Kweli Marehemu Dennis Michael (R.I.P) ni mhanga wa Demokrasia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Marehemu Dennis Michael (R.I.P) ni mhanga wa Demokrasia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMARADE, Jan 13, 2011.

 1. K

  KAMARADE Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi na Mwanafalsafa nguli wa itikadi ya ukombozi wa bara la Africa, Kamarade Amilcar Cabral aliamini kuwa mafanikio ya mapambano ya ukombozi yatategemea sana nidhamu binafsi (Personal Moral Behaviour), uungwana (Dignity) na uaminifu (Honesty) wa viongozi wa mapambano hayo na wafuasi wake.


  Na katika kuangalia mafanikio na matatizo mengi yaliyolikumba bara la frika miaka hamsini baada ya uhuru, wasomi kadhaa wametanabaisha kuwa ukosefu nidhamu binafsi, uungwana na uaminifu miongoni mwa viongozi waliopo na wale wanaotarajiwa kuchukua nafasi za waliopo pamoja na jamii kwa ujumla ni moja ya sababu kubwa za tatizo la ombwe la uongozi linalodidimiza bara letu hivi sasa.


  Tangu na baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 kufanyika hapa nchini, chama cha CHADEMA kimejitanabaisha na mambo mengi mengi ambayo yameweza kuendeleza na kujenga hamasa kubwa zaidi miongoni mwa mashabiki wao na pia kuzua maswali kadhaa miongoni mwa watanzania wengine. Lilianza lile la kumsumsia na kutomtambua rais Kikwete, likaja la vita vya kumsulubu kisiasa Naibu Katibu Mkuu wao Kabwe Zitto, likaja la maandamano ya Arusha yaliyopelekea mauaji ya watu watatu ambao wote kwa pamoja wakapewa hadhi ya uhanga wa kile kinachoitwa Mapambano ya Demokrasia na sasa hili la mazishi ya kizalendo ya wahanga hao wawili. Wapo wanaosema kuwa haya ni moja ya mambo ya kawaida kujitokeza pale mafanikio yanapozidi kiwango matumaini na wapo wanaosema kuwa hiyo ni sura halisi ya haiba, fikira na dhima zinazotawala chama hicho.


  Katika suala la maziko ya kizalendo ya waliohadhiwa kama wahanga wa maandamano hayo nimekuwa najiuiliza sana maudhui na mantiki mazima ya uhanga wa Marehemu Dennis Michael. Hii inatokana na taarifa kuwa wakati ni kweli Marehemu Ismail alikuwa ni mmoja wa waandamanaji , taarifa kutoka ndani ya familia ya Dennis Michael zinadai kuwa kijana wao Dennis hakuwa ameshiriki katika maandamano hayo bali alikuwa mpita njia katika eneo alilouawa akielekea kuchukua gari la jamaa yake mmoja baada ya kupigiwa simu muda mchache kabla ya tukio hilo. Wanaendelea kudai kuwa kamwe Dennis hakuwahi kushiriki katika mambo ya siasa na hata siku hiyo alikuwa akilalamika sana kuhusu uamuzi huo wa Chadema kukimbilia hatua ya maandamano ambayo yangeleta machafuko.


  Kutokana na taarifa hizo imenibidi nijiulize hivi inakuwaje Marehemu Denis akawa mhanga wa mapambano ya demokrasia kama yalivyoitwa na Chadema na washabiki wao? Hivi nini maana ya mhanga wakati anayepewa hadhi hiyo hakuwa miongoni mwa waandamanaji na alipatwa na dharuba hiyo bila ya hatia yoyote? Lakini zaidi najiuliza, hivi Chadema hawakujua hili ama waliamua kufunika kombe ili uharamia upite? Lakini zaidi, ni kwa nini ndugu zake hawakuwa wakali kulinda haki yake ya kiutu na kumuacha Dennis kutumika kama turufu ya kisiasa?


  Lakini zadi inanileta katika suala zima la hulka ya viongozi wetu wa kisiasa ambao wako tayari kutumia kila njia kuweza kufanikisha mradi wao wakati mwengine bila ya kujali misingi rahisi ya utu kama vile uungwana na uaminifu kwa unaoamini kuwa unawatumikia.


