Kwanini watu hawasemi asante?

Kibundi wa getto

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
455
Reaction score
878
Wakuu,

Kuna ndugu yangu yupo mkoa, Mara nyingi huwa ananiomba ela na ananililia shida kweli kweli na mimi huwa najitaidi kumtimizia.

Cha kushangaza kila nikimtumia pesa kwenye tigopesa huwa hasemi asante. Sasa mimi huwa najiuliza huyu ananichukuliaje, kwasababu huwa naangaika ili nimtumie kwa wakati lakini hajawai kushukuru.

Kwa kweli nimeapa simtumii pesa tena
 
Aisee watu wanatofautiana sana aisee, Malezi yanachangia sana.

Unaweza kuta hata akiipokea, hadi wewe umuulize tena """Vipi umeipata"""??? Hahahah[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119] ( Hapo ndo balaa zaidi).


Waungwana; Ukifanyiwa kitu, Kushukuru ni jambo jema. Linatia moyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Embu Siku umuulize, mbona hujashukuru! Uone atasemaje? Anzia hapo kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaumiza na kuvunja moyo halafu hawajui kama mkono unaotoa ndiyo unaopata baraka japo inaumiza sana, yeye nikuopkea tu bila asante na hizo pesa hata hawezi kufanyia cha maana, Mungu mwenyewe anataka mtu wa kushukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabia mbaya sana hio, japo si lazima mtu kusema asante ila naona sio ustaarabu kabisa. Naichukia hio tabia mbaya mno!
Watu wa hivyo hata kusema samahani hawawezagi pia.
 
Nilikutana na mzee mmoja kapinda, nikamuuliza uchochoro wa kuelekea nilikokuwa nataka kwenda, akanionesha. Nilivyoshukuru akaniambia: "kumbe ww mstaarabu, njia sahihi kuelekea unakokwenda ni hii, huko nilikokueleza mwanzo siko". Toka siku hiyo nikajifunza kushukuru, sasa nashukuru hata nikimaliza kupiga papuchi. 😛😛🙂
 
Mmmhh nnae mtu mwenye tabia hio neno asante gumu kwake
 
Hela,najitahidi,nahangaika,hajawahi,Naona umegombana mpaka na herufi "h" nayo pia hutaki kuitumia tena!!
 
huyo ni dadangu mmoja hv nimeacha kumtumia hata buku! hajui neno ahsante kbs ukimsema ananuna!.. mie ht kbl hujanituia hela nishashukuru aisee! hata kitandan lazma useme asante! nadhan sio malezi ni ukata wa maisha
 
Watu wa Mara na ahsante wapi na wapi?!?
Kuomba tu hawaombi utasikia "nipe, nataka"
Soma uelewe kwanza kuliko kukimbilia kucomment tu, mleta mada hajasema huyo ndugu yake yupo mkoa wa Mara,ila amesema yupo "mkoa" "mara nyingi hua ananiomba ela..." hilo neno mara limetumika kama "more than once" na sio kama jina la mkoa.
 
Kashindwa Akhsante.

Japo kukufahamisha ya kuwa amepata Mzigo.

Cha ajabu kuna Watu hawana Muda huo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…