Kuoa/kuolewa kuna kukamilisha...msaidizi wa kufanana naye ni jukumu tofauti kabisa na kuoa/kuolewa swali linataka sababu za kuoa/kuolewa
Samahani ndugu kwa kuwa upande mmoja. Nilimaanisha kuyasoma Maandiko Matakatifu. Kila kitu kimo humoswala kuoa halijalishi dini mkuu wakisto/waislam wote linawahusu
kwani adam na hawa walioana...?hebu nisaidie nimepoteza kumbukumbu...?hayo ni mambo ya asili ndo maana MUNGU alipomuumba ADAM akaona ADAM atakuwa ajakamilika bila kupata msaidizi hivyo MUNGU alimuumba HAWA ili asaidiane majukumu na ADAM...hivyo mtu anaoa au kuolewa ili tu apate mwenza wa kusaidiana nae katika maisha.
Wana jf naomba kujuzwa sababu hasa inayotufanya kuoa/kuolewa au kwa wale walio kwenye ndoa kwa nini umeoa/kuolewa?, mimi ni kijana mwenzenu ambaye nipo katika mchakato wa kutafuta mwenza, lakini kutokana na mabandiko kadha wakadha hapa jf inaonesha ndani ya ndoa kuna misigishano mingi mno inayopelekea watu kuchit, kulea watoto wasio wao pia wakati mwingine na mengine mengi sasa ule upendo ninaousikia huwa umeenda wapi?
Kwa hali ya kawaida mtu unaweza fikiri nina matatizo kuleta uzi huu ila kuna watu wameoa/kuolewa wasijue kwa nini walifikia maamuzi hayo? (kuoa/kuolewa) kama umeoa/kuolewa naomba sababu ya:-
i) Kwanini umeoa? Kwanini unafikiri kuoa?
ii) Kwanini umeolewa? Kwanini unafikiri kuolewa?
Tafadhali fikiri kabla ya kujibu then unisaidie kwa namna ya kunijenga na siyo kunibomoa ili vijana wengine wafaidike pia.
View attachment 417422
Nilichokuja kugundua ni kwamba wengi wanaoa/kuolewa pasipo kukaachini na kufikiria kwanini waoe/kuolewa,ni vitu gani wanavifata katika ndoa,na je wapotayari kwa dhati kuyavumilia watakayo yakuta huko?
Ni kitu ambacho pia nimekuwa nikijiuliza siku nyingi. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini ndoa zimekuwa ni mojawapo ya kitu ambacho kimekuwa kama vile adhaa kwa wanandoa mda mfupi baada ya kuoana? ili hali asilia kubwa wanaoana kwa hiari yao wenyewe?.Huwa nafika mbali kwa kujiuliza ni kitu ambacho huwafumba macho watu kiasi kwamba kabla yakuoa/kuolewa hawaoni kile ambacho huwa wanakiona baada ya kuingia kwenye ndoa nakuanza kuzua varangati licha ya mambo mengi yahusuyo maisha ya ndoa kuwa wazi ?
Nilichokuja kugundua ni kwamba wengi wanaoa/kuolewa pasi na kukaachini na kufikiria kwanini waoe/kuolewa,ni vitu gani wanavifata katika ndoa,na je wapotayari kwa dhati kuyavumilia watakayo yakuta huko?
Badala yake wengi wanafikia maamuzi hayo kwa sababu tu umri unawatupa mkono,tamaa za mda mfupi (pasipo kuhusisha ubongo kwa kiasi kikubwa),kwa kushawishiwa na ndugu na jamaa ,wengine wanaiga na pia kutaka sifa tu.Kama mtu ameingia kwa sababu hizo nithahiri ndo maana ndoa nyingi haziishi mizozo kwa vile wanandoa wamekutana na vitu ambayo hawakuvifikiria kabla.Mwanandoa hataona shida kuchepuka kwa vile hajajicomit hicho kwa mwenza wake wala hicho hakikuwa kipaumbele chake kuingia kwenye ndoa.
Mtazamo wangu ndoa siyo lazima kwa vile vingi ambavyo watu wanadhamiria na kuvifata katika ndoa unaweza kuvipata hata ukiwa nje ya ndoa(hujaoa/kuolewa).Sioni sababu ya kuchepuka wakati una mke au mme ambaye anaweza anaweza kukupa hicho unachokifata huko kwenye mchepuko.Tunatakiwa tuingie katika ndoa kwa sababu tuko tayari kukaa na kuiishi ndoa, tuko tayari kwa dhati (wote wawili) kwenye ndoa , tunahaja ya kuyatambua mapungufu yetu ili kisiwe kikwazo kwa wengine(wenza wetu)
inatosha kwa leo
Mkuu ukichunguza kwa makini utagundua kuna vitu vingi sana ambavyo havina maana yoyote lakini watu tumekua tukivifanya bila hata kuwa na sababu za msingi. Ni mila tuu na mazoea tuliyorithishwa
1. Kummiliki mwenza katika unyumba na kumhalalisha kijamii, kiserikali na kidini.
2. Kuanzisha milki yetu mimi na mwenza kiunyumba.
3. Kutafsiri hisia za upendo katika ulimwengu wa matendo halisi.
Kwani kupenda mwanadamu mwingine kunanizuia kumpenda MunguMpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na siyo umpende mwanadamu