Kweli hii ni Tanzania au ni Dubai au Calfonia kama ahadi inavyosema. Hivi huyu Nahodha anatusaidia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli hii ni Tanzania au ni Dubai au Calfonia kama ahadi inavyosema. Hivi huyu Nahodha anatusaidia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fasta fasta, Jun 29, 2011.

 1. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  nyumbayagorofa.JPG SERIKALI inatumia zaidi ya sh milioni 50 kwa mwezi kwa ajili ya kugharimia malazi na chakula kwa ajili ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, anayeishi katika Hoteli ya New Afrika tangu alipoteuliwa, Tanzania Daima Jumatano, limebaini.

  Taarifa ya Waziri Nahodha kuishi hotelini, ziliibuliwa bungeni wiki iliyopita wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Ingawa taarifa ya bungeni hazikuwa za kina, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini Nahodha ambaye amepata kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), amekuwa akiishi hotelini hapo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo Novemba mwaka jana.

  Habari kutoka ndani ya hoteli hiyo yenye hadhi ya Nyota Nne zilisema waziri huyo amepangishiwa vyumba vitatu ndani ya hoteli hiyo.
  Inaelezwa kwamba amepanga kwenye moja ya vyumba maalumu kwa vigogo, (Executive); chumba ambacho kina sehemu mbili, ikiwemo ya kulala na ya kumpumzikia.

  Kwa mujibu wa habari hizo, chumba hicho kinalipiwa dola 300 kwa siku, sawa na sh 480,000.
  Vyanzo vyetu vya habari vilitonya kuwa chumba cha pili kinatumika kwa ajili ya walinzi na wasaidizi wake na cha tatu ni kwa ajili ya wageni muhimu wanaomtembelea hotoleni hapo hasa familia yake ambayo iko Zanzibar.
  Habari hizo zinasema vyumba hivyo vinagharimu dola 220 kila kimoja kwa siku.
  "Kwa maana hiyo, serikali kwa siku inalipa dola 740, sawa na sh 1,124,800 kwa ajili malazi tu ya Waziri Nahodha.
  "Kwa hiyo ukifanya hesabu kwa mwezi serikali inalipa sh milioni 33.7 kwa ajili ya malazi tu ya Waziri mmoja na hadi sasa ana miezi saba hotelini," kilisema chanzo chetu cha habari.
  Kwa mujibu wa habari hizo, gharama hizo ni mbali ya chakula na huduma zingine hotelini ambazo kwa mwezi ni zaidi ya sh milioni 20, hivyo kufikia kiasi cha sh milioni 50 kwa mwezi.

  Sababu kubwa ambayo inadaiwa na serikali kumfanya waziri huyo aishi hotelini ni uhaba wa nyumba za mawaziri.
  Inadaiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliyepita, Laurence Masha, alikuwa akiishi nyumbani kwake katika kipindi chote alichoshika nafasi hiyo na wala siyo kwenye nyumba ya serikali.
  "Kwa hiyo Nahodha alipoteuliwa kushika wadhifa huo, serikali ikajikuta haina nyumba kwa ajili ya Waziri wa Mambo ya Ndani na hicho ndicho chanzo cha Waziri Nahodha kulala hotelini," kilisema chanzo chetu cha habari.
  Mbali ya Nahodha, kuna mawaziri wengine wanne wanaoishi hotelini kutokana na uhaba wa nyumba za serikali.
  Uchunguzi zaidi unasema kuwa sababu kubwa ya Waziri Nahodha na wenzake kukosa nyumba, ni serikali kuwaacha baadhi ya mawaziri waliotemwa kuendelea kuishi kwenye nyumba za serikali.
  "Kuna waziri alifariki; mjane wake bado anaishi kwenye nyumba za serikali, wapo mawaziri waliotemwa, wameomba wabaki kwa muda kwenye nyumba za serikali, ili wajipange. Hawa wote wameziba nafasi za mawaziri wa sasa," alisema mmoja wa maofisa wa Wizara ya Ujenzi.

  Habari zaidi kutoka ndani ya Wizara ya Ujenzi zimedokeza kuwa Nahodha ilishapata nyumba ya kuishi, lakini alikataa kwa madai kuwa haina ulinzi na samani za ndani.

