Kwanza katiba au uchaguzi

Wakuletwa

Senior Member
Oct 31, 2010
134
9
Lipi lililo bora kufukuza mamba waliopo mtoni ndio tuogelee au kuogelea na kuwafukuza tukiwa ndani ya mto huo huo. Yes nimelazimika kusema hivyo kwa kuwa tumekubali kuingia katika uchaguzi ilhali tukijua fika kuwa katiba iliyopo haitufai na haiwezi kutupa haki nafikiri sasa tumeshapata somo la kutosha tuhangaikie mabadiriko ya katiba kuanzia sasa ili itakapofika 2015 tuwe tumefikia mahali pazuri. Ni ushauri tu wana JF:peep:
 
Lipi lililo bora kufukuza mamba waliopo mtoni ndio tuogelee au kuogelea na kuwafukuza tukiwa ndani ya mto huo huo. Yes nimelazimika kusema hivyo kwa kuwa tumekubali kuingia katika uchaguzi ilhali tukijua fika kuwa katiba iliyopo haitufai na haiwezi kutupa haki nafikiri sasa tumeshapata somo la kutosha tuhangaikie mabadiriko ya katiba kuanzia sasa ili itakapofika 2015 tuwe tumefikia mahali pazuri. Ni ushauri tu wana JF:peep:
Support. Agenda kuu kuanzia sasa iwe ni mapambano ya kupata Katiba mpya. CHADEMA iongoze mapambano hayo. Kenya kila mtu alichangia kuanzia NGOs, Viongozi wa kidini, wanasiasa, wanafunzi, n.k. Tatizo la waTz serikali ikikataa jambo au kutishia kidogo wote tunanywea na wengine hawachelewi kuanza ngonjera za 'amani na utulivu,. Kwenye mapambano kuna kuumia. Huwezi kupata unachotaka kwa huruma ya anayekunyima.
 
Ni muhimu sana kupata KATIBA MPYA kabla ya kuingia kwenye uchaguzi ujao wa 2015.
Tukipata katiba mpya tutaweza kupata TUME HURU YA UCHAGUZI, TAKUKURU HURU na UCHAGUZI HURU KUANZIA 2015 na mambo haya ya uchakachuwaji yatapotea kabisa. Pia chini ya Katiba Mpya tutaweza kumuadabisha hata Rais akienda kinyume na Katiba. Kwa Katiba ya sasa Rais aliye madarakani na wale wastaafu hawawezi kushitakiwa hata kama anafanya/walifanya udikiteta wakiwa madakani

Tusije tukajidanganya kufanya uchaguzi bila kuwa na Tume huru ya Uchaguzi; kwani CCM na vibaraka wao Tume ya sasa ya Uchaguzi (NEC) wataendelea kuchakachuwa kura.

Wenzetu wakenya wamepata KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHAGUZI NA TAASISI HURU YA KUZUIA RUSHWA na mambo yao yanaenda vizuri kwa sasa. Mafisadi wote wanapelekwa mahakamani chini ya Katiba Mpya bila kujali cheo cha mtu.

Swala hili la KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCAGUZI na TAKUKURU HURU ni kwa faida ya kila mtanzania na ni lazima mtanzania yeyote mwenye uchungu na raslimali za nchi yake, anayeweka maslahi ya Taifa mbele lazima avipiganie hivyo. Naomba vyama vya SIASA vya Upinzani na ASASI ZA KIRAIA vituongoze katika hili. Kama wakitaka kuandamana "We are more than ready to do that" (Tupo zaidi ya tayari kuandamana kwa ajili ya Katiba mpya)

CCM hawako tayari kuandaa mkutano wa Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi inabidi wananchi tuwashinikize kwani wanataka waendelee kuchukuwa raslimali za nchi kwa manufaa yao. Nadhani unakumbuka walivyofanya EPA, RICHMOND, BUZWAGI, MEREMETA, IPTL na mikataba mingine mingi (listi ni ndefu).

Watanzania tuamke tuwe tayari bila kujali itikadi ya chama kuyapiganiya hayo kwani ni kwa maslahi ya watanzania wote na KIZAZI KIJACHO!!!!!!!!
 
Lipi lililo bora kufukuza mamba waliopo mtoni ndio tuogelee au kuogelea na kuwafukuza tukiwa ndani ya mto huo huo. Yes nimelazimika kusema hivyo kwa kuwa tumekubali kuingia katika uchaguzi ilhali tukijua fika kuwa katiba iliyopo haitufai na haiwezi kutupa haki nafikiri sasa tumeshapata somo la kutosha tuhangaikie mabadiriko ya katiba kuanzia sasa ili itakapofika 2015 tuwe tumefikia mahali pazuri. Ni ushauri tu wana JF:peep:

Nakumbuka mtazamo wa wasomi wengi wakati wa kuanza kwa mfumo vyama vingi ulikuwa ni kuanza na kuwafukuza mamba mtoni kabla ya kuingia kuogelea. Mimi naamini kuwa huu ndio mtazamo sahihi. Lakini wanasiasa wengi wa upinzani wakati huo walikuwa na mtazamo kuwa unaweza kuogelea mamba wakiwemo mtoni na ukafanikiwa kuwafukuza. Hii ilitokana kwa kiasi kikubwa na msimamo wa chama tawala wakati huo na hata sasa kuwa hakuna umuhimu wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Wapinzani hawakujua kuwa ukishaingia kwenye mto wenye mamba lazima uchague moja ama kuwafukuza mamba au kuogelea. Na ukichagua moja kati ya hizo basi jingine haitafanyika kwa ufanisi unaotarajiwa. Ukiamua kufukuza mamba hutaogelea na unaweza kuzama na ukiamua kuogelea hutafika kwani mamba watakutafuna.

Sasa ni wakati muafaka kuangalia upya mikakati ya kuandika katiba mpya, kuunda tume huru ya uchaguzi, na mfumo mzuri wa usimamizi wa uchaguzi kuanzia kuandikisha wapiga kura, kuandaa vituo vya kupigia kura, kusimamia upigaji kura, kusimamia uhesabuji wa kura na hatimaye utangazaji wa matokeo. Bila hivyo wapinzani watakuwa wameula wa chuya tena watakapoingia kwenye uchaguzi wa 2015 na katiba hii hii, tume hii hii, sheria hizi hizi za uchaguzi, wasimamizi hawa hawa, polisi hawa hawa ................................
 
will it be possible! katiba iliyopo inawasupport ccm na wana more than 70% seats in the parliament, i also thought of that but i almost cried after remembering the fouls the ccm play in their branch NEC
 
sitegemei maajabu tofauti na haya tunayoyaona kama katiba haitabadilishwa!huu ndo wakati wa kuanza mchakato wa kudai katiba mpya!
sikiliza wadau!
katiba tuliyonayo ilianza miaka ya 1977 na kamati iliyotengeneza hii katiba ndo hiyo hiyo iliyotengeneza katiba ya ccm chini ya bwana thabit kombo!
ni dhahiri kuwa hii katiba haikidhi matakwa ya watanzania tulio wengi bali wanaccm

haiwezekani raisi akawa na mamlaka kama
1.kumteua waziri mkuu
2.jaji mkuu
3.mwanasheria wa serikali
4.mkuu wa majeshi
5.mkuu wa polisi
6.wakuu wa mikoa yote.(tuna mikoa mingapi?)
7.wakuu wa wilaya (tuna wilaya ngapi?)
8.wakurugenzi wa mashirika ya serikali (tuna mashirika mangapi)
9.kupandisha vyeo maafisa wa jeshi
10.kuteua wabunge kumi
11. kuteua mawaziri
12.mwenyekiti wa nec
na mengine kibao haya ni baadhi!
haya aliyaweza mwl kwa kuwa kichwa chake kilikuwa hakijachakachuliwa
.
lets us stand up guys na tudai haki yetu ili huu udharimu tuukomeshe!2015 its gonna be a year of victory
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom