Kwanini Watanzania wengi hawatumii mtandao wa LinkedIn?

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,831
Habari za muda huu wanajamvi, bila kupoteza muda nijikite moja kwa moja kwenye mada husika kama kichwa cha habari kinavyoashiria. Binafsi ni mpenzi mzuri na mtumiaji mkubwa wa mtandao huu wa LinkedIn na nimekuwa nikipost na ku-comment katika topics mbalimbali katika mtandao huo. Humu wana msemo wao kuwa "Jamiiforums the home of great thinkers" ila kiukweli great thinkers humu ni wachache sana, wengi humu ndani ni fix na umwamba yaaani kila mtu ni PhD holder humu, Billionaire yeye, Boss yeye yaani kwa ufupi kila mtu kavimba humu kwenye mtandao huu. Nilichogundua katika mtandao wa LinkedIn watumiaji wengi kutoka nchi za Africa ni Nigeria ndio inaongoza, Watanzania ni wa kutafuta kwa tochi katika mtandao huo.
Sio kwamba hawaujui la hasha bali mtandao huo kwa maudhui yake ya haraka haraka umekaa ki-professional zaidi yaani hakuna kuchati hovyo hovyo bali kila post inayowekwa humo ipo professionally kwaajili ya sector fulani, yaani ni mtandao ambao ukitaka kukuza taaluma yako na career yako kwa upana zaidi basi unalink na wanataaluma wenzako au hata kujifunza taaluma ya wenzako na kuongeza knowledge zaidi. Asilimia kubwa ya wabongo wamejazana Instagram sababu ya umbea wa kila mara ambao hauna tija, humu kuna baadhi ya topics zinaletwa humu kweli zimeshiba haswa ila porojo ni nyingi sana, Facebook ndio kabisa nadhani hadi watoto wa shule ya msingi wana accounts zao mule, Twitter ni mtandao ambao pia unajitahidi kwa kutumiwa na watu ambao wamepevuka akilini ndio maana wale wakimbia umande wengi wanaukwepa mtandao wa Twitter pia na hujisemea kuwa ni mtandao mgumu kuutumia jambo ambalo si kweli
Je kinachopelekea Watanzania wengi kutouzimikia huu mtandao wa LinkedIn ni sababu ya
1) Lugha gongana, yaani kiingereza hakipandi na ukizingatia ili uufaidi mtandao huo inabidi kidogo lugha iwe haijakuacha na meli
2) Ukanjanja wa taaluma, kwa minajili kuwa katika mtandao huo huwezi kumdanganya mtu kuwa una PhD ya Law ilihali aina ya comments zako zimekaa ki-form four failure so ndio maana wengi wanaingia mitini kuogopa kuaibika?
3) Kukosekana kwa udaku, kwa maana kwamba mtandao huo ulivyokaa haumpi mtu nafasi ya kusambaza umbea kupita website hiyo jambo ambalo inakua ngumu kwa wale wazoea udaku na umbea kuukwepa mtandao huo makini?
 
Umekosea kuidisi Jamiiforums, Ungeuelezea huo mtandao wa nyie 'wasomi' kwa njia nyingine pasipo kuiona Jamiiforums kama mtandao wa 'kindezi'.
Usinilishe maneno mkuu, hakuna mahala ambapo nimesema mtandao wa jamiiforums ni wa kindezi bali nimesema humu kila mtu kavimba, boss yeye, billionaire yeye, msomi yeye, mla bata yeye yaaani fix za kutosha ila sijauponda kuwa ni wa kindezi, rudia kusoma tena
 
Back
Top Bottom