Kwanini wengi hawakutani na fursa jf?

Kwanini wengi hawakutani na fursa jf?

bereng

Senior Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
114
Reaction score
21
Wadau, Napenda ``kushare`` nanyi jambo hili. Humu JF kuna fursa nzuri sana ambazo huwa zinatolewa na watu. Lakini sio wote wenye fikra au mtazamo sahihi. Kuna wengine inapotolewa fursa watu `wanacomment` vile wanavyojua wao. Matokeo yake watu wengine wanakatishwa tamaa na kushindwa kufuatilia ile fursa. Kumbe pengine ilikuwa ni fursa ya maana ambayo ingemsaidia mtu.
Mimi nilishawahi kukutana na mtu alikuwa ameweka tangazo la fursa, lakini kuna watu walikuwa `wamecomment` vibaya sana. Ila nilifuatilia nikagundua ni kitu kizuri ambacho kimegusa maisha yangu kwa kiasi kikubwa sana. Napenda kuwashauri wenzangu mnaotaka fursa, ukiona jambo zuri fuatilia ili upate uhakika na maelezo ya kutosha kutoka kwa muhusika badala ya kukata tamaa kwa mawazo ya wengine ambao pengine hawajui hilo jambo au hawana mtazamo sahihi kuhusiana na hilo jambo.
 
Back
Top Bottom