Hivi mnaamini hizi takwimu?. Hizo ni overstated figure za waliojiandikisha ambazo zinawekwa strategically kama top up options sehemu CCM inapokuwa imeshindwa ili kubinulia meza ya kuhesabia kura na kuanza kuziokota wakati chini tayari kuna uchafu wa kuza za tick kwa CCM.
Nyie tujadiliane hapa mambo yote lakini wenyewe wanaangalia wanacheeka na kusema kweli strategy yetu inafanya kazi. Hayo matokeo waliyoweka tume ni uwongo ni mwendawazimu tu ndiye ataamini ni ya kweli. Hebu jiulize maswali haya yafuatayo
1. Iweje JK aongoze kila jimbo?, wakati kuna yaliyoenda kwa wapinzani katika ubunge?
2. CUF ilishika nafasi ya pili ya kura za urais iweje ilikosa mbunge hata mmoja Tanzania bara?
3. Kwa nini wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa maendeleo wawe wafanyakazi wa Tume inayomcheza bosi wao aliyewapa ulaji na timu "alien"
My prediction this October: CUF kilikuwa chama tishio kwa CCM kutokana na kukua kwa kasi na kupata wafuasi wengi hasa Zanzibar na maeneo mengi ya Tanzanua bara. Walichofanyiwa 2005 ilikuwa ni mkakati wa kukiondoa kwenye uso wa watu wa bara kwa miaka mitano, hivi sasa CHADEMA ni tishio kwa upande wa bara usishangae mwaka huu CHADEMA ikapoteza 99% ya wabunge wake wa sasa au kukosa hata kiti kimoja na CUF kupewa baada ya kupiga goti kule Zanzibar. Wasipoungana wapinzani ni sawa na dumuzi katika ghala la CCM wakizidi kubungua unapiga dawa ya DDT au unajenga ghala jipya ili dumuzi wa ghala la zamani wateketee kwa njaa. CCM haina ubavu wa kushinda kihalali pasi na kutumia mabavu na dola.
Kura za maoni zilizoisha zimetoa picha halisi ya nini huwa kinafanyika kwa wagombea wa CCM ama kwa kusaidiwa na chama chao, tume, TISS, au mtu binafsi akiachwa kwa kuwa mbele ya jina lake kuna CCM