi wao wametoka kwa baba mmoja na tumbo moja la mama. Kama kuna kitu nimekisahau, basi mwana ukoo mwingine asaidie kukiweka wazi.
   
 2. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Asante sana mkuu kwa kutujuza! Ubarikiwe.
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  duh....family pyramid
  Good to kniw and keep for the benefit of new generation
   
 4. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe magamba matatu ndio umeandika hii habari?
   
 5. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  asante kwa ufafanuzi mkuu! zile za Mkapa zilikuwa ni mbwembwe za kampeni tu lkn ukweli alikuwa anaujua vizuri sana.
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Che Nkapa ametusaidia kuijua historia ya ukoo wa Mwalimu Nyerere, ingawa tume learn in a hard way...

  Bado majibu kuhusu Mkapa kumuua Nyerere, Je ni kweli walikuwa wametofautiana kuhusu ubinafishaji? Na je ni kweli kama ukoo mlikataa asipelekwe Uingereza kwa kuwa waingereza walikuwa na bifu naye ya kulete uhuru, Mkapa akalazimishwa aende huko kutimiza Conspiracy theory??? Tujuze kiongozi wa ukoo
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  NIlimdharau sana mkapa kwa hoja yake hiyo ya kipuuzi, kwamba hata yeye anaweza kuwazuia watoto wa mdogo wake wasitumie jina la ukoo/babu yao la mkapa kwa sababu tu yeye Ben amekuwa rais na hivyo watoto wake yeye binafsi ndiyo wenye hati miliki ya jina la mkapa.
   
 8. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Unataka kujua ukweli wa malumbano na kujua nani muongo kati ya mkapa na Vicent au wataka kujua nani kaiandika hii habari????
  Be serious,,,,,
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Che Nkapa kaombe radhi....umechemka mazima!!!!
   
 10. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Namkumbuka kiboko (josephat) nyerere alisumbua sana pale musoma mjini.
   
 11. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hivi mkapa ana watoto wangapi?
  Yule keneth mkapa wa yanga ana undugu na huyu rais mstaafu?
   
 12. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Benjamini William Mkapa (amezaliwa 12 Novemba, 1938) ni Rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi, CCM (Revolutionary State Party)

  Mkapa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere. Nafasi alizoshikilia zamani ni pamoja na kuwa afisa wa utawala huko Dodoma na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. Yeye pia aliongoza ujumbe wa Tanzania huko Marekani na alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka 1977 hadi 1980 na kutoka 1984 hadi 1990.


  Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kwa kumuunga mkono kwa nguvu rais wa zamani Julius Nyerere Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi.


  Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha makampuni yanayomilikiwa na serikali na akaweka sera za soko huru. Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.


  Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi [SUP][3][/SUP] vilevile njia yake duni ya kutumia fedha. Alitumia £15 milioni kununua ndege ya kibinafsi ya kirais, vilevile karibu £30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalam waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi . Ilikuwa juu ya ununuzi huu wa mwisho ndipo Katibu wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania.

  Baada ya kutoka ofisini kutokana na kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa anakumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa fedha Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo.

  Kwa kujibinafsishia mwenyewe mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu.

  Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007.[4
   
 13. d

  daligo JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 535
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mapambano yanaendelea
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  mkapa kaua, jamani baba wa taifa.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkapa anasema alikuwa anatania!!!
   
 16. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Copy paste and save for future use
   
 17. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Aibu ya Mkapa itakuwa kubwa pale tu CCM watakaposhindwa Arumeru. Ila kama wakishinda kama Igunga hii habari itasahaulika just the following week...
   
 18. mwenyenchi

  mwenyenchi JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo inawezekana BM (na mafioso wenzake JK, EL, RA) walimpumzisha kwa lazima Mwalimu ili waweze kutafuna rasilimali za taifa bila bugudha?! Shutuma nzito hizi
  BM kama kawaida yake kanuna na kufumba mdomo hawezi kuzijibu
  Mzee wa ukoo (Magamba Matatu) your opinion please
   
 19. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,163
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Magamba Matatu na Wana JF,
  Nikupongeze kwa Historia fupi na kuondoa kutojua na kutuweka kwenye ufahamu mzuri, my take Mzee Mzima BM alikuwa anapima Upepo wa Siasa, ila hope meseji send, siasa chafu hazitakiwi na utani anaosema utamletea shida sana. Nampongeza kwa kutaka suluhu aka kupatana mapema kabla mambo hayajaharibika.
  Nawakilisha   
 20. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  haya sisahngai kwa jibu lako..mimi nataka nikupe crediti zako wewe unapanic..ni wasi sio wewe nimeshapata jibu. asante kwa kuileta jamvini.
   
Loading...