Kweli fedha zimepungua mikononi mwa watu

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Katika Jiji la Mwanza Mitaa inayosifika au kuongoza kwa biashara ni Mitaa ya Liberty na Rwegasore. Kwa kawaida ikifika siku hasa ya Jumatatu Mitaa hii niliyotaja haipitiki kwa urahisi kwa sababu ya msongamano mwa watu wengi wanaotoka mikoa ya Kagera, Mara, Shinyanga hata na Tabora.

Lakini siku ya Jumatatu sikuamini macho yango hasa kwenye Mtaa wa Rwegasore. Wanunuzi wamepungua kwa kiasi kikubwa na ile mikiki mikiki ya watu kununua bidhaa imepungua sana.

Mtaani watu hawapo na wenye maduka naona ukitazama nyso zao wana huzuni sana.

Nilipomuuliza mmoja wao kumuuliza sababu ya hali kutokea akanieleza kwa kifupi tu Acha Ndugu yangu tumuachie Mungu.

Kwa kifupi kuna tatizo na wafanyabiashara wengi aidha hawana mbinu za biashara au kuna tatizo ambalo wanashindwa kulieleza kwa Serikali.
 
Tunapaswa kufanya kweli October la sivyo tutateseka zaidi ngwe ya pili.
 
Chanzo kikuu cha fedha mtaani ni watumishi wa umma na 10%. Sasa mkuu kabana kotekote kwa hiyo lazima mtaani kukauke.
 
Mji umepanuka wewe, masoko kama Makoroboi yapo mengi ila kuhama kwa soko kuu kwa muda pia ni sababu! Angalia pia tarehe zenye wanunuzi wengi...
Acha kuwa biased mkuu!
 
Labda hao walikua wapigaji sasa mianya imezibwa

Aliskika mwanasiasa mmoja akiwajibu
 
Kama watu hawana pesa mifukoni kufanya biashara yoyote ni ku-take risk ya hali ya juu, na ndio hali tuliyonayo sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kutakuwa na shida tu,ila ni shida tayari,kwa kauli yake hiyo ni kuwa HATOSHEKI, sasa si hatari kumkabidhi hazina mtu asiyetosheka? Yeye si alituambia tutosheke na mishahara yetu? Inakuwaje yeye hatosheki?
Hahaha... Kama hadi rais analalamika kutakuwa na shida mahali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom