Kwanini waziri alitaka kuifuta tawiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini waziri alitaka kuifuta tawiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 1, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 1, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  HIVI NI KWANINI WAZIRI ALITAKA KUIFUTA TAWIRI  Utangulizi:


  TAWIRI ni taasisi ya utafiti ya wanyama pori iliyo anzishwa kwa mamlaka ya bunge Mwaka 1980, kwa jukumu la kufanya, kusimamia na kuhakiki shughuli zote za utafiti wa wanyama pori nchini na kuishauli serikali katika matumizi endelevu ya wanyamapori nchini.


  Hata hivyo utafiti wanyamapori kama ulivyo utafiti wa vitu vingine duniani ni zoezi ghali kutekelezeka na hivyo huhitaji gharama kubwa za kifedha au vifaa kama vile ndege, computer, maabara, magari na wataalam. Ndio maana fani hii imeingiliwa sana na wenzetu waupe na imekuwa ikifaidisha wazungu na watanzania wachache sana waliokosa uzalendo, ambao wanaamua kuwasaidia wazungu watumie jina la taasis na matatizo yaliyoko katika sekta ya utafiti wanyama pori kuombea fedha za miladi kutoka kwa wahisani mbalimbali duniani kwa malengo ya kuwaboresha wazungu na vibaraka hao wachache. Taasis imekuwa ikitegemea ruzuku kutoka serikalini na hivi punde wadau kama Ngorongoro na TANAPA wamekuwa wakiichangia fedha za kujiendesha ingawa kishingo upande kwa kutokuona dhamila ya dhati ya uwajibikaji wa taasis hii.Wazungu wamepewa uhuru wa kuvunja sheria kama vile kusafirisha wanyama na samples za utafiti nje ya nchi bila kuwa na kibali cha serekali ila cha vibaraka.


  Pamoja na nia nzuri ya serikali kuanzisha chombo hiki, baadhi ya NGOs zinazoendeshwa na wazungu (kama Borner, Packer, Sinclair, Sara Durant, Sara Clevaland, na wengine) kwa kipindi kirefu wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha kuwa utendaji wa chombo hiki unalegalega kwa faida zao. Taasis imara kwao maana yake wao hawatafanikiwa na kupeta katika nyanja hiyo. Hali hii imechangiwa sana na kundi hili kuwa na nguvu kubwa kiasi hata cha kuichagulia serikali pasipo serikali yenyewe kutambua au kutokuwa makini kuwa ni nani wanayemtaka (mamluki) kuwongoza, sio taasis ya TAWIRI tu bali hata idara ya wanyamapori, TANAPA na Ngorongoro hata bila kujali uwezo wa mtu katika kusimamia na kutekeleza sera za wizara. Ili mradi ni mtu wao au wanayeweza kumyumbisha kirahisi.


  Tumeshuhudia viongozi wa juu wa TANAPA, Ngorongoro na hata Idara ya wanyama pori wakikumbana na misukosuko isiyokuwa na kifani ambayo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na hawa wazungu. Wameigawa TAWIRI katika vipande vipande kadha ili kuweza kuibaka taasis vizuli na kuifanya isiweze kufikia kiwango chake cha utendaji. Ndani ya TAWIRI kuna CIMU inayosimamia na Borner kwa mbali (remote), Kuna canivora inaendeshwa na Sara Durant, kuna mradi wa Siclair unaosimamiwa na Mduma na watafiti wawili wengine wa Kitanzania licha ya wote watatu kulipwa na hazina, kuna kituo cha Gombe ambacho kiko chini ya Jan Godhall mia kwa mia. Kituo cha Mahale kimekuwa chini ya taasis ya TANAPA kwa zaidi ya miaka saba kama vile TAWIRI haina wataalamu wa kukisimamia. Sasa hivi kituo hiki licha ya kuachiwa na TANAPA hakina kitu wala kiongozi. Ni juzi juzi tu mladi wa Savanna forever wa Packer ulikuwa uingizwe kinyemela TAWIRI kwa mtindo huo lakini tushukuru wazalendo fulanifulani waliosaidia kuwatonya wakubwa wa wizara. Kwa kufanya hivo ilibidi waandamwe na management kiasi cha kutafuta ajira mbadala sehemu nyingine. Mishahara na marupurupu kwenye vijitengo hivi hutofautiana kwa kiasi kikubwa mpaka imepelekea manunguniko kuwa TAWIRI kuna watumishi wa aina mbili kuu: wa kawaida na wa United Nations! (UN). Kikubwa katika mfumo huu unaobarikiwa na viongozi wa Taasis ni kuwa NGUVU KUBWA YA SERIKALI INAYOINGIA KWENYE TAASIS inawanufaisha mamluki wa Kitanzania na wazungu basi!! Hakuna anayekemea, kukaripia, wala kununa wala kupiga kelele.


