Kwanini watanzania wengi hawapigi kura?

RedDevil,
Heading yako ilitakiwa isomeke hivi: Wananchi wengi hawapigi kura, na si kama ilivyo sasa,..., ni paradox!
 
Tatizo ni kadi ya kupigia kura imefanywa kitambulisho. Wanajiandikisha wengi lakini si kwa lengo la kupiga kura; na yawezekana ni mbinu chafu ya CCM ili waweze kucheza na matokeo!! Ila mimi mwaka huu lazima nitapiga kwani miaka ya nyuma nilikuwa sipigi kura!!!!!!!!
 
Mimi nilikuwa sijapiga toka 1985...mwaka huu nitakuwa wa kwanza kupiga....SLAA4LIFE

Mimi sijawahi kupiga kura kaka aibu kubwa - na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote tangu nizaliwe - nakumbuka nilipigwa viboko vinne, 0'level kwa kukataa kujiunga na UVCCM. ila mwaka huu mzee kituo kinafunguliwa tu mimi na ndugu zangu wote wa karibu tupo mstarini hadi kumchagua rais wetu, mpiganaji wetu.
 
Mimi sijawahi kupiga kura kaka aibu kubwa - na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote tangu nizaliwe - nakumbuka nilipigwa viboko vinne, 0'level kwa kukataa kujiunga na UVCCM. ila mwaka huu mzee kituo kinafunguliwa tu mimi na ndugu zangu wote wa karibu tupo mstarini hadi kumchagua rais wetu, mpiganaji wetu.

Aloo tafadhali...mimi nimesema ntakuwa wa kwanza usichukue nafasi yangu....
 
Hivi mnaamini hizi takwimu?. Hizo ni overstated figure za waliojiandikisha ambazo zinawekwa strategically kama top up options sehemu CCM inapokuwa imeshindwa ili kubinulia meza ya kuhesabia kura na kuanza kuziokota wakati chini tayari kuna uchafu wa kuza za tick kwa CCM.

Nyie tujadiliane hapa mambo yote lakini wenyewe wanaangalia wanacheeka na kusema kweli strategy yetu inafanya kazi. Hayo matokeo waliyoweka tume ni uwongo ni mwendawazimu tu ndiye ataamini ni ya kweli. Hebu jiulize maswali haya yafuatayo

1. Iweje JK aongoze kila jimbo?, wakati kuna yaliyoenda kwa wapinzani katika ubunge?

2. CUF ilishika nafasi ya pili ya kura za urais iweje ilikosa mbunge hata mmoja Tanzania bara?

3. Kwa nini wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa maendeleo wawe wafanyakazi wa Tume inayomcheza bosi wao aliyewapa ulaji na timu "alien"

My prediction this October: CUF kilikuwa chama tishio kwa CCM kutokana na kukua kwa kasi na kupata wafuasi wengi hasa Zanzibar na maeneo mengi ya Tanzanua bara. Walichofanyiwa 2005 ilikuwa ni mkakati wa kukiondoa kwenye uso wa watu wa bara kwa miaka mitano, hivi sasa CHADEMA ni tishio kwa upande wa bara usishangae mwaka huu CHADEMA ikapoteza 99% ya wabunge wake wa sasa au kukosa hata kiti kimoja na CUF kupewa baada ya kupiga goti kule Zanzibar. Wasipoungana wapinzani ni sawa na dumuzi katika ghala la CCM wakizidi kubungua unapiga dawa ya DDT au unajenga ghala jipya ili dumuzi wa ghala la zamani wateketee kwa njaa. CCM haina ubavu wa kushinda kihalali pasi na kutumia mabavu na dola.

Kura za maoni zilizoisha zimetoa picha halisi ya nini huwa kinafanyika kwa wagombea wa CCM ama kwa kusaidiwa na chama chao, tume, TISS, au mtu binafsi akiachwa kwa kuwa mbele ya jina lake kuna CCM
 
RedDevil,
Unajua sisi watanzania hatujapata mwamko wa kisiasa na kujua umuhimu wa kupiga kura. ukiangalia takwimu hizi zinatupa picha halisi. Idadi ya waliojiandikisha (wapiga kura) na waliopiga kura ni wazi tunahitaji kuhamasishana mwaka huu.

Takwimu zinaonyesha wazi kuwa kama vyama vya upinzani angalau viwili vikiweka mgombea mmoja mfano CUF & CHADEMA tunaweza kuiangusha CCM. Hebu angalia takwimu za CUF & CHADEMA kama zingeenda kwa mtu 1 tu na kwamba kuanzia muda wa kampeni wananchi wangeshawishiwa kupigia upinzani ni wazi JK asingepata huo ushindi wa kimbunga.

Prof Lipumba angemuunga mkono Dr. Slaa na Pengine kuwa mgombea mwenza mbona ushindi ungekuwa wazi. Ubinafsi wa vyama vya upinzani unatuponza.

Mwamko wa watu kupiga kura utakuwepo pale wananchi wataona upinzani uko serious, hawapigi kura kwa sababu wamekata tamaa, ukweli CCM hawaipendi. CCM wao wanamtaji wa wana-CCM walio na mwamko wa kupiga kura maana wanahamasishana nyumba hadi nyumba kama ilivyo kwa CUF pemba.

Mfano halisi ni wana-CCM waliojitokeza kupiga kura za maoni 2010 ni ushahidi tosha.

Nionavyo mimi Maalimu (CUF) tuwaunge mkono zenji na Dr. Slaa (CHADEMA) tumuunge Tanganyika tunaweza kung'oa utawala dharimu wenye lengo la kupora mali na utajiri wa watanzania.
 
Wote ambao hamjapiga kura miaka ya karibuni ni vizuri mkafanya hivyo mwaka huu na kuelekeza kura zenu kwa Shujaa wa Watanzania Dr Slaa. Matatizo ya wengi kutopiga kura yanasababishwa na mengi ikiwemo labda foleni ndefu kupita kiasi, vituo vichache vya kupigia kura, umbali wa vituo vya kupigia kura na pia labda wengi wa wa piga kura hawakujiandikisha katika kupiga kura katika uchaguzi ujao.

Ni vizuri katika kampeni ya kuwahamasisha ndugu, jamaa na marafiki kumpigia kura Dr Slaa na wagombea ubunge wa CHADEMA pia wakafahamishwa umuhimu wao wa kushiriki kupiga kura. Itakuwa ni hatua kubwa sana kama ikiwezekana 60% au zaidi ya wapiga kura wote kushiriki mwaka huu.
 
Ndugu zangu wanaJF, waTanzania wezangu! muda ni huu najua idadi kamili ya wananchi watakao piga kura october NEC wanayo, ijulikane mapema ili baadhi yetu tuanze kujiridhishan na kumlika zaidi kila kona.

Boss kasema, "wananchi mjitokeze katika kutekeleza haki ya msingi ya kupiga kura, mkisha piga kura basi msizengee zengee maeneo ya kupigia kura mrudi nyumbani" Hapo ndo wasiwasiwangu. Ndo maana nikataka kujua sasa hivi hiyo idadi ya wapiga kura mwaka huu. Ili nguvu tuanze kuzierekeza maeneo yenye population kubwa na macho yetu yaanze kumlika kwa makini yanayojiri.
 
Mod, kuna haja kubwa sana ya kuwaelewesha wananachi wa JF maana ya break news, news alerts na mengineyo. Ona sasa kama hii thread, inavuruga kabisa mihihili yetu ya kufikiria mambo ya maana na kupoteza morale wa kuisoma.
 
Hivi mnajua kwamba nguvu za CCM ziko kwa wap[iga kura wanawake? Kwa mfano kama kuna uwezekano, siku ya kupiga kura mtu aweze kuwazuia nusu ya wanawake wote nchini waliojiandikisha kupiga kura wasiende vituoni kupiga kura. CCM itakuwa matatani sana!

Hii ni kwa sababu wanawake wengi hupiga kura kwa kusukumwa na maamuzi ya myoyo yao, na siyo vichwa vyao! (they vote from their hearts, and not from their heads). Ingefaa Chadema wakalitambua hili -- suala ambalo liko karibu kila nchi hasa zile zenye demokrasia dhaifu kama Tanzania.
 
Tatizo kubwa liko kwenye ulinzi vituo vya kupigia kura.watu inabidi waache njaa na kuokoa nchi yao.

Mkuu ulinzi gani wa vituo vya kura?, huwezi linda vituo vya kura wakati mwizi wa kura analindwa kwa bunduki ili aibe vizuri. Wanaposema watu wakimaliza kupiga kura watawanyike maana yake ni kutoa fursa ya kufanya wayawezayo. As long as vyama vya upinzani vipo kimya tu hakuna wa kukulindia kura kama wewe mwenyewe unakubali kuibiwa. Chama tawala wameshika mpini sasa usidhania hata siku moja utamnyang'anya mpini kwa kumbembeleza wakati yeye akijua fika akiachia tu makali yanageukia kwake. Ninakubaliana kabisa na JK kuwa CCM itaendelea kutawala for unseable future kwani anajua kuuachia mpini ni makosa makubwa kwa mpiganaji. Ndiyo maana anakuambia uchaguzi ni vita mpinzani "akileta kombania wewe unapeleka bataliani akileta bataliani wewe unapeleka brigade akileta brigade wewe unapeleka division"



 
Last edited by a moderator:
Samahani kutoka katika mada ya kura na kuingiza mjadala mdogo wa Kiswahili.

