Kwanini watu huchukua maamuzi ya kujinyonga hadi kufa?

Kwanini watu huchukua maamuzi ya kujinyonga hadi kufa?

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,471
Reaction score
9,532
Katika moja ya pita pita zangu mitandaoni nimekutana na video [emoji116] ikimuonyesha mwanaume mmoja wa makamo akitaka kujinyonga hadi kufa kwasababu ambazo hazijawekwa wazi huku baadhi ya mashuhuda wakimrekodi wakati wakisubiri atekeleze jaribio lake.

Kwanini binadamu tunakata tamaa katika haya maisha mpaka kuamua kutekeleza ukatili huu dhidi ya nafsi zetu wenyewe? Sijawahi kuelewa ujasiri wa mtu kujiondoa uhai kwa njia ngumu kiasi hichi huwa unatokana na nini!

 
Huyu fala hakuwa na nia ya kujiua maana mtu mwenye nia asingekuja sehemu ambayo kuna watu weeengi wanapita pita angeenda eneo ambalo hakuna jam ya watu na kutekeleza hilo lengo lake. Kiufupi ni mgonjwa wa akili au anatafta atrend mitandaoni tu
 
Kwenye saikolojia ya kujiua (suicide), mpaka unamuona mtu kafanikiwa kujiua, basi ujue alishafanya jaribio/majaribio kadhaa ya kutaka kujiua, kitaalamu wanaita suicide attempt(s).

Kichocheo kikubwa kikiwa ni msongo wa mawazo (depression). Sometimes fikra tu ya kutaka kujiua inahesabika pia kama suicide attempt na kadri mtu anavyozidi kufanya attempts ndio inakua rahisi kwake kujimaliza, maana siku atakayofanya anakua ashajiridhisha kwamba kitendo anachofanya ni sahihi!

Hivyo haitokei kwa bahati mbaya.
 
Binadamu tupo tufauti karibia kwenye kila nyanja, kinachokuumiza wewe mwenzako kinamchekesha na kinachomuumiza yeye wewe kwako ni mboga.

Ni lazima tuwe hivyo ili tuishi hatuwezi lingana kimtizamo,maono,imani na kisirka...
 
Nadhani premise yako ina makosa kudhani jibu moja linaweza ku-apply kwa matukio kama hayo yote...

Lakini in short logically mtu akiamua kuchukua uamuzi huu badala ya ule kwa mtizamo wake uamuzi uliopo ni mgumu na haufai kuliko uamuzi anaochagua kuufanya...
 
Mtu anapofikia hatua ya kujiua anakua sio yeye kiakili na kifikra,yaani mgonjwa wa akili,

Ni sawa na mtu uchukue Dada poa njiani kisha ukisha maliza haja zako uanze kujuta kwa ulichokifanya,

Pia unaweza kuua kisha baadae baada ya akili yako kurudi sawa,utaanza kujuta na kujilaumu kwa mauaji uliyoyafanya.
 
Ni ugonjwa wa akili hakuna sababu nyingine.
 
Back
Top Bottom