  Kwa kuwa haielewi ni kwa kiasi gani serikalii na vyombo husika wanalielewa jambo hii ndio maana tumesukumwa na hisia za kizalendo kubainisha yafuatayo kwa watanzania wenye uchungu na nia njema na mali asili ya nchi hii na kwa vizazi vijavyo.


  1.Utawala wa kuanzia 2000 -2005


  Hali ya uongozi katika taasis hii ilianza kulegalega na hatimaye kuteteleka kipindi cha uongozi wa kiongozi aliyekuwepo kipindi hiki. Hii inatokana na ukweli kwamba wakati kiongozi huyo alipofika alikuta fedha nyingi za wafadhili kama NORAD, DARWIN na JICA ndani ya taasis zilizo tafutwa na kiongozi aliyemtangulia. Ni kipindi hicho Taasis ilifikia kiwango ambacho ilionekana kuwa na mwelekeo wenye matumaini. Hata hivyo alichokifanya kiongozi huyo ni kuwapanga watumishi kwa mtindo wa kupangua na kupanga timu yake ya kufanya nayo kazi. Katika pangua panga hii watumishi kadhaa waliikimbia taasis na wengine ni majeruhi hadi leo. Kama vile ilikuwa ni ajali ya kihistoria ya kiongozi huyo kulamba bingo ya kujikuta ghafla ameteuliwa kuwa mkuu wa taasis hii, na kwa kuwa alikuwa hajawahi kuongoza hata timu ya watu watano katika maisha yake alianza na kutokujiamini na kufanya kazi kwa kubahatisha huku akikodi afisa Utumishi wa nje ya taasis kwa fedha nyingi kumwelekeza namna ya kuongoza na kufisadi. Pamoja ni msaada wa afisa Utumishi huyo ambaye ilikujajulikana kuwa ndugu yake wa karibu, mkurugenzi huyo ilibidi aanze kwa kujikweza, kujisifia, kutaka kutukuzwa na kuchukia kushauriwa au kukosolewa na watumishi ndani ya taasis. Wazungu wasio itakia Taasis mambo mema hupenda watu wa namna ya mkurugenzi huyo na waliendelea kumsifia na kumpa vitu na kumpotezea mwelekeo na wao wazungu kufaidika kwa udhaifu huo. Udhaifu wa namna yake ulipelekea mkurugenzi huyo kulazimisha utukufu uliopelekea kukidhiri kwa ufisadi usiokuwa na kifani. Hayo yaliambatana na kuajiliwa kwa watu wasio kuwa na sifa au hata kuhitajika katika muundo wa taasis pasipo kufuata taratibu, kanuni na sheria. Cha pili alichojitahidi kufanya ni kufuta rekodi nyingi za nyuma za taasis zilizokuwepo kabla ya yeye kuajiliwa (kuchoma kumbukumbu muhimu) na kuanza utaratibu wake usiokuwa na mkia wala kichwa ili histori ionekane mambo mazuri ya taasis yalianzia kipindi chake wakati ni kinyume chake kwa nyuzi 180.


  Miongoni mwa kazi ambazo fedha za wafadhili hawa zilipaswa kufanya ilikuwa ni kujenga jengo la ofisi kuu na maabara ya kisasa (DNA lab) pale Njiro. Cha kushangaza ni hadi leo hii fedha zote zilikwisha majengo hayakukamilika ni yamebaki magofu yenye nyufa za kutisha kuanzia sakafuni mpaka ukutani, huku magorofa na mabangaluu yakijengwa Njiro kama uyoga na wahusika na wasimamizi wa fedha hizi. Hakuna wakukemea wala kukalipia, wala aliyenuna huku Bodi inapigwa chenga na kudanganywa. Hali hii iliwahi kuwafedhehesha wafadhili hasa jinsi mradi wa NORAD ulivyokuwa ukitekelezwa na TAWIRI wakati wa kiongozi huyo. Walifikia hatua ya kusema endapo meneja wa mladi hangeondolewa yaani Samwel Bakari basi fedha zao zitasitishwa.


  Katika uchunguzi uliofanywa na mtaalam kutoka NORAD ulibaini ubadhirifu mkubwa wa fedha za mradi zilizoishia kwenye mifuko ya watu kama ilivyobainishwa na gazeti la Sunday Citizen la tarehe 17 Augusti 2008. Hakuna wa kununa au angalau kukaripia, ilifikia mahali mitaani watu wakawa wananongónezana kuwa ukitaka hela ya haraka haraka za kujichotea bila mikwara uingie TAWIRI.


  Utendaji wa kiongozi huyu haukuwa kero kwa wafadhili tu ila hata Bodi ambayo katika vikao kadhaa waliikemea, kitu ambacho kililetea yeye kutofautiana na Bodi kwa kiasi kikubwa. Hii ilimsababishia aone kiti cha ukurugenzi ni msalaba bola atafute njia ya kutoka na ndipo akakimbilia Shinyanga kwenye ubunge. Na kabla ya kuondoka aliajili na kuwapanga watu ambao aliamini kuwa wangemsaidia kuficha maovu aliyokwisha yafanya. Hii ilikuwa sambamba na kuchoma na kuhalibu nyaraka muhimu kwa mara ya pili na kama kuna kosa kubwa aliloitendea TAWIRI ni kumwachia Mduma ofisi kukaimu ofisi ya serikali wakati alikuwa sio mwajiliwa wa serikali wala taasis bali alikuwa mwajiliwa wa NGOs za wazungu (Boner na Sinclaer). Pamoja na kusomeshwa na serikali hadi degree ya PhD ili akafundishe UDSM aliweka uzalendo pembeni akaajiliwa na wazungu kitendo ambacho wengi walikiona kama usaliti kwa nchi.

  Katika ajira ya Mduma TAWIRI kulifanyika mchezo mchafu ambapo waliweza kumpatia balua ya ajira ya TAWIRI iliyoonyesha kwamba alikuwa ameajiliwa tangu miaka ya nyuma. Utata huu wa ajila unajionyesha kwenye Mishahala yake, ambao hadi leo hii analipwa Mishahal a mitatu: i) kutoka kwa Borner, b) kutoka kwa Sindair na c) kutoka hazina. Hakuna wakukemea pamoja na kwamba hali hiyo imefahamika na wengi. Mshahara wake kwa mwezi kwa mpangilio huo unazidi Tshs 10,000,000/= ukijumuisha na safari za mara kwa mara kana kwamba hakuna wengine wenye stahiki ya kusafili. Pia pamoja na kuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi mkuu amemweka kibalaka wake Maliti kukaimu nafasi aliyokuwa ameshikilia ya mkuu wa kitengo cha CIMU. Huyo Maliti ameegeshwa CIMU ili kuendeleza kufisadi marupurupu waliojiwekea kwenye kitengo cha CIMU na kufisadi fedha za wadau, mipango ambayo hufanyika jumamosi na jumapili au usiku (kuchola line).

  Baada ya NORAD kusema kuwa wangesitisha ufadhili kwa TAWIRI kama Samwel Bakari hangeachia ngazi ambaye ni shwahiba mkubwa wa kiongozi wa 2000-2005, kiongozi huyo aliamua kumwajili ndugu yake (Julius Keyyu) kama meneja mpya wa mradi wa NORAD. Keyyu aliajiliwa ili aweze kuficha maovu ya Samwel na huyo kiongozi na pia kufanikisha kuendelea kufuja pesa za taasis bila kikwazo. Kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa kwenye taasis Keyyu ana nyumba Njiro, magari yasiyopungua matatu na tayali ameshawaajili ndugu zake wasiopungua watatu kwenye ngazi za juu baada ya kuchagulia kuwa mkurugenzi wa utafiti wa TAWIRI badala ya Sabuni.

  2. Utawala wa 2005-mpaka sasa

  Kama ilivobainishwa awali ni vyema ikumbukwe kuwa Mduma alisomeshwa na serikali hadi PhD lakini kwa mshangao wa wengi na kwa kukosa uzalendo badala ya kuja kulifanyia taifa kazi angalau kwa muda aliamua kuajiliwa na wazungu (Borner na Sindair) ambao hawajawahi kuwa na mapenzi na taasis. Kibaya zaidi Mduma aliachiwa ofisi ya serikali akitokea kwa watu binafsi. Kimsingi lilikuwa chaguo lilililazimishwa na ufisadi wa kiongozi aliyekuwa anaondoka uliopewa baraka na hao wazungu. Haingii akilini mtumishi asiyekuwa ameajiliwa au serikalini au kwenye taasis zake anaachiwa ofisi ya serikali. Hata hivo mwelekeo wake ni wa kuendesha taasis hii ya umma kama shirika la mtu binafsi. Mpangilio huu kamwe hauwezi kuwa na maadili na tija kwa taasis wala kwa taifa bali kukidhi mahitaji ya hao watu binafsi. Kutokana na aina hii ya uongozi taasis sasa imeshindwa kutekeleza majukumu yake ya msingi kama ifuatavyo:

  1.Utafiti- jukumu kuu la taasis ni utafiti. Taasis imeshindwa kusimamia na kutekeleza kazi za utafiti, kuandika ripoti za sensa za wanyama, kushauri serikali na hii imejidhihilisha pale ambapo wadau hawariziki na matumizi ya fedha wanazoipa taasis kwa ajili ya utafiti na hata wakati mwengine data zinazotolewa ni za kugushi/uongo. Vifaa kama magari ya utafiti yanatumika katika kazi binafsi kama za ujenzi na shughuli nyingine za kifamilia kama graduation na harusi. Ukifika makao makuu ukiona magari yaliyoegesha majira ya asubuhi siku inapoanza utadanganyika kuwa taasis ina mikakati madhubuti ya utendaji kazi. Changa la macho!!

  2.Taasisi imeshindwa kutekeleza mpango kazi (strategic plan), tunaishangaa sana hazina kuiruhusu taasis kuendelea kuwalipa mishahara mikubwa mikubwa watafiti wa taasis waliopo na wanaoendelea kuajiliwa wapya huku hakuna kazi zinazofanywa siku hadi siku. Kama vile viongozi wanadhani watumishi wa chini yao wameajiliwa kupata mishahara midogo na sio kufanya kazi. Eti kazi hufanyika na watu wachache wa juu kwenye taasis na ndio majina yao yanayoonekana kwenye vocha za malipo za siku hadi siku. Wengine ni kenge kwenye msafara wa mamba. Uwepo wa watafiti wapya hali wazamani wanacheza karata na kushinda kwenye mtandao wa internet au kwenye shughuli binafsi. Uliza mtumishi wa kawaida TAWIRI atakuambia asilimia 99 ya watumishi wa taasis huenda ofisini kuweka sahihi katika kitabu cha mahudhulio na kusubili mwisho wa mwezi. Na 1% ni hao mabosi walio bize na kazi za wazungu. Cha kushangaza zaidi ni kwamba wakati taasis imeshindwa kutekeleza mpango kazi wake mwaka huu (2008) katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi wakurugenzi (Mduma na Keyyu) waliamua kwa ubinafsi wao wawe wafanyakazi BORA. Wakapata mshiko na vyetu kwa kuhodhi madalaka badala ya kugawa majukumu kwa watafiti wengine.

  Hali kama hiyo mara nyingi hukatisha tamaa watendaji kazi wa chini ya viongozi wa namna hii. Pia inaonyesha jinsi viongozi hao wasivyojali taratibu, kanuni na sheria za kazi na uongozi. Wasomi ambao hawajaelimika.

  2.Ajila na mafunzo

  Kuanzia Keyyu achukue nafasi ya ukurugenzi wa utafiti badala ya kusimamia shughuli za utafiti amekuwa akifanya kazi za utawala kama afisa utumishi ambazo kwa hakika hana hata chembe ya hiyo taaluma kwani yeye ni daktari wa mifugo. Hii imepelekea taasis kupoteza seniority za Utumishi wake kama ilivyo kwenye taasis nyingine za selikali. Seniority ndani ya TAWIRI inategemea yeye Keyyu ataamua mtumishi awe wapi kwa kisingizio cha maamuzi ya management. Na vigezo anavyotumia ni ukabila (usukuma) na udini (usabato). Tumeshuhudia akimfanikisha ndugu yake Hamza awe ni project meneja Tabora, wakati huo huo akapewa project ya mtu mwingine Serengeti, kabla hajamaliza akapelekwa kwenye exchange program Africa ya Kusini, kabla ya muda akaacha na kwenda Netherlands kwa masters. Wakati taasis ina watumishi wengine wengi wenye kuweza kushika hizo nafasi. Katika ajira za hivi karibuni walihakikisha kuwa ukabila ndio kigezo kikuu ambapo waliajiliwa watafiti 4, watatu ni wasukuma na mmoja ni mpare. Keyyu alihakikisha kuwa aliowataka wote wamepata maswali ya interview. Kati ya hizo ajira mpya mmoja (Ernest) ambaye atalipwa na hazina amepelekwa kwenye mladi wa mzungu Sinclair unao simamiwa na Mduma akisaidia na Nkwabi wote wawili pia wakipata mishahara ya hazina na mishahara na marupurupu ya mradi wa mzungu. Hii siyo kudumaza taasis ya umma?

  Pia amekuwa akitoa upendeleo wa waziwazi kwa masekretari wasabato kwa kuwaambia waandike extra duty allowance kwa kuandika ripoti za uongo hata kama hakuna ripoti walizoandika. Pia wengine wanapewa magari matatu DFP mbili na STK moja kwenda nayo kwenye graduation za watoto wa jamaa zao na shughuli za ujenzi binafsi. Pamoja na Mduma kuwa na gari binafsi la Mkurugenzi mkuu anazo Land Crusar mkonga tatu za mradi wa Sinclair na ya kwake binafsi yasiyopungua manne. Hata ivo ya Taasis ndiyo yanayotumiwa kila wakati bila ya shaka sababu ya ahueni ya mafuta ya bure na maslahi ya matengenezo over invoicing kule Wakulima Engineering. Baada ya kujifanya anakwenda kukagua shughuli za taasis Serengeti kumbe kufuatia ushauri wa mara kwa mara toka kwa Borner na kufuatilia ujenzi wa hoteli ya kitalii ya Sinclair iliyoko ufukweni mwa ziwa Victoria ambapo pia na yeye anajengewa. Muda, vifaa na fedha za taasis zinashughulikia maswala binafsi tena ya wazungu.

  Pia tumeshuhudia upendeleo kwenye fedha za mafunzo ambayo yeye anasimamia Samwel Bakari akatumia fedha toka wizarani na NORAD kusomea masters (double scholarship) ikiwa ni fadhila kwa kuwa kwenye mtandao wa kuchota fedha za NORAD.

  Kutokana na kutokuwepo na utaratibu wa utendaji kazi katika taasis pamoja na upendeleo wa kikabila na kidini watumishi wengi wamedhamiria kuondoka kufanya kazi sehemu nyingine na wengine wameshaaza kuondoka kwa kurudi wizarani,idarani na wengine kufundisha vyuo vya elimu ya juu. Ukionekana wewe ni tishio katika utawala uliokuwepo na uliopo unapewa kibano mpaka unachanganyikiwa. Baadhi ya watafiti waliokuwa nyuki na idara ya wanyamapori wanatamani kurudi wizarani. Wahasibu kwa kuona mwelekeo wa ufisadi ndani ya taasis wameshanza kutafuta namna ya kuondoka kutafuta ajira sehemu nyingine. Ma sekretali nao ni manunguniko mtindo mmoja. Walinzi ndio usiseme! Fununu ni kuwa ambao au wako kwenye masomo ya PhD au wanaoenda sasa hivi mipango yao ni kuondoka kwenye taasis na kujiunga na taasis za elimu ya juu. Hii yote ni kwa taasis kukosa uongozi thabiti na wenye maslahi ya kizalendo. TAWIRI inayopigiwa debe la capacity building kwa hali hii ya uongozi inaweza kuwepo tena miaka mitatu ijayo kweli. Au itakuwa NGO ya wazungu na mamluki wa kitanzani.

