Kwanini watu wapole wanaitwa Silent killers?

Kwanini watu wapole wanaitwa Silent killers?

Focus120

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
1,094
Reaction score
804
Habari wadau,

Naomba niulize, hivi kwanini watu wakimya, au wengine hutumia lugha " wapole" wanakuwa regarded kama "silent killers".Juzi nilikuwa kijiweni, kuna kijana mmoja ambae ukweli ni mstaarabu kwakuwa kwa kiwango chake heshima anayo, pia sio mtu wa totoz kama vijana wengi hapa mtaani, cha ajabu mmoja wetu akasema wapole wote ni ma silent killers especially yeye.

Basi hapo nikabaki najiuliza hivi kwanini watu wapole au wakimya hutafsiriwa kama silent killers.
Silent killers - watu waovu wanaofanya mambo yao kwa kificho.

Naombeni tujadili jamani.
 
Kwa mtazamo wangu hapo naona kuna kitu kimoja kinachotofautisha watu...wote ni killers ila kuna wengine ni "makeke-killers" na wengine ni "silent-killers"
Kama Jumatatu zote zingekuwa "blue" tusingekuwa na "blue-monday" ila tungekuwa na "blue-day"
 
Haimaanishi kuwa wapole wote ni ma silent killer but kuna wale watu ni wapole i mean hana maneno mengi but ukimtibua iyo vita hutaiweza
 
sema wapole mademu wanakufagilia wenyewe na wanajileta wenyewe...unakula na hawajuani..dah acha tu
 
Watu wapole mara nyingi wanatumia muda wao mwingi kuusoma mchezo, na kila move wanayofanya inakuwa well calculated. Ni rahisi sana ku-win trust ya watu and b4 you know it, wameshatimiza malengo yao, kama walikuwa nayo. Speaking from experience.
ukweli 100%
 
Ni watu wa kusoma mchezo na kufanya kile kinachotakiwa bila papara na kimya kimya. Utaona kama hataki vile vile kumbe ndiyo anapita.
 
Ninyi ndo mnafungwa mahakamani kirahisi rahisi...shahidi aliyetoa maneno haya ni mshkaji wako uliyemwacha kijiweni kwanini hukumhoji vizuri? Sisi hatuna mchango wowote hadi umlete huyu aliyetoa maneno tajwa tumlime maswali aeleze vizuri!
 
Wengi wao sio watu wa maneno mengi...wanaangalia possibilities za kutosha kabla ya kufanya smart move....wanajua wanachofanya...na mara nyingi ushindi ushindi unakuwa upande wao
 
Hata mimi ni mpole sana. Majirani zangu na wafanyakazi wenzangu wananiambia hivyo.
 
Watu Wote ni killers tofaut ni hii, mcharuko ye ni LOUD killers na mpole ye ndo SILENT killers.
 
Habari wadau,

Naomba niulize, hivi kwanini watu wakimya, au wengine hutumia lugha " wapole" wanakuwa regarded kama "silent killers".Juzi nilikuwa kijiweni, kuna kijana mmoja ambae ukweli ni mstaarabu kwakuwa kwa kiwango chake heshima anayo, pia sio mtu wa totoz kama vijana wengi hapa mtaani, cha ajabu mmoja wetu akasema wapole wote ni ma silent killers especially yeye.

Basi hapo nikabaki najiuliza hivi kwanini watu wapole au wakimya hutafsiriwa kama silent killers.
Silent killers - watu waovu wanaofanya mambo yao kwa kificho.

Naombeni tujadili jamani.

Kwasababu muda wote huinama kutunga sheria na kuzifanyia kazi kimyakimya!!
 
What do they kill anyway?:thinking:
 
Watu Wote ni killers tofaut ni hii, mcharuko ye ni LOUD killers na mpole ye ndo SILENT killers.

Sasa kuna muda mwingine hata mtu innocent anaitwa ni Silent killer
 
Usione kobe kainama ujue anatunga sheria...
 
Back
Top Bottom