Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Nikifatilia kwa makini mkutano mkuu wa CCM hapo Dodoma kweli nimeamini chama hicho kimeamua kufanya mabadiliko makubwa. CCM ni chama tulichokizoea kikifanya mikutano yake mikuu kwa mbwembwe na utoaji rushwa kwa wazi, kinyume na hayo wakati huu nidhamu ni hali juu kwa wajumbe.
Mabadiliko makubwa yalihitajiwa kwenye chama hicho ili kukidhi matakwa ya watanzania na ile tabia ya kuonea aibu ilileta madhara makubwa kwenye chama hicho.
Natoa pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu na Halmashuri kuu kwa kuchukua uamuzi mgumu wa kuwaondoa viongozi waliokuwa hawana nia njema na chama hicho. Sasa tusubiri mwaka uchaguzi wa mwaka 2020 tuone chama kipi kitakuwa cha kifisadi, kichaka cha mafisadi ama watetezi wa mafisadi.