  Mtoa habari huyo alisema mvutano uliopo sasa ni kuwa kiongozi huyo anataka apewe stahiki hizo kama Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wakati Wizara ya Ujenzi ikipinga jambo hilo kwamba anapaswa kugharimiwa sawa na mawaziri wengine.
  Chanzo hicho kimedokeza kuwa kilimtaarifa Waziri Shamsi kuwa kama anataka samani za nyumba awasiliane na Wizara ya Mambo ya Ndani anayoiongoza ili kuangalia uwezekano wa kupata vitu anavyovitaka.

  Chanzo kingine cha Tanzania Daima Jumatano, kimedokeza kuwa Shamsi, anaweza kupewa huduma hizo kama angeendelea kuwapo Zanzibar na si bara ambako hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri.
  Kilibainisha kuwa SMZ, haina utaratibu wa kuwapangia nyumba na kuwapa huduma mbalimbali ikiwemo ulinzi na wahudumu wa ndani viongozi wake wanaoishi nje ya Zanzibar.


  Kiliongeza kuwa Shamsi, anapata huduma za hadhi ya Waziri Kiongozi kila anapokuwapo visiwani humo lakini anapotoka nje ya mipaka hiyo kwa maana ya kuwa Tanzania Bara, anagharimiwa sawa na mawaziri wengine.
  Alipoulizwa na gazeti hili sababu za Waziri Nahodha kuendelea kuishi hotelini na gharama ambazo serikali inazipata, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ol- Medeye, alisema wizara yake haihusiki na utoaji wa makazi ya viongozi na watendaji wa serikali, bali inahusika kwa Watanzania wote.
  "Suala hili sio la wizara yetu, hatuhusiki kabisa na makazi ya mawaziri wala viongozi wengine wa serikali, tunahusika na makazi ya Watanzania wote," alisema Naibu Waziri huyo.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alipoulizwa kuhusiana na suala la makazi la Waziri Nahodha na wengine, alisema hajui chochote kwani yuko mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti.

  "Mimi sijui chochote, muulizeni Katibu Mkuu ambaye yuko jijini Dar es Salaam, atawapa ufafanuzi," alisema kwa kifupi Dk. Mwakyembe.

  Sakata la Waziri Nahodha kuishi hotelini, liliibuliwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF).
  Mbubge huyo alitoa taarifa zilizomshtua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na wabunge wengine kuwa Waziri Nahodha, anaishi hotelini.
  Kabla ya kutoa kauli hiyo, mbunge huyo alihoji dhamira ya serikali katika kupunguza matumizi.
  Alisema serikali inakusudia kusitisha ununuzi na matumizi ya mashangingi, kuacha kuagiza fenicha kutoka nje na kupunguza posho kama moja ya njia ya kupunguza gharama za matumizi kwa serikali.
  Alisema pamoja na dhamira hiyo ya kubana matumizi, serikali imewaacha baadhi ya mawaziri wake waishi hotelini na hivyo kuongeza gharama za matumizi.
  "Kuna mawaziri wanaishi hotelini tangu walipoteuliwa hadi sasa, serikali haioni kama hali hiyo ni kikwazo kwa mafanikio ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano tulioupitisha hivi karibuni bungenin?" alihoji mbunge huyo.
  Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Pinda kwanza alionekana kushangazwa na taarifa hiyo na baadaye alimtaka ataje majina ya mawaziri anaowajua wanaishi hotelini hadi sasa tangu walipoteuliwa.

  "Naomba Mheshimiwa Mbunge nitajie majina ya mawaziri unaowajua kwamba wanaishi hotelini," alisema Pinda.
  Mbunge huyo ambaye alikuwa akisubiri majibu ya Waziri Mkuu kwa hamu, akataja jina la Waziri Nahodha kwamba ni mmoja wa mawaziri wanaoishi hotelini.
  Huku akiwa haamini na kumwangalia Waziri Nahodha, Pinda alijibu kwa kifupi tu: "Basi nimesikia."

  View attachment 32856 View attachment 32856

  View attachment 32857

  View attachment 32858

  Haya ndio maisha ya mtanzania wa leo baada ya miaka 50 ya uhuru.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,486
  Likes Received: 19,879
  Trophy Points: 280
  hapo ni kilindi
   
 3. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sasa kwa nini waliuza nyumba za serikali za Masaki, Oysterbay na kwingine? Inasikitisha sana ndugu zangu. Zile nyumba lazima sirudi tu ktk mikono ya serikali. Mauzo yote ni batili. Nyie mnaokaa ktk nyumba hizo mjue mko kwa mda na mtakuja lia baadae
   
 4. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Hivi huyu Nahodha ni mtanzania au ni mgeni anatembelea tanzania. Ninadhani yupo Paris bana sio kilindi.
   
 5. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Huyu Mzanzibari..Huku bara ni nchi ya Ugenini!
   
 6. A

  Arsen New Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njia zote wanazotumia mafisadi kupitishia pesa za wananchi zimeanikwa hadharani na wakereketwa kilichopo sasa ni kutumia njia hii. Ninachojiuliza, hawa mawaziri siyo watu kama sisi? labda hawana nyama kama binadamu wengine. Nilibahatika kuiona nyumba aliyojenga hayati baba wa taifa kule butiama kabla Bw. Mkapa hajamjengea nyumba ya kifahari, mbona aliishi bila madhara yoyote na mbona haikumvua heshima ya uraisi? Ipo siku Kikwete, Mkulo na Pinda watatakiwa kuwaeleza watanzania wanakopata hizo pesa za kumlipia Nahodha huku mshahara, posho nk anapata.
   
 7. N

  Ngaywembe Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 25
  jambo la msiki la kujiuliza, pinda ndiye msimsmizi wa seriksli inakauwaje atambui kama baadhi ya mawaziri wamepangishiwa

  hotel, kuna walakini wa maneno ya serikari kuwa na nia kupunguza na kubana matumizi ya serikali yake. Lakini watanzania

  tusisahau kauli ya kwanza ya waziri pinda pindi alipoteuliwa kuwa waziri mkuu kwamba kukamata mafisadi ni kuteteresha

  uchumi wa nchi. Ndio maana leo watanzania tulio wengi tumepoteza tumaini kwa waziri pinda. He is not mtoto wa mkulima

  nay more.
   
 8. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Makubwa!
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ukisema wanasema unachochea vurugu, unavunja amani, amani gani watu hawa wanayo? CCM mmeshindwa kabisa na hata munishi aliimba
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sijui ni suse kuingia JF maana naona ugonjwa wa moyo unani nyemelea
   
 11. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu watanzania hizo nyumba zinazojengwa na shirika la nyumba huko tegeta hazifai kukaa mawaziri jamani. Hizo nyumba wanawajengea akina nani wakati watanzania ni masikini hawawezi kununua? Wanazinunua wao wakubwa halafu wanaziacha wanakuja kupangishiwa mahotelini na bado anapewa shangingi la kuvinjari hapa Dar na kuwasahau wapiga kura wake.
  Huyu Nahodha angeishi huko Zanzibar asingefanya kazi zake kama kawaida tena angekaa karibu na wapiga kura wake ili wampe ulinzi wa kutosha.
  Ili tuinusuru hiyo milioni 50 kwa mwezi tuifunge hiyo barabara ya kuingia huko hotelini. hapo msg itafika kwa Kikwete na huyo Pinda wake. Watanzania acheni uoga.
   
 12. JS

  JS JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Aiseee......lazima atakuwa anapewa na urojo uliotengenezwa spesheli na Hoteli ambayo bei yake itakuwa kama laki hivi bila kusahau halwa halwa ya kunywea gahawa.....................mmmh
   
 13. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Ukizingatia hayo maandishi na picha jinsi zinavyo present hii tanzania duh......uvumilivu basi jamani da.........! tuoneane huruma sisi wamoja. Halafu ukiongea unaambiwa wewe ni mchochezi. Hapa ninampongeza Mh Mboye, Zitto na wengine wote wanaopigania maslahi ya watanzania wote. Hao ndio wanaoitakia Tanzania iwe na amani sio huyu Nahodha. Ukweli utabaki kuwa ukweli hata mbele ya mungu.
   
Loading...