Joachimmpanda97
Member
- Apr 17, 2017
- 20
- 27
Habari zenu wana JF
Leo nataka kushare na nyinyi sababu kuu inayowafanya kundi hili liwe kwenye wakati mgumu sana kupata kazi na njia wanazoweza kutumia kupata ajira kwa urahisi zaidi.
Kwa kuanza, “waliomaliza chuo” namaanisha watu wanaoingia kwenye soko la ajira bila ya uzoefu wowote yaani “no experience”
Kitu kinachonisikitisha na kilichonifanya kuandika uzi huu ni kuona idadi kubwa ya kundi hili wa kiamini kwamba watapata kazi yenye mshahara wa laki 7 mara tu wanapomaliza chuo na kuanza kutafuta kazi. Kibaya zaidi ni idadi ndogo sana ya watu hawa hupata kazi yenye mshahara wa aina hiyo, wengi wao wako mtaani wa kilia na kuilaumu serikali, kumbe shida ni yao!
Hiyo idadi ndogo hupata kazi za muda mfupi na wengi hupata kazi za mishahara ya aina hiyo kwasababu wana connection na watu kwenye soko la ajira (Network).
Kwanini Hawapati kazi?
Ni nafasi ngapi za kazi ambazo umeona kwamba hawajaorodhesha kigezo cha uzoefu? Chache mno! Kwa ufupi ni kwamba makampuni na mashirika mengi yanawaona watu waliomaliza chuo moja kwa moja kwamba wanahitaji (intensive training) mafunzo ya kina, kitu ambacho kina gharimu muda na pesa nyingi na hawajui itifaki za kazi. Hivyo ni bora wawaajiri wenzao ambao wana uzoefu.
Lakini kikubwa zaidi kinachowarudisha nyuma watu hawa ni imani yao ya kwamba watakapomaliza chuo watapata kazi yenye mshahara mnono. Kitu cha kwanza mwanafunzi wa chuo anapaswa kufahamu kwamba baada ya kumaliza chuo yani kupata ujuzi, anapaswa kutafuta uzoefu na sio pesa
Nini cha kufanya?
Mtu yeyote anapomaliza chuo anapaswa kutafuta kazi za mafunzo yani internship, kulingana na uzoefu wangu mimi, anapaswa kufanya internship hiyo kwa angalau miaka miwili.
Makampuni mengi na mashirika hayatoi mshahara kwa watu wa internship. Kama pesa za kujiruzuku ni tatizo, jaribu kuongea na mhusika kwenye kampuni hiyo aweze kukupatia angalau pesa ya nauli na chakula cha mchana. Wengi wamejaribu hivi na wamefanikiwa!
Faida za kutumia utaratibu huu
Kitu cha kwanza kikubwa utakachopata wewe ni uzoefu wa kazi. Utajiongezea alamu nyingi za kupata kazi unapotuma maombi. Utofauti wa mtu asiye na uzoefu na aliye na uzoefu wa angalau miaka miwili ni mkubwa mno kwenye soko la ajira.
Kama hukufahamu, njia yenye matokea zaidi ya kutafuta kazi ni kupitia kujuana connection(Networking) ulizo nazo sio kuomba kazi moja kwa moja. Unapojitolea kufanya kazi mahala Fulani kwa bidii na ufanisi, kwanza kabisa unajiongezea nafasi ya kuajiriwa na kampuni hiyo na pia unajitengeneza kujuana na watu tofauti tofauti ambao watakuunganisha na fursa nyingi za ajira
Wewe kijana ulioko chuo bado au tayari umeanza kutafta kazi, nakushauri utumia utaratibu huu utakujengea jina zuri katika soko la ajira kwa miaka mingi ijayo!
Wiki ijayo nitajitahidi kutengeneza uzi utakao tueleza namna ya kutafuta hizo internship opportunities
Ukipenda nkufikishie elimu hii karibu zaidi nawe unaweza kuni WhatsApp 0621151090. Nitakutumia kwa wiki mara moja