Kweli CCM Mabadiliko Yanakuja

Kweli CCM Mabadiliko Yanakuja

Tusishangae kama watabambikiwa kesi na kuwekwa ndani kwa miezi chungu nzima kama siyo miaka. Chezeya Malaika Mkuu weye! Hataki kabisa kujaribiwa.
Kina Bashe na Msukuma walijifanya kupinga fikra sahihi za mwenyekiti... wakajikuta wamepelekwa nyumbani kwa Lema kwa muda. Mwenyekiti hajaribiwi...
 
Nikifatilia kwa makini mkutano mkuu wa CCM hapo Dodoma kweli nimeamini chama hicho kimeamua kufanya mabadiliko makubwa. CCM ni chama tulichokizoea kikifanya mikutano yake mikuu kwa mbwembwe na utoaji rushwa kwa wazi, kinyume na hayo wakati huu nidhamu ni hali juu kwa wajumbe.
Mabadiliko makubwa yalihitajiwa kwenye chama hicho ili kukidhi matakwa ya watanzania na ile tabia ya kuonea aibu ilileta madhara makubwa kwenye chama hicho.
Natoa pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu na Halmashuri kuu kwa kuchukua uamuzi mgumu wa kuwaondoa viongozi waliokuwa hawana nia njema na chama hicho. Sasa tusubiri mwaka uchaguzi wa mwaka 2020 tuone chama kipi kitakuwa cha kifisadi, kichaka cha mafisadi ama watetezi wa mafisadi.

Mabadiliko ni muhimu kuondoa mawazo mgando ya baadhi ya viongozi wa chama na serikalini
 
Àluta contina,JPM kaza kamba heshima ya Taifa letu lazima irejee
Kabisa maana kati ya watanzania milioni 46,watanzania laki moja ndo walijipa hatimiliki ya Taifa letu wao ndo walifaidi utajiri wa nchi yetu kwa kutumia nguvu yao na kufisadi nchi yetu,sasa wanaisoma number.Kuna wengine mpaka walidiliki kutengeneza ARV fake na bado wakashinda kesi.Sasa tumepata Rais makini,tumwache ainyooshe nchi yetu.
 
....Fikra potofu za udikteta uchwara! ZIDUMU! CCM oyee! CCM oyee!
Na zitaendelea kudumu,muiteni kama mnavyotaka kumuita,yeye anaendelea kunyoosha nchi.Eti dikteta uchwara wakati dikteta nyangumi mnae kwenye sacosi yenu ,anaebadili gia angani.Mbowe ndo anaeamua nani awe mgombea,aaaaaah jamani jichunguzeni kwanza kabla hamjamnyooshea kidole Rais.By the way ndo Rais ,hata mkimuita majina gani hilo haibadili kuwa yeye ndo Rais
 
Naona mnashangilia jahazi kuzama.kama wafuasi wa kibwetere.
 
shaba haitageuka kuwa dhahabu hata uisugue milele,dhana ya kusafisha ccm ni sawa na kumwaga asali baharini
 
Hivi watu wanaosifia huyu mtu na hili lichama mbona huku mtaani huwa sikutani nao?

Nadhani huwa hampo serious mnafanya tuu kwa ajili ya tumbo na maslahi mengine vinginevyo mngekua mnaonekana na huku field.
 
Hahaha Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo.
Hakuna cha demokrasia wala nini,Mbowe mwenyekiti wa maisha,mkwepa kodi numero uno,huyu kweli ana uchungu na nchi yetu au ni msaka tonge tu?
 
Hongera sana JPM, Mangula na Kinana kwa utendaji mkubwa wenye tija ndani ya CCM. Tunataka CCM inayotumikia Watanzania zaidi,kuliko CCM ya kujinufaisha watu fulani fulani. Tunataka CCM ambayo msingi wake ni IMANI, siyo kupata vyeo,siyo kutoa ajira. Watu wanavyeo 5 wakati wengine hawana hata kimoja. What do you expect. Tunataka CCM yenye nidhamu, siyo iliyofulika wasaliti. Tunataka CCM inayoisimamia vizuri serikali yake. Tunataka CCM yenye sura ya UTENDAJI, siyo utitili wa mikutano isiyo na tija. Changes are inevitable. CCM lazima IBADIRIKE kadiri ya falsafa na mahitaji ya wakati. Katiba ya CCM lazima iendane na mahitaji ya wakati. Hoja: Kazi ya kwanza iwe ni kufukuza wasaliti wote ndani ya CCM.Hili lifanyike bila hofu.
 
CCM ni chama cha taifa. Mabadiliko Yake ndio mabadiliko ya Nchi yote.. Asante magufuli, anayempinga magufuli na CCM mpya hata kwenda Mbinguni
 
JPM kang'oa visiki ...walitaka kuiweka CCM mifukoni mwao

cc: Makongoro Nyerere
 
Back
Top Bottom