kende
JF-Expert Member
- Dec 2, 2013
- 3,527
- 1,669
Currently niko Bukoba, jana pasaka kulikuwa na mashindano ya kushake na kuimba maeneo ya beach, msanii Songa wa Tamaduni Music na M-Rap walikuwa na show kwenye Club moja maarufu huku, wakaja kutumia hilo jukwaa kuwavuta watu usiku waje kushuhudia show yao maana kulikuwa na nyomi ya maana, MC kwa mbwembwe akawaita jukwaani wajitambulishe hawa wasanii 'wa dar' akidhani watu watashoboka, cha ajabu wamepanda watu kimyaaa, wanajitambulisha watu kimyaa, MC ikabidi aseme wangapi wanamjua Songa mikono juu ikaonekana kama mikono 7 (ukijumlisha na wangu). Dah nikasema kweli ukitaka ufanye hiphop ya kweli unachallenge kubwa maana ni raia wachache sana wanaokusoma, kama unataka kufanya biashara ya muziki ni bora ufate nyayo za kina Neema Wa Mitego tu