Kwann watu wanaidharau degree ya Open University?

Kihistoria, kupata digilii ilikuwa dili sana. Yaani mtu mwenye nayo angejulikana kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba kadhaa. Taasisi za umma zilikuwa zikigombea wenye nazo hata kabla hawakuhitimu. Haikuwa ajabu mhitimu kuwa na barua tatu nne za taasisi za umma zikimtaka akaripoti kwao.

Kupata digilii ilikuwa ni kwa wachache. Wilaya nzimanzima zilikuwa zinatoa wanafunzi wachache "waliopasi" kwenda sekondari. Huko sekondari, wachache zaidi walichaguliwa kwenda sekondari ya juu. Kutoka huko sekondari ya juu, ni wachache sana waliochaguliwa kwenda kusoma digilii "Chuo Kikuu".

Ndio. Haikuhitajika kutaja jina la chuo. "Msimuone vile, jamaa anasoma Chuo Kikuu!!1!" Mkuu wa nchi ndiye aliyekuwa Mkuu wa Chuo.

Vyuovyuo vingine vilivyotoa elimu ya juu havikuruhusiwa kutoa digilii. Vilitoa "Diploma ya Juu" ambayo wenyewe walisema "ni sawa tu na digilii". Lakini wenzetu wa Chuo Kikuu hawakuwa wanatambua hilo la usawa. Baadhi ya kozi ilikuwa ukienda na Diploma yako ya Juu, hukupokelewa kusoma digilii ya Mastaz. Salama yako ilikuwa ukasome nje ya nchi walikokuwa wakitambua Diploma za Juu.

Nafikiri umepata picha kuhusu digilii ilivyokuwa dili.

Sasa mning'inio wa mawazo ya hivyo bado uko. Mtu akisoma digilii ya chuo kingine ambacho siyo "Chuo Kikuu", huonekana kutiliwa shaka hiyo digilii yake. Ndio utaona wengine wanaviita baadhi ya vyuo kuwa ni "vya kata". Dhana nzima ya chuo kuwa "cha kata" ni ileile: ilikuwa dili sana kusoma sekondari, hasa "ya kupasi". Zamani hizo kwamba ulisoma sekondari "binafsi" ilikuwa ni ushahidi kwamba wewe "hukupasi", na kwa hiyo siyo wa "viwango" kama wale waliokuwa shule za "kupasi", yaani za serikali.

Zilipokuja shule za kata, yaani kila kata iwe na shule ya serikali "ya kupasi", wanafunzi wengi walipata fursa ya kupata elimu ya sekondari. Na hivyo ile kujitutumua kwamba "nimepasi" iliisha.

Kuibuka kwa vyuo vingine vingi vinavyotoa digilii kulisababisha kupungua kwa makali ya kusema "niko Chuo Kikuu", kwa vile sasa ulianza kuulizwa, "Chuo Kikuu Kipi?"

Ndipo kikaja Chuo Kikuu Huria. Huria kwenye jina la Chuo Kikuu haliko kwa urembo. Lina maana chuo kikuu ni huria -- mtu yeyote apendaye kujiunga nacho anakaribishwa. Bila kujali kasoma kiasi gani. Bila kujali ana cheti cha kidato cha nne au cha sita. Mradi tu awe na nia (na ada!) ya kusoma. Walau ndivyo vilivyo vyuo vikuu huria vingine duniani.

Zamani, ili ujulikane "umepasi" kwenda sekondari, mara nyingi ni kwa vile sasa utapanda basi kwenda shule ya kutwa au ya bweni... Mning'inio wa mawazo kama hayo upo kwamba, ili ujulikane unasoma "Chuo", inabidi uwe uko "kampasi" au umepanga "geto"; unachukua "bumu". Sasa digilii gani unaweza kuchukua bila kukaa kampasi? Nini sasa faida ya kwenda "chuo"?

Hata kama digilii za vyuo vya matofali nyingine baadhi ya wanafunzi ni wavivu na wazembe, waishiao kutumia "madesa" yaliyopitwa na wakati, hujiona ni bora kuliko wale wa huria ambao inabidi wasome kweli mpaka wapate digilii zao.

Ndugu yangu, kwa kifupi mawazo-mgando ndiyo sababu ya kudharaulika kwa digilii za Chuo Kikuu Huria.

Yapuuze.

Angalia:

Mkuu, hv tofauti ya advanced diploma na diploma ni ipi.? Kwa hapa Tanzania kuna advanced diploma.?
 
Best comment

Pamoja na Uchambuzi wako wa kisomi nashangaa neno degree/digrii limekushinda kabisa

Btw uzi umeishia hapa, hakuna kilaza wa chuo chochote anayejiona bora ataendeleza mjadala
Kwa nilivyo msoma sidhani kwamba limemshinda, nadhani amelitumia kwa makusudi kabisa labda tu kwa kuwa hakuliwekea quotation ('digilii').
 
Yes utofauti upo kati advance diploma & diploma, advance diploma inahadhi sawa na degree na kiukwel ukikuta mtu mwenye advance diploma yupo nondo kuliko mwenye bachelor degree
Bc ndo maana mm nimepigwa chini kwenye ajira portal kwenye kaz flan hv
 
Kihistoria, kupata digilii ilikuwa dili sana. Yaani mtu mwenye nayo angejulikana kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba kadhaa. Taasisi za umma zilikuwa zikigombea wenye nazo hata kabla hawakuhitimu. Haikuwa ajabu mhitimu kuwa na barua tatu nne za taasisi za umma zikimtaka akaripoti kwao.

Kupata digilii ilikuwa ni kwa wachache. Wilaya nzimanzima zilikuwa zinatoa wanafunzi wachache "waliopasi" kwenda sekondari. Huko sekondari, wachache zaidi walichaguliwa kwenda sekondari ya juu. Kutoka huko sekondari ya juu, ni wachache sana waliochaguliwa kwenda kusoma digilii "Chuo Kikuu".

Ndio. Haikuhitajika kutaja jina la chuo. "Msimuone vile, jamaa anasoma Chuo Kikuu!!1!" Mkuu wa nchi ndiye aliyekuwa Mkuu wa Chuo.

Vyuovyuo vingine vilivyotoa elimu ya juu havikuruhusiwa kutoa digilii. Vilitoa "Diploma ya Juu" ambayo wenyewe walisema "ni sawa tu na digilii". Lakini wenzetu wa Chuo Kikuu hawakuwa wanatambua hilo la usawa. Baadhi ya kozi ilikuwa ukienda na Diploma yako ya Juu, hukupokelewa kusoma digilii ya Mastaz. Salama yako ilikuwa ukasome nje ya nchi walikokuwa wakitambua Diploma za Juu.

Nafikiri umepata picha kuhusu digilii ilivyokuwa dili.

Sasa mning'inio wa mawazo ya hivyo bado uko. Mtu akisoma digilii ya chuo kingine ambacho siyo "Chuo Kikuu", huonekana kutiliwa shaka hiyo digilii yake. Ndio utaona wengine wanaviita baadhi ya vyuo kuwa ni "vya kata". Dhana nzima ya chuo kuwa "cha kata" ni ileile: ilikuwa dili sana kusoma sekondari, hasa "ya kupasi". Zamani hizo kwamba ulisoma sekondari "binafsi" ilikuwa ni ushahidi kwamba wewe "hukupasi", na kwa hiyo siyo wa "viwango" kama wale waliokuwa shule za "kupasi", yaani za serikali.

Zilipokuja shule za kata, yaani kila kata iwe na shule ya serikali "ya kupasi", wanafunzi wengi walipata fursa ya kupata elimu ya sekondari. Na hivyo ile kujitutumua kwamba "nimepasi" iliisha.

Kuibuka kwa vyuo vingine vingi vinavyotoa digilii kulisababisha kupungua kwa makali ya kusema "niko Chuo Kikuu", kwa vile sasa ulianza kuulizwa, "Chuo Kikuu Kipi?"

Ndipo kikaja Chuo Kikuu Huria. Huria kwenye jina la Chuo Kikuu haliko kwa urembo. Lina maana chuo kikuu ni huria -- mtu yeyote apendaye kujiunga nacho anakaribishwa. Bila kujali kasoma kiasi gani. Bila kujali ana cheti cha kidato cha nne au cha sita. Mradi tu awe na nia (na ada!) ya kusoma. Walau ndivyo vilivyo vyuo vikuu huria vingine duniani.

Zamani, ili ujulikane "umepasi" kwenda sekondari, mara nyingi ni kwa vile sasa utapanda basi kwenda shule ya kutwa au ya bweni... Mning'inio wa mawazo kama hayo upo kwamba, ili ujulikane unasoma "Chuo", inabidi uwe uko "kampasi" au umepanga "geto"; unachukua "bumu". Sasa digilii gani unaweza kuchukua bila kukaa kampasi? Nini sasa faida ya kwenda "chuo"?

Hata kama digilii za vyuo vya matofali nyingine baadhi ya wanafunzi ni wavivu na wazembe, waishiao kutumia "madesa" yaliyopitwa na wakati, hujiona ni bora kuliko wale wa huria ambao inabidi wasome kweli mpaka wapate digilii zao.

Ndugu yangu, kwa kifupi mawazo-mgando ndiyo sababu ya kudharaulika kwa digilii za Chuo Kikuu Huria.

Yapuuze.

Angalia:

Ufafanuzi mzuri sana.
Ahsante na Hongera sana.
 
Aisee hili susla la kuidharau degree ya OUT kwa kiasi flani lina ukweli! Mie mwenyewe nilitaka kwenda huko ili niendelee na mishe zangu za pesa huku nikipiga kitabu. Aisee kuna uncle wangu mmoja akaniambia ukisoma huko utakuja jilaumu kwamba bora pesa yote uliyolipa ungeinvest kwenye bussiness! Ni kweli kuna watu wameshasoma huko toka miaka mingi mpaka leo wanasotea ajira, ni kila unakokwenda ukikarimiwa sana utaambiwa uache namba ya simu, alafu inakuwa imetoka!
 
Kuna mawaziri wamesoma open, na kuna waliosoma vyuo vikuu vingine hawana ajira miaka nenda rudi
 
Aisee wewe unayebisha jaribu kufanyia experiment wewe mwenyewe au peleka ndugu au mtoto wako huko alafu akihitimu anza kuzunguka nae kutafta employment ndo utajua ukweli ulivyo nina hakika hata mtoa post yuko positive zaid kwenye disadvantage ya kusoma OUT!
Hicho chuo wanaosoma kwa mafanikio ni watu ambao tayari wana employment sasa anataka kurefusha kimo cha elimu lakini sio eti umetoka zako faorm six alafu ukajipeleka huko badae uje utegemee soko la ajira likubebe, umepotea aisee!
 
Hata kwenye kufanya kazi walomaliza huko Wengine utakuta ni wazito sana kujifunza na kuelewa kazi na kuifanya under less supervision!
 
Open University ni elimu ya kisasa inayotufaa sisi wazee ambao hatutaki kuacha majukumu mengine.

Yaani ninasoma wakati ninalinda ajira yangu. Hii ndio njia ya kisasa. Elimu sio ugomvi. Yaani utoke Mbozi kwenda kusoma Arusha chuo cha Makumira, unaacha kazi, mke na watoto hizo akili au matope? Tena degree yenyewe ualimu wa Kiswahili na History teh teh teh
 
Hakuna anaye wadharau ni wewe tu unafeel inferior kwa kuhisi unadharauliwa
 
Hello Habarini za wanajamii forum?

Nahitaji kusoma degree ya Bachelor of science in Energy Resources Open University kwa anaefaham namna ya usomaji wa masomo ya science katika chuo hiki anisaidie maana kwa sasa mimi ni muajiriwa na nahitaji kusoma hii degree!
pia Advance nilisoma EGM na O-Level nilifaulu vizuri tu masomo ya science ila wamesema watanipokea angali Advance sikusoma Physics!
Swali je kuna uwezekano wa kuperform vizuri kama adavance sikusoma physics?

Msipuuze wadau nategemea sana mawazo na ushauri wenu asanteni sana.

asanteni sana kwa msaada wenu wa mawazo.
 
Inasemekana vilaza wakijasoma huko huwa na uhakika wa kufuzu masomo yote!
si kweli. nawafah ma officer wakubwa serikalini. vyombo vya ulinzi na baadhi ya mawaziri waliosoma open.
ndio kusema ni vilaza... sidhani.
 
Back
Top Bottom