  Ukweli ni kuwa pamoja na kuhoji uhalali wa kumtangaza Marehemu Dennis kama mhanga na kumtumia kufanikisha malengo ya kisiasa ambayo kwa kiasi fulani Chadema wamefanikiwa lakini pia hili linanileta katika kuamini kuwa tatizo la uongozi usioamini katika umuhimu wa nidhamu binafsi, uungwana na pia uaminifu ni kubwa kuliko tudhaniavyo. Na ubaya zaidi ni hali ya wengi wetu (raia) kuwa tayari kuyafumbia macho na kuyakumbatia mapungufu hayo sasa tukijidanganya kuwa kufanya hivyo kutatusaidia kuondokana na tatizo la sasa (CCM) huku tukisahau kuwa kuna zaidi ya sasa huko tuendako (Tanzania).
   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  ushujaa wa Denis unakuja pale alipouawa kwa nguvu za uzalimu na mabavu ya chombo cha dola ..polisi chini ya utawala wa sisiem pasipo kuchukua taadhari ya wapi matumizi ya nguvu yatumike... this is brutal killings of innocent civilians ..... nani asiyejua hilo....

  makala yako yote ni Crap...umekurupuka
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ndio maana watu wanaitwa wahanga; Dennis amekuwa mhanga kwa sababu he became a casualty of police brutality in a political setting. Amelipa gharama ya maisha yake kwa sababu kuna smart guy somewhere aliamini kuwa watu hawana haki ya kutumia haki yao ya kutoa maoni yao ya kisiasa kwa njia ya maandamano. Ni sawasawa na na hawa waliouawa huko Arizona ambao wengine walikuwa katika shughuli za kawaida wakati mlengwa alikuwa ni congressman.

  Kwa hiyo ni mhanga wa demokrasia kwa sababu ameuawa mikononi mwa dola iliyokuwa inajaribu kuzima harakati za demokrasia. Like the kid shot in Soweto, au wale waliouawa wakati wa Civil right movements hapa kule Alabama. ​
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu, iwe Dennis alikuwa kwenye maandamano au hakuwepo suala zima hapa ni kwamba Dennis aliuwawa na polisi katika zoezi zima la kujaribu kuwatawanya waandamanaji. Dennis asingekufa kama sio kuwepo kwa hayo maandamano na hivyo sioni kwa nini asipewe heshima ya kuwa muhanga!!!! Haijalishi kama alikuwa mwanachama na shabiki wa CDM au hapana.

  Tiba
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Natumaini ndugu yetu anayehojia uhanga wa Dennis atapata mwanga kuwa mtu anapoitwa mhanga (victim) simply haijalishi hasa ilikuwaje bali ni mhanga. Na inaonekana karibu wote tunakubaliana kuwa alikufa katika mazingira ambayo ni ya kisiasa kwa kosa lisilolake.
   
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280

  alikufa kishujaa katika mazingira hatarishi pasipo kutambua yanayojiri ... sote tukiamini polisi wangelinda amani na si kukiuka na kuvunja sheria kwa kufanya mauaji ..yaani kupiga risasi za moto passipo na uvunjaji wa sheria....

  political illusions dilutes law enforcing agents
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  KAMARADE, hivi mhanga ni mtu wa namna gani kwa uelewa wako. Wewe ni kati ya wale watu utadhani wana akili wakati wako kimya lakini subiri waongee ndio utatambua kuwa hata kule kudhani tu wana akili japo kidogo ni kuwapa sifa wasiyokuwa nayo.
   
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Rais Obama kasafiri kwenda Tucson kwenye memorial service ya walikufa kwa risasi,Huyu Congress woman alikuwa kwenye shughuli za kisiasa
  akiwatembelea wapiga kura wake,je yule mtoto wa miaka 9 aliyefariki alikuwa member wa chama chochote? kwa nini bendera imepepea nusu mlingoti?kwanini hujahoji hayo?

  Obama has already spoken to many of the victims' family members by phone.


  "The president thought it was important to visit the Tucson community since this tragedy touched everyone there as well as throughout the entire country in some way," White House spokesman Nick Shapiro said.

