Kwanza tuliambiwa,wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi watachangia kutatua kero za elimu Dar es Salaam,makontena ya vifaa vya ofisini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Hapa ndipo "strong media" na "active citizens" wanatakiwa.

Kwanza tuliambiwa,wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi watachangia kutatua kero za elimu Dar es Salaam,makontena ya vifaa vya ofisini na vitabu yatakuja kutoka ughaibuni.

Baadae tukaambiwa si hayo tu bali na mengine yatatoka China kwa ajili ya maziwa ya watoto waliotelekezwa na mengine yataleta vitabu kwa ajili ya maktaba.
Baada ya hapo tukaambiwa Makontena yamefika yapo 36 yanavifaa vya maofinini kwa ajili ya ofisi za walimu kwa Shule za Dar ES Salaam. Baadae tukaambiwa hayatoki mpala yalipiwe kodi kwani yamekuja kwa anuani ya mtu binafsi.

Baade tukaambiwa,kama TRA watataka yalipiwe kodi,wao na waziri wa fedha watashtakiwa kwa Rais. Baadae tukaambiwa yanapigwa mnada ila yakapungua mpaka 20.

Baadae tukaambiwa atakaeyanunua atalaaniwa. Baadae tukaambiwa,lazima yalipiwe kodi na aliyeyaleta na kama hatalipa yatapigwa mnada.
Baadae tukasikia waziri akisema,kama sheria ya kodi itapindishwa katika hili atakuwa tayari kumuomba Rais aachie ngazi.

Baadae tukamsikia Rais akisema,makontena hayo kwanza yana masofa na lazima yalipiwe kodi. Baadae tukaambiwa mnada utapigwa leo jumamosi.
Baadae tunaambiwa mnunuzi kakosekana.

Na sasa tunaambiwa kuwa kwanza hayo makontena hayana masofa kama tulivyoambiwa na vitu ni vichache sana eti vikipangwa vizuri yatabaki makontena yasiyozidi nane.
Haya mambo hayaaaaaa!
Akili za kuambiwa changanya na za kwako. Ila kaeni mkijua Tanesco wameshindwa kesi ya Standard Chartered na wanatakiwa kulipa Mabilioni ya Shilingi.
Chaguzi ndogo nazo zinaendelea, na pia jueni kuna kundi kubwa la vijana lililomaliza vyuo vikuu, vyuo na kwenye taasisi za elimu ya juu wanasubiri ajira tangu mwaka 2015.
Wasalaaam.
 
Back
Top Bottom