Kweli michepuko inabalaa na vijana UKIMWI hautawaacha

Kweli michepuko inabalaa na vijana UKIMWI hautawaacha

bomouwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,149
Reaction score
800
Habari wana jamvi?

Juzi majira ya saa mbili na nusu usiku, nilikua maeneo fulani na washikaji zangu tunabadilishana mawazo. Lakini wakati tunaendelea maana hiyo sehemu ni hotel panaitwa Malaika ipo Jijini Mwanza.

Katika kuzungusha macho sikuamini nilipomuona mke wa rafiki wa baba yangu mzazi akiwa na kijana ambae ninamfahamu kabisa ni afisa manunuzi wa kampuni ya familia ya mama huyo wakiwa wanaingia hotelini hapo.

Lakini nilishindwa kuamini ikabidi nimuite mtu fulani ambae ni mfanyakazi wa hoteli hiyo nikamuuliza juu yao na akaniambia kua uyo jamaa mbona ni kawaida yake na huyo mama wanakujaga sana hapo na ni watu waliokatika mahusiano.

Nilichoka kabisa yani huyu mama anamiaka kati ya 50-55 na huyo kijana namfahamu ameoa juzi juzi anamiaka kati ya 28-32.Baada ya kuona nilioyaona ukizingatia mmewe ni mgonjwa wa mambo yetu haya ya siku hizi.

Nikasema hea zinaangamiza vijana sana maana mama anajijua kabisa kaumia lakini kijana najua anavolazimisha ushindi anapiga kama ilivo.

Mungu atusaidie jamani
 
acha wapate UKIMWI arv's zenyewe ni bure wasipopata ukimwi zitakua hazina mtumiaji
 
Pole zake, anusurike tu na ngoma maana ndo inapelekwa kwa mke hivo
 
hata sasa hivi wewe mwenyewe unaweza kuwa na UKIMWI, au hujui kirefu cha hilo neno
 
usivuke barabara huku umefumba macho UKIMWI upo
 
Tafuta email ya jamaa fungua email mpya mweleze huyo kijana huwezi jua pengine bado hajapata maambukizi na ukaweza kuoa maisha ya mtu mwengine asie na hatia yani mke wake, roho inapokusukuma kufanya jambo hasa la tahadhari inakuwa ni malaika wema hao, jarib kufanya hivyo pengine anaweza akaenda kucheki afya yake na akavunja hao mahusiano hakuna anaetaka kupoteza maisha yake kirahisi.
 
Si mnapenda kitonga acha mfe tu! Anampa hela na tiketi ya kuliona kaburi.
 
duuuu totoz napenda ila ngoma naogopa pia mpenzi revola siku hizi hayuko though nlimtumia sana enzi hizoooo!!!!!
 
Tafuta namna ya kumsaidia huyo mshkaji wako asiangamie.
 
Dunia ina speed kali sana katika kujizungusha kwake kwenye mhimili wake wenyewe
 
Tafuteni tu hela ya maana kuhudumia afya zenu kwa maana Ngoma ni lazima mpate kwani hamna namna eeeeh! Hamna namna.
 
Nenda kamwambie ukweli kuwa umemuona na huyo mama na umpe ushauri aangalie afya yk na aachane na huyo mama immediately,usipofanya hivyo utakuwa humjatendea haki huyo kijana
Ushauri:vijana wote acheni tamaa,kumbukeni there is no free lunch ni hatari,kijana tafuta pesa kwa juhudi na maarifa fursa tz bd zipo nyingi sana
 
Boda boda zinaua na kila siku mnapanda...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom