Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Nimefuatilia hoja za viongozi wengi wa Umma wenye PhD na Masters, kila wanaposimama kuzungumzia mstakabali wa nchi yetu wamekuwa wepesi sana KUTUDANGANYA.
Matumizi ya elimu za wasomi ambao ndio viongozi waandamizi wa Taifa letu hayaendani kabisa na kile wanachokichangia kwa Taifa.
Msemaji wa serikali ana PHd ila sikiliza hoja zake katika vipindi na maeneo mbalimbali utagundua lipo tatizo la kusema ukweli hapa nchini na tatizo linachangiwa na wasomi.
Msikilize Mbobezi wa sheria, Mzee wa Mambo ya nje anapozungumza kuhusu nchi yetu utagundua lipo gonjwa la uongo ndani yetu. Waziri wa Mambo ya nje alituaminisha sisi ni matajiri na kuwaita matajiri MABEBERU huku akijua tunao mabalozi nje wanaotuombea tupate misaada na wahisani, ni kulewa UONGO wa kisomi.
Nenda kutana na mtumishi wa Umma mwenye master's na Phd zungumza naye japo kwa dakika kadhaa unagundua wazi hata kile anachokifanya hakijui.
Najiuliza kwanini tunadhani tunahitaji wasomi wakubwa kuingoza sekta ya umma hapa Tanzania?