  Ujenzi wa Nyumba

  Taasis ilishindwa kusimamia fedha za wafadhili zilizotolewa kujenga Nyumba 3 za watafiti Seronera. Hali hii imepelekea watafiti kushindwa kuhamia katika Nyumba hizo kwa hofu ya kuangukiwa ukuta kutokana na nyufa zilizosababishwa na ujenzi wa chini ya kiwango huku fedha hizo za ujenzi zimepelekwa Njiro hill kwa ujenzi wa nyumba binafsi. Malugu aliyeajiriwa karibuni alipewa kuongoza kituo cha serengeti baada ya Samweli kwenda kusoma kwa scholarship mbili. Malugu kwa kipindi kifupi na kwa kuwezesha na viongozi wa taasis alichukuwa kiasi kikubwa cha fedha na ameshajenga Njiro hill kwa kipindi kifupi sana na kununua landlover ya taasis. Wamejipanga Njiro hill na ujenzi unafanyika kwa mashindano. Kwa kuwa hakuna wa kuwakemea wanadhani ukishakuteuliwa kuwa kiongozi kwenye chombo cha umma kazi ni kukibaka chombo hicho kwa manufaa yako na familia yako.

  Matengenezo ya magali

  Magari ya taasis yamekuwa yakitengenezwa kwa gharama kubwa mno huko Wakulima Engeneering. Fedha nyingi za OC zinaishia kwenye matengenezo ya magari fedha nyingi hubakwa na viongozi wawili au watatu wa taasis wengine ni wacovu na hawaoni ndani.

  Vitalu

  Katika kuandaa maandalizi ya kutathmini vitalu vya uwindaji Maliti alikuwa ameanda invoice ya ramani ya kuonyesha nchi nzima kwa tsh 22,000,000/= wakati bei ya halali ilikuwa tshs 5,000,000/=. hatuna uhakika kama azma hiyo ya kiufisadi ilifanikishwa. Hata fedha nyingi za kuidadi wanyama zinatumika kwa namna ambayo haileti maslahi katika zoezi hilo. Ndiyo maana kuna viporo vya mda mlefu vya ripoti hazijakamilika chini ya usimamizi wa fisadi Maliti na mshauri mkuu wa Mduma.

  Hitimisho

  Waziri Diallo alitaka kuifuta TAWIRI labuda kwa sababu kuu kadhaa. Kila mkurugenzi mkuu alipoulizwa pamoja na kuchangiwa fedha na wadau huwa wanafanya nini alikuwa hana jibu, Watumishi kufuka Njiro kuweka saini kwenye vitabu vya mahudhuria basi. Hakuna mipango ya kazi na hivo watumishi kujiendea tu kazini ili mradi. Hakuna mpango wa wazi wa mafunzo na watu kusoma kwa upendeleo wa kinamna. Wazungu wameingilia taasis kwa namna nyingi kiasi kuwa serikali ni kama haina mamlaka na TAWIRI. Ajira zinafanyika kiholela pasipokuwepo kwa mipango ya utendaji kazi. Ubadhilifu ni wa hali ya juu kiasi kuwa kinachofanyika TAWIRI ni mashindano ya kujenga Njiro hill na kununua magari binafsi kwa fujo za ushindani. Akifika mgeni akiona magari yaliyoegesha anasema yes hapa ndiyo mahali pa kufanya kazi maana baada ya miezi una magari na Nyumba njiro hill. Watumishi wengi kukata tamaa na kukosa mwelekea na kuanza kujiondoa mmoja mmoja. Kutokuelewa kinachofanyika ndani ya TAWIRI (uongo mwingi–minitis za vikao kubadilishwabadilishwa) na Bodi na hata wizara. Hali hii inaashiria kuwa TAWIRI ni mzigo kwa serikali au ni kama vile kujaza maji kwenye magunia. Au ipo iendelee kuwepo kuwanufaisha wazungu na mamluki ila sio kwa manufaa ya watanzania. Ni UFISADI wa hali ya juu wa kuididimiza taasis na maliasili ya nchi hii!

  MWENYE UCHUNGU NA NCHI HII ATUPIA JICHO LA MWEWE KWENYE CHOMBO HIKI MAPEMA KABLA JUA HALIJATUA. AIDHA SERIKALI IIFUMUE NA KUISUKA UPYA TAWIRI AU WAZO LA WAZIRI DIALLO LITEKELEZWE KWA MANUFAA YA TAIFA


  Mungu ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika
   
Loading...