Kwanini watu hawasemi asante?

Watu wa Mara na ahsante wapi na wapi?!?
Kuomba tu hawaombi utasikia "nipe, nataka"


Ohoooo..! Hii Lugha gongana, kama Magu na Billgate.
Ulitakiwa usome kimoyomoyo then kwa sauti, wewe unaparaza majicho.,
Taratibu teacher, Usjie chana page zetu pendwa za Jf bure.
 
Soma uelewe kwanza kuliko kukimbilia kucomment tu, mleta mada hajasema huyo ndugu yake yupo mkoa wa Mara,ila amesema yupo "mkoa" "mara nyingi hua ananiomba ela..." hilo neno mara limetumika kama "more than once" na sio kama jina la mkoa.
Hiyo mara ilitakiwa iwe herufi ndogo, jina ndo lina herufi kubwa
 
Wa mikoani ndo walivyo aseee yaan wanachukulia kama ni haki yao uwatumie, mkuu we kula kobisi tu kwann ukonde na hela yako mwambie sina. Unajua toka waambiwe atakaefikisha julai yupo mjini kidume naona heshima imewarudi watu wa mikoani.
 
Hiyo ni tabia ambayo mtu akuwa nayo toka utoto wake, huku kwetu kusini hasa Mkoa wa Lindi hiyo tabia ipo sana yaan kutoa neno asante ni nadra.
 
Tenda wema wende zako usingoje shukrani,huikumbuki methali hii?
 
Nadhani ni aina ya maisha ambayo mtu anakuwa ameishi kuna wengine hawajuagi hata ahsante inatumika wapi na wakati gani

Japokuwa mi pia huwa nachukia sana yaani unaweza mtumia mtu hela hawezi kupiga kukwambia ahsante mpaka umuulize na hata ukimuuliza bado hatokwambia ahsante zaidi ya kusema nimeshaipata.
 
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
[emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] sio kwa kunichekesha huko mkuu.

Haya nami nasema ahsante. [emoji124] [emoji124]
[emoji2] [emoji2] [emoji120] [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
Mkuu neno'ASANTE & SAMAHANI'ni maneno muhimu na ya maana sana lkn watu wengi hatuyatumii.Huwa invunja sana moyo unapomfanyia mtu jambo jema na asishukuru,japo wengi huwa hatusemi tunapotezea tu.Mtoto huwa nikimpa kitu asipo shukuru namnyang'anya hadi aseme ahasante.Nafikiri tunahitaji kuujenga utamaduni wa kutumia haya maneno kama tunavyotumia neon 'NAOMBA'na tutafanikiwa kama wenzetu wazungu kwani nawasifu kwani utdhani wamezaliwa nayo!hata kama hakujui!Nadhani ni moja ya siri ya mafanikio yao kwani hata maandiko matakatifu yana sema "shukukuruni kwa kila jambo"nadhani kuna siri nyuma ya hayo maneno.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…