  "The president believes that right now, the main thing we should be doing is offering our thoughts and prayers to those who've been impacted and making sure that we're joining together and pulling together as a country," he added.

  Obama on Monday led the nation in a moment of silence as flags across the country flew at half-staff to honor the victims.
   
 9. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MM umechapia, congresswoman. but point taken
   
 10. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu Kamarade tumekusikia. Basi tu tuseme kidumu chama chako......mengine tuachie wenyewe.
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  makala ndefu sana maneno 551; swali na hoja ni moja tu "Kwa nini DENIS awe VICTIMS wa serilkali dhalim, au VICTIM wa serikali inayouwa raia wake kwa mabavu, au VICTIM wa Mauaji ya Kuzima democracy huko Arusha" hii si haki hata kidogo; hizo sentensi tatu zinajieleza kabisa haziitaji Insha ya maneno 551.

  Nimesema hivyo kwa sababu watu wanajaribu kutoa majibu wakidhani huelewi, lakini kama ungalikuwa huelewi hakika kwa lugha sahihi swali lako singalizi maneno 8; "kwanini DENIS aitwe mhanga wakati hakuwa kwenye maandamano?

  Pole sana, ndugu yetu Mpendwa majibu yametolewa mazuri sana yanatosha ukiongezana na maswali matatu hayo hapo njuu pia ni majibu unaweza kuyatumia; Mwambie aliyekutuma kwanza akupeleka shule upate Elimu, kaka Elimu na kuelimika ndio uje na hoja tata
   
 12. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwani Dennis kafa kwa ajali ya ndege?
  Si kapigwa risasi na polisi wakizuia maandamo ya CDM!
  Kwa nini polisi walimuua kama alikuwa tu kwenye mishe mishe zake?
  Sasa unaongeza kosa jingine kwa polisi, wameua hata wapita njia!
  Kwa nini aliuwawa?
  Ukijibu swali hili, utanisaidia kujua kama ni mhanga wa demokrasia au la.
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  KAMARADE wewe ni KADA wa CCM, MWana CCM damu kijani au FISADI uliyeumizwa na kuachwa na Donda ndugu kwa kuona Mazishi yanafanyika bila vurugu na bila ulinzi wa Polisi wenye kubeba Silaha kali.
  KAMARADE umekuja hapa kuchujua AMANI na Haki ya Marehemu.
  Umekuja hapa kumbeza Marehemu.
  Umekuja hapa kusema uongo dhidi ya mtu anayeweza kujitetea kupitia historia ya maisha yake tu.
  Umekuja hapa kama Fisi alojeruhiwa vibaya lakini anamatumaini tele ya kifisi.

  Kifupi unaleta Mzaha mbele ya jambo kubwa na muhimu kwa kila binadamu, KIFO.
  Unakubali POLISI walipiga Risasi kwa nia ya kuua waandamanaji, haya tuseme Denis hakuwa pale kuandamana na Risasi ile ilimpata na kumpokonya uhai wake.
  Je huo Marehemu amekufa kwa niaba ya waandamanaji na waleambao hawakuandamna lakini wanaunga mkono maandamano?

  Kama ingekuwa ni rahisi kujijenga kisiasa kwa kumtumia Marehemu sidhani kama CCM ingeacha kupokonya nafasi hiyo, tuache hilo.
  Dennis Michael amefariki kwa sababu POLISI wa Arusha walipewa Amri na IGP kutumia Risassi za Moto dhidi ya MAandamano bila kujari nani atadhurika(Hii inaonyesha ufupi wa akili ya IGP) Naye IGP alipata Amri ya Kisiasa kutoka ngazi ya juu kabisa ya Serikali ya CCM.
  Mkuu wa Kaya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ndiye aliye ua na kujeruhi watu pale Arusha.

  KAMARADE Riwaya yako hapo juu ni upuuzi na wazimu mkuu.Ni watu wenye akili kama yako msimamo wa kisiasa kama wako na mtizamo wa kiuchumi kama wako ndiyo pekee ambao hawawezi kuona kwamba RIWAYA yako imesimama juu ya MASHONDE.

  KAMARADE you SUCK!!!!!!!
   
 14. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  vic┬Ětim


     [vik-tim] [​IMG] Show IPA
  –noun1.a person who suffers from a destructive or injurious action oragency: a victim of an automobile accident.

  Sijaona kosa la Chadema hapo.Dennis ni victim wa injurious action ya Polisi wa Arusha. Victim = Mhanga.
  Does this need the whole 6 paragraph? au una lako jambo?

   
 15. K

  KAMARADE Member

  #15
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri mnaojua kiswahili mmenifahamisha maana ya uhanga, lakini mnasemaje kuhusu hali ya kukosa uungwana na uaminifu wa kuweka wazi kuwa marehemu Denis Michael hakuwa mmoja wa waandamanaji ama wafuasi wa Chadema kama ambavyo viongozi wa Chadema wamekuwa wakikaririwa katika kumuelezea marehemu huyo. Na jee hii si dalili mbaya ya aina ya wakombozi tunaowapa imani yetu na kuwashabikia?

  Na jee ni vipi mtazam uliojengwa kwa watanzania kuhusu uhusika wa marehemu Dennis na maandamano hayo? Msimamo ambao viongozi wa Chadema wametumia nguvu nyingi kuujenga kwa faida ya kisiasa?
   
 16. K

  KAMARADE Member

  #16
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moderator acha ushabiki. Ni haki yangu kutumia kichwa cha habari nilichochagua na kama hakina madhara ya kijamii si jukumu lako kubadilisha na kuweka kichwa cha habari kinachokufurahisha ama kukidhi maslahi yako.....Kichwa cha habari (Title) niliyotumia ni Ninahoji UHANGA wa Marehemu Dennis Michael (R.I.P) na sio Kweli Marehemu Dennis Michael (R.I.P) ni mhanga wa Demokrasia?
   
 17. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umepata na umeelewa maana ya mhanga?
   
 18. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Good! Kama polisi waliuwa mpita njia then Mwema must be taken to the hague!
   
 19. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kamaradi, ushabiki wa siasa unao wewe. Hiyo unayoita turufu ni nini?

  Je ulitaka CHADEMA waiachie familia ya Dennis mzigo wa kumzika bila kupaza sauti ili umma ujue nini kilichotokea? Haya, tuwe waungwana, kama CHADEMA ingekaa pembeni na kuachia familia izike kimya kimya kwa kuogopa watu kama wewe kusema mnayoyasema ni michango kiasi gani ingetolewa kuwasaidia watoto wawili, Angel na mwenzake, wa marehemu? Watu kama wakina Sabodo wangeguswa vipi kuchangia sh. Milioni Tano kwa kila familia kusaidia angalau kidogo? Serikali kama inajua kwamba Dennis hakuwepo kwenye maandamano kwanini hawajatoa hata sanda ya kumzikia??? Kwanini hakutoa msaada wowote badala wakawaachia CHADEMA kufanya hicho unachoita siasa??

  Labda hujui, Polisi walienda nyumbani kwa marehemu wote wakawa wanawashawishi wasipeleke miili uwanjani kuagwa. Familia ya Ismail ilisumbuliwa sana mpaka asubuhi tarehe 12-01-2011 bado walikuwa wanasumbuliwa. CHADEMA wakaamua kusema wanaheshimu uamuzi wa familia na mwili wa Ismail hautapelekwa uwanjani lakini baada ya muda familia ikawafuata vingozi wa CHADEMA na kusema wako tayari marehemu aagwe uwanjani. Hiyo ilikuwa saa tano asubuhi!!!! Ikabidi ratiba iangaliwe upya, utaratibu ufanyike ndipo Ismail akaletwa uwanjani!! Na ndiyo sababu ratiba ilichelewa kuanza!

  Unayoyasema ni kutoka kichwani kwako na siyo hali halisi iliyopo. Ni vyema ukauliza badala ya kuwa mwepesi kuconclude jambo.

