Kweli kua uyaone; Nimeamini ndoa ni kitu kigumu sana

Ukiangalia mtiririko wa matukio yote haya unaweza kuona kuna pattern za usaliti.

Cha msingi ni kwamba kabla ya kufunga ndoa hakikisha mwenzio umemjua nje na ndani. Yes najua wanasema ukimchunguza bata hutomla ila kwakweli kwa haki ilivyo ni bora kujua mapem kuwa mwenzangu yuko vile ili uamue unao au lah.

Vitu kama tabia ya usaliti mwenzako akiamua usijue hutajua. Kwa wanaomini kwenye maombi basi wanasema maombi pekee ndio yatakayokupa mwenza mwema. Hatakua malaika ila mazuri yake yatafunika mabaya/kasoro alizonazo. Plus uaminifu lazima uwepo. Kama haupo hapo hata maombi hayaoni ndani
 
Usaliti hata ufanye hivi IPO siku utashtukiwa tu tena kiulaini ndoa nyingi chanzo huwa ni usaliti wa mmoja na mwingine anasaliti, sasa hapo upendo inaisha,
 
Usaliti hata ufanye hivi IPO siku utashtukiwa tu tena kiulaini ndoa nyingi chanzo huwa ni usaliti wa mmoja na mwingine anasaliti, sasa hapo upendo inaisha,

Si ndio lile box sasa, mume kaweka usaliti na mke nae anaweka usaliti 😀😀kwisha kazi
 
Si ndio lile box sasa, mume kaweka usaliti na mke nae anaweka usaliti kwisha kazi
Kwanza ukishaanza kujua mwenza wako anachepuka upendo hupungua kabisa, na wewe u natafta wako hapo hamsikilizani wala kukanyana maana ngoma droo
 
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili ya hiari bila kuhamasihwa na mtu yeyote sasa ukiona ndoa haidumu kuna sehemu mwiko umekiukwa
 
Kuishi kwenye ndoa ni kipaji sio kila mtu anacho, kwenye maisha ya ndoa kitu pekee kuwe na mapenzi toka Pande zote, hapo ndio utasikia uvumilivu, subra, lakini mapenzi yakikosekana Hakuna lolote, kama unampenda mtu utamvumilia kwa kila upungufu wake, kama humpendi hata akupeleke peponi hutashukuru, ila utakuja kuachana nae kwa kuambiwa tu umbea
 
Mbona yakwangu ni ya mfano mzuri, na wengi wanaotufahamu tume wa inspire waingie ndoani hasa ukizingatia tulioana tukiwa vijana wadogo umri wa 24.
Sasa tunawatoto wa wili na bado kama kumbikumbi na michezo yetu yakitoto....

So hizo ndoa za kizinifu na nyingine zilizofeli zisiwe mfano kwako.
Bado ndoa yako changa! Siku likikukuta ndo utajua why watu wanalalamika ndoa hazina maadili siku hizi
 
ndoa ni kitu kizuri sana kwa kuwa toka mwanzo kinajengwa kwa mazingira ya kisanii hivyo sio ajabu kuishia hivyo inavyokuwa.
tunaanza kutongozana kwa kudanganyana na usanii mwingi sana.
lakini toka ndoa ya kwanza ya Adamu na Eva aliyechangia kuondoa upatanisho na MUNGU ni mwanamke, lakini bado MUNGU hakumuhukumu mwanamke bali mwanaume.
ukiwauliza wanaume wengi walio bar mpaka saa sita za usiku kwanini wapo muda huo wakikwambia ukweli tatizo ni wake zao. wanawake ni wa kuishi nao kwa akili.
waislamu sio wengi bar kwa kuwa option zinawasaidia ukichoka unaacha au unaongeza mwingine.
 
Mifano mitatu uliyotoa haitoshi kusema ndoa ni ngumu. Msafara wa mamba kenge pia wamo.
 
Muhimu ni kuishi kwanza pamoja miaka 5 kabla ya kufunga ndoa. Lolote zuri au baya Litafaamika tu.
 
Mbona yakwangu ni ya mfano mzuri, na wengi wanaotufahamu tume wa inspire waingie ndoani hasa ukizingatia tulioana tukiwa vijana wadogo umri wa 24.
Sasa tunawatoto wa wili na bado kama kumbikumbi na michezo yetu yakitoto....

So hizo ndoa za kizinifu na nyingine zilizofeli zisiwe mfano kwako.
Mkuu ndoa ni endelevu. Kuna Siku unawezafanyiwa kituko ukaja kuifuta hii comments.. Endelea kuitetea kila Siku. Omba sana usije hundua wala kuujua ubaya mwenza wako.
 
Back
Top Bottom