Kwanini Zanzibar wanaweza Tanganyika mshindwe mna nini ?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,921
3,801
Nauliza tu, inakuwaje Upinzani Zanzibar wanaweza kuisakama Serikali tu maximum na tunaona mpaka Raisi Hussein inabidi aonekane kwenye vyombo vya habari kujielezea mwenendo wa serikali yake?

Ukija kwenye Muungano WaZanzibari wanarapu kwa sauti kuu na hueleza kila kitu kwa weledi na mwenye kutaka kuelewa huelewa.

Kivyama ACT Zanzibar wakizungumza utapenda uwasikilize namna wanavyobanjua hoja kiutaifa zaidi kuliko kimaslahi ya kichama.

Tanganyika Vyama vingi vinajitetea kimaslahi na havipo katika hoja za kitaifa, jambo ambalo ni tofauti Zanzibar wanaweza na wameweza hadi kufikia kuipigisha magoti serikali na kukaa mezani kuyazungumza mambo yao Kitaifa zaidi.

Je viongozi wa vyama vya upinzani na hata wasio vya upinzani wanashindwaje kuivalia njuga serikali katika mambo mengi tu ambayo hayaendei sawa? Kisiasa mikutano hakuna hadi leo, mnashindwa wapi?

Hata WaZanzibari wanaweza, au hapa Tanganyika vyama vipo kibinafsi zaidi, kiukabila zaidi kuliko ilivyo Zanzibar.

Zanzibar wanaweza kukiwasha na imeshatokea, na inatokea kwa sababu viongozi wapo kitaifa na kizalendo zaidi hakuna aliekimbia kuelekea uhamishoni, wanaamini fimbo ya mbali haisaidii.

WaTanganyika changamkeni msikimbie nchi katika kuwatetea wananchi, kudai katiba na kufuatilia ubadhirifu ndani ya ripoti za mkaguguzi wa mahesabu.

Ukiangalia huku wanakimbizana wengine wanafukuzana na kina mdee na kuzifanya ndio ishu za kitaifa kwa wananchi.
 
Tofauti ni baada ya nchi hizi mbili kupata uhuru, Zanzibar ilifuata mfumo wa vyama vingi, Tanganyika ilifuata mfumo wa chama kimoja. Nyerere (mzanaki) na Karume (mnyasa) ndiyo waliuwa demokrasia ya Wazanzibari lakini tayari demokrasia imeshaota mizizi Zanzibar kuliko bara.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom