sheiza
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 7,634
- 11,691
Kweli nimeamini mpira ni mpaka filimbi ya mwisho ipigwe ndio muda mzuri wa kushangilia na kutamba.. Nakumbuka 2010 jinsi Dr Silaa alivyokuwa anakusanya mafuriko kwenye mikutano ya kampeni..huku e-polls zote za kwenye mitandao zikionyesha amemuacha mbali JK..Hapa mtu atakuambia watu hawakujiandikisha lakini hao hao watu ndio walifanikisha kupitisha wabunge wa chadema kwa uwingi wao..
Kikubwa hapa hususani kwa hiki kizazi kipya cha siasa msidanganyike na wingi wa watu kwenye mikutano ya Lowasa mkadhani ushindi tayari..hakuna kitu kama hicho..Kwa nchi za kiafrika matokeo ya mwisho ndio hutoa mshindi wa urais.. Kwa hiyo msitegemee ushindi kwa kutumia hicho kinaitwa mafuriko kwenye mikutano.
Labda kuna mtu atasema kuchakachua lakini nani kathibisha..tunarudi palepale kwamba matokeo ya mwisho ndio hutoa mshindi wa urais..