Kusema "Wapiga kura wengi hawapigi kura" ni mkinganyo usioafikika. Ni sawa na kusema "Wakristo wengi si Wakristo" au "Wanadamu wengi si Wanadamu"

Ukishasema "Wapiga kura" maana ninayoipata mimi ni watu waliopiga/ wanaopiga kura. Hizi njia za mkato zinatuharibia lugha na kufanya tuongee bila busara kasi cha kutoeleweka.

Kama unamaanisha "Wenye stahili kupiga kura wengi hawapigi kura" sema hivyo. Kama unamaanisha "Wanaojiandikisha kupiga kura wengi hawapigi kura" sema hivyo. Ukisema "Wapiga kura wengi hawapigi kura" nashindwa kuelewa unamaanisha wenye stahili ya kupiga kura hawapigi kura, wenye kujiandikisha kupiga kura hawapigi kura, wenye kwenda kupiga kura hawapigi kura haswa kwa sababu kura zao hazihesabiwi au madudu gani mengine?

"Wapiga kura wengi hawapigi kura" yeah right, right back at you, "waandishi wengi hawaandiki"
 
Kumbe CHADEMA kina wafuasi katika mikoa isiozidi minne na sehemu zingine zote kwa kila sehemu walioipigia Chadema hawazidi hata mia tano ,seemu zingine wanaambulia kura 20 , hii ni 2010 jambo kubwa gani mliolifanya ambalo litawezeha kujaza wanachama wapiga kura na kiasi mfikie labda kura 30000 pale arusha ambapo kura za Chadema ndipo zilipo ,msifanye mchezo hapa hamgombei ubunge unahitaji kukubalika sehemu kubwa na ndio vyama vingine vifikirie kukuunga mkono.Chadema haikubaliki au labda nisitumie neno hilo niseme haina wafuasi wengi waliochawanyika Tanzania nzima kama ilivyo CUF ambayo hadi vijijini ndani ndani imeshafikisha mtandao na inawanachama wa kuaminika kabisa.Tofauti na Chadema ambao wapo zaidi sehemu ndogo sana hapa Tanzania.

Nionavyo kama kuungwa mkono basi CUF ndio ya kuungwa mkono maana inakura nyingi sana ukichukulia Zanzibar sio kura kidogo na sehemu ya mikoa ya kusini na sehemu kubwa ya Tanzania ukilinganisha na Chadema
 
Makanyaga na Kiranga! Uko sahihi! ila maada yangu inalenga kuelezea kuwa watu wenye uwezo wa kupiga kura(wapiga kura) wengi hawapigi kura( wamejiandikisha lakini hawaendi kupiga kura).

Ndo maana nikaweka hiyo hapo juu ili mtu aweze kubofya hapo na kujionea tofauti ilivyokubwa. Utakuta watu waliojiandikisha niwengi, wanaopiga kura ni chini ya nusu.
 
Mwiba, Tanzania ya l2010 siyo sawa na tanzania ya mwaka 2005. You may say anything you want lakini ukweli upo pale pale kuwa watu wamechoka, nawanataka mabadiriko. Acha kura ziibiwe, lakini cha msingi mabadiriko yawepo.

Hizo kura unazosema, hapo zilipatikana kwa haalali? Subiri makombora 20 ya Dr yatakapoanza kulipuliwa. Mimi na wewe ni mashabiki tu wa siasa, na wapiganaji huru ambao hata hatuko tayari kuona Tanzania ikiendelea kuitwa masikani.

Tusubiri hapo tarehe ya kampeni ikianza.
 
Great thinkers,
Katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 idadi kubwa ya wapiga kura waliojiandikisha na wale waliokwenda vituoni siku ya uchaguzi inafikirisha sana.Watu wengi hawakwenda kupiga kura.
Tujiulize ni kwanini.
1.Rafu za wasiotaka kushindwa ambao hununua kadi za wapiga kura na kuzitupa barabarani wakishatangazwa washindi?
2.Watu wamekata tamaa na hivyo hawaoni umuhimu wa kupiga kura?
3.Watu hawajajua umuhimu wa kupiga kura?

Maswali ni mengi na majibu yake sio mepesi.Sisi tunaojua umuhimu wa kupiga kura tuna jukumu la kutafuts sababu zinazowafanya watu wajiandikishe kwa wingi,mikutano ijae wakati wa kampeni lkn idadi iwe pungufu baada ya matokeo kusomwa/kutangazwa kama tulivyojionea leo hii matokeo ya kura za ubunge wa jimbo la Igunga.
Tutafakari kwa pamoja na tuiokoe nchi yeti iliyo katika hatari ya kuporomoka kwa demokrasia maana uchaguzi bila idadi tosha ya wapiga kura ni upuuzi mtupu unaoweza kuwaweka madarakani wapuuzi na hivyo kuwatia kitanzi watanzania maskini
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom