Inategemea unamaanisha Pesa kwa namna ipi,..1. Pesa "as a medium of exchange"? 2. Pesa utajiri. Kama jibu ni moja basi 100% kweli,kwasababu dunia ya sasa kila kitu kinahitaji pesa for exchange,kwa mfano. Ukienda hospitali huwezi kupata huduma kama huna pesa ya kumwona daktari au ya kununua dawa. Hivyo katika mapenzi Pesa kwa maana hiyo namba 1 inahitajika kwasababu kuna mambo ya msingi na ya lazima kama kula,makazi na malazi ambapo kuvipata hivi kwa dunia ya sasa pesa lazima.
Kama utakuwa umemaanisha namba 2 yaani utajiri,basi hiyo si kweli,wapo watu waliishi,wameishi,wanaishi na wataishi katika hali za kawaida tu na mapenzi yakawa motomoto.