Kwanini watu hutoka nje ya ndoa zao?

Kwanini watu hutoka nje ya ndoa zao?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
486
Habari zenyu bhana!
Siku nyingi sana ila kiukweli nimewamiss sana!
Sasa nakuja na hii! Ni kwa nini wanandoa hutoka nje ya ndoa zao!
Nimemkuta jamaa mmoja kijana hivi ndoa yake ka miaka 5 hivi! Alikuwa na binti naye ndoa yake kama miaka 3. So wote wanandoa! Hawa ni zaidi ya wapenzi! Yaani utafikiri ndo wanandoa ila kila mtu kaacha mme/mke nyumbani. Sasa najiuliza kwa nini wana cheat? Kuna shida gani?
 
[h=3]MWANAMKE ANACHOTAKIWA KUFANYA MUME ASITOKE NJE YA NDOA.[/h]

​

Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.


Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.


Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.


Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee kwake.


Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.


Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.


Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.


Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.


Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.


Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.


Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?


Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.


Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume zao.


Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazooonekana kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.


Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe huu ni mwezi wa pili baada ya mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye aliona kinyaa kuyafanya.


Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya kuguna ni kwamba niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe. Niseme tu kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa nini nasema hivyo.


Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama mwanaume huyo anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa, mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.


Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.


Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatilizia.
​
 
Somo zuri sana... ngoja nizidishe mautundu.. Elli angalie usije ukagoma kwenda kazini...maana naanza tuition upyaaaa..
 
(1) Sababu kubwa ni kutokumuongopa Mungu, kutokuwa na hofu ya Mungu.
(2) Ndoa iliyotokana na madawa kama limbwata au ushirikina wa aina yoyote dawa zikiisha nguvu ndio mambo hayo hutokea.
(3) Ndoa iliyotokana na shinikizo la wazazi upendo haupo kamili.
(4) Ndoa iliyotokana na tamaa sababu ya mtu kuwa na pesa, pesa zikiisha ndiyo hivyo tena.
(5) Kutamani kupata kazi bila kuwa na sifa stahiki, waajiri ni rahisi kuomba rushwa ya ngono.
(6) Tamaa ya kuwa na vitu vizuri wakati mtu huna uwezo, wanawake mara nyingi huwa wanapenda kushindana hapo ndipo wanapokutana na wanaume wakware wenye mihela ya kuchezea.
(7) Wanandoa kutokutimiziana kimwili na kutokuwa wazi kudai haki ya kutimiziwa, yaani kufikishwa kileleni.
Haya yote yanaweza kusababisha mwanandoa asiye na hofu ya Mungu kutembea nje ya ndoa yake.
 
Ndoa na iheshimiwe,hao wanaotoka nje hawajui heshima ya ndoa na ni watu waliopotoka.Unapoapa kwa Mungu na wanadamu wenzako halafu unakuja kukiuka baadae ni kupotoka na inaonesha wazi kuwa kile kiapo ulichoapa hakikuwa cha dhati na ilikuwa ni kama maigizo tu.
 
Joseph Isaack sio kwamba tunajiuliza kwa ushabiki tu! Inawezekana kuna watu ambao pia ni waathiriwa wa hii kitu. Nakushauri kama unayo ya kuchangia changia! Kama huna kaa kimya na uone watu wanachangiaje! Hakuna credits zozote kujibu majibu kama yako!

Englibertm - Asante sana kwa uchambuzi! Kwa hapa umechangia makosa wayafanyayo wanawake! Ila sasa wanawake nao wanatoka nje! Je wanakosa nini kwa waume zao!

Katika kuongea kwetu huyu kaka mke wa mtu alikuwa na hayo uliyoyasema! Karibia yote!

Sasa binti naye aliishia kumlaumu mumewe kuwa hataki inputs mpya! Yaani mumewe hataki madoido! Akitaka siku hiyo basi anarukia then anamaliza faster anajilaza pembeni anaanza kukoroma!
Anadai yeye anahitaji kuandaliwa! Kuchezewa hapa na pale na mwisho wajikute huko! Hapati hii kitu!
 
sio lazima kuwe na sababu.., some people just do it because they can
 
Hili ni jambo linalokusanya mambo mengi sana,sio jambo moja au sababu moja!
 
Somo zuri sana,mtaalam waambie,wachane live wanabweteka ndoa ni maujanja na mautundu ndo unaofanya wanandoa wasichokane!!
 
Hahahahaa twende zetu mwaya tukatest kama somo limeeleweka, mie napenda kusoma kitu na kukifanyia kazi Switihati Lotion wangu
Somo zuri sana... ngoja nizidishe mautundu.. Elli angalie usije ukagoma kwenda kazini...maana naanza tuition upyaaaa..
 
yani hapo kila mmoja kwny ndoa yake ni kama jehanam so wameamua watoane stress wenzenu!
 
For me if I could carry my wife in my trouser pocket I dare would have not cheated! Ingalikuwa na nafasi au uwezo wa kutembea na mke wangu kwenye mfuko wa suruali nisingejaribu kutoka nje ya ndoa.
 
MWANAMKE ANACHOTAKIWA KUFANYA MUME ASITOKE NJE YA NDOA.



​

Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.


Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.


Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.


Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee kwake.


Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.


Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.


Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.


Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.


Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.


Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.


Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?


Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.


Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume zao.


Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazooonekana kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.


Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe huu ni mwezi wa pili baada ya mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye aliona kinyaa kuyafanya.


Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya kuguna ni kwamba niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe. Niseme tu kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa nini nasema hivyo.


Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama mwanaume huyo anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa, mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.


Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.


Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatilizia.
​
Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama mwanaume huyo anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa, mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.

Hapa nahisi kkuna mtihani kidogo, je akitoka kwa sababu ya hicho ulichosema isipokuwa..... atakuwa amefanikiwa kumdhibiti? manake ndo visa vyenyewe hivyo siku hizi za dijitali, kulamba chumvi, kwenda njia iso barabara, kukaa mikao ya kichina nk nk!
 
"Kwanini watu hutoka nje ya ndoa zao" ??
A%20S%20angry.gif

Ebooo! si milango iko wazi!
Ajitokeze mwenye ndoa ambaye milango yake imefungwa kama yupo hata mmoja!
Subutu yake!!!!!! Ndo maana 47% ya wana ndoa ni HIV+
Chezea dushelele na kibobo weye.
 
U-boo ukisha semama akili zinaruka, hakuna sababu zaidi ya hio kwa wanaume, ama kwa wanawake sijui sababu gani labda wanawashwa washwa :biggrin1:
 
Back
Top Bottom