  Ndugu wa Dennis (baba yake mkubwa) wakati wa mazishi alisema "sitanyama mpaka niambiwe ni mahakama gani iliamuru Dennis ahukumiwe kifo. Sitanyamaza mpaka haki na ukweli vipatikane". Kwa hasira kubwa alifikia mahali akasema "yeyote anayesema viongozi wa dini wavue majoho waache kukemea dhambi ni malaya" (Mod hayo si maneno yangu nimenukuu kuonyesha ukweli.) Huo ndio msimamo wa familia au ndugu zake Dennis. Sasa kama ukweli utakuwa ni CHADEMA ndio wamesababisha basi watajua!!

  Mazishi yaliyoratibiwa na CHADEMA yalikuwa na malengo yafuatayo;

  1. Kuonyesha kusikitishwa kwake na vitendo vya polisi kutumia nguvu kupitiliza na kuua raia wasio na hatia.

  2. Kutimiza wajibu wake kama chama cha siasa kinachojali uhai wa mtu na kuguswa na maisha ya kila mtu.

  3. Kuuonyesha umma kwamba vitendo vya polisi havina nafasi katika jamii yetu.

  4. Kuwapa wanananchi fursa ya kushiriki mazishi ya binadamu wenzao ambao wameuwawa kikatili na polisi.

  Ndio sababu hukuona CHADEMA wakitumia magari kueleka watu uwanjani. Ndio maana hukuona CHADEMA wakipita mitaani na miili ya marehemu kuwaonyesha wananchi. Ndio maana wananchi wote walijaa uwanjani walienda pale wenyewe kwa mapenzi yao. Usilaumu CHADEMA kwa sifa wanazopata kutokana na kufanikisha hilo.

  Kuhusu suala la 'imani' kwamba waislamu hawaweki marehemu hadharani lazima ujue yafuatayo;

  1. imani ya kiislamu hairuhusu polisi kuua raia wasio na hatia.

  2. imani ya kiislamu hairuhusu unyanyasaji wa raia.

  3. imani ya kiislamu haizuii ukweli kusemwa na haki kupiganiwa.

  4. Na mbona hukuhoji Dkt Omar Ali Juma alivyofariki? Au Ismail ndio imeleta shida??

  Si kwamba naifahamu imani ya kiislamu au nina uelewa bali nadhani kwa kiasi kikubwa kulikuwa na msukumo kutoka kwa baadhi ya watu kuzuia mwili wa Ismail usiletwe NMC ili kueonyesha kwamba CHADEMA ni chama cha wakristo na hawakumjali muislamu. Pili kuongeza nguvu kwenye hoja kwamba Masheikh Arusha wamemtambua Meya. Sasa hii kwako inaweza kuwa sio siasa ila ni vyema ukaipatia jina!!

  Siku ambayo tutaacha kuwa mashabiki na wakurupakaji badala yake tukatoa hoja objectively then tutakuwa tumewatendea haki watanzania wote wasio na nafasi kama ya kwetu. Endapo tutaendelea kutoa mawazo kwa ushabiki basi nchi itaendelea kuzama kwenye tope na sisi tutabaki kupiga story humu JF!!
   
 20. K

  KAMARADE Member

  #20
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Msando,

  Hivi wewe ambaye ni wakili wa viongozi wa Chadema huku ukwaita askari polisi kuwa ni mbuzi na kushangilia kuwa kuna askari polisi wamafukuzwa katika nyumba ya kupanga bila ya kusema kuwa mwenye nyumba ni mchaga amabye ni mfuasi mkubwa wa Chadema unadhani kuwa unaweza kuwa objective kwa kitu chochote.

  Uzuri ni kuwa wote hapa hakuna aliyepinga kuwa Dennis hakuwa mfuasi wa Chadema wala miongoni mwa waandamanaji lakini cha ajabu hamuoni tatizo na kutumia kifo chake kufaidika kisiasa. Na hapa ndio ninahoji uungwana na uaminifu kwa watanzania ambao mnadai mnafanya yote haya ili kuwakomboa.

  Lakini pia sikushangai sana kwani kwa taarifa nilizonazo ni kuwa hata katika halmashauri ya Moshi Vijijini ambayo uligombea kuwa mwenyekiti ulihonga sana madiwani wa TLP ili wakupigie kura lakini mmoja wao akakataa kudanganyika.
   
Loading...