Huo si utamaduni wa Kigoma, watu wa Kigoma sisi ni wazuri sana ni wakalimu sana hatuna matatizo na mtu, tunapapenda nyumbani, na kwa sasa maendeleo mimi naona ni mazuri inazidi mikoa mingi ie kuna stand ya mkoa ambayo inajengwa ni nzuri sana ukitoa dar hakuna mkoa ambao una stand nzuri kama hiyo, nitajitahidi niweke na picha, tuna sehemu ya kupumzika nyingi sana mikoa mingi haina ie Bangwe beach, golden beach, kibirizi beach, katonga beach, Lake Tanganyika hotel beach, Zungu beach nk. kuna mikoa mingi tu haina beach, kwa sasa zinawekwa lami nzuri kwa kiwango cha zege na sio ya tabaka moja yaani asphat concrete. Maji ndio usisema, mawese, hifadhi, samaki, dagaa nk.