Kwanini watanzania wengi hawakai karibu na mito?

maji tunaambiwa ni uhai.ukikaa mbali nayo hutaki uhai.
Nimetembea sehemu nyingi tanzania unakuta mito inatiririka maporini ikiwa yatima bila watu karibu wakiwa wanakaa mbali na mito wengine kilomita hata 10 au zaidi toka mto ulipo.

Halafu kitu cha ajabu unakuta wanatuma wabunge wakaombe serikali iwapelekee maji kwani wanachota umbali mrefu kiasi cha kushindwa kufanya shughuli zingine za maendeleo.hivi kwa nini wasihamie karibu na hiyo mito au serikali badala ya kugharimia miondo mbino ya maji iwahamishie huko kisha iachane nao waendelee chota ili wasiendelee sumbua bunge na sirikali?

India kuishi karibu na mto ni bahati sana tena watu hufurahi mito yote imefurika wakazi pembezoni.hivi watanzania wengi vijijini mbona wanakaa mbali na mito kwa nini? Pita njia zote za barabara kuu na ndogo hali ni hiyo.
walikuwa karibu na mito
mnamo mwaka 1974
operation sogeza ilipita
moja ya mitihani iliyojitokeza ni huo.
 
Haihitaji elimu ya darasani kufahamu kuwa kukaa mbali na mito ni miongoni mwa njia za kuhifadhi mazingira, kama watu wakikaa karibu na mito wataharibu mazingira ya mito hiyo kwa kukata miti matokeo yake hiyo mito itakauka na maisha yao na wengine walio upande wa chini au eneo lingine linalotegemea maji kutoka mto huo watapa shida.
 
Hapa nadhani kunahitaji kupitia kwa umakini vinadharia vya uanzishaji wa makazi ili tuone nini kilitokea.
Tunaweza kuanzia na kuchunguza ukuaji mdogo wa Ruvu darajani ukilinganisha na Mlandizi au Chalinze.
Kunahitajika study kabisa.MIJI MINGI MFANO ULAYA ilkua haraka kwenye maeneo karibu na mito
 
Maji tunaambiwa ni uhai.Ukikaa mbali nayo hutaki uhai.
Nimetembea sehemu nyingi Tanzania unakuta mito inatiririka maporini ikiwa yatima bila watu karibu wakiwa wanakaa mbali na mito wengine kilomita hata 10 au zaidi toka mto ulipo.

Halafu kitu cha ajabu unakuta wanatuma wabunge wakaombe serikali iwapelekee maji kwani wanachota umbali mrefu kiasi cha kushindwa kufanya shughuli zingine za maendeleo.Hivi kwa nini wasihamie karibu na hiyo mito au serikali badala ya kugharimia miondo mbino ya maji iwahamishie huko kisha iachane nao waendelee chota Ili wasiendelee sumbua bunge na sirikali?

India kuishi karibu na mto ni bahati sana tena watu hufurahi mito yote imefurika wakazi pembezoni.Hivi watanzania wengi vijijini mbona wanakaa mbali na mito kwa nini? pita njia zote za barabara kuu na ndogo hali ni hiyo.
Labda wanamuogopa mkuu wa wilaya ya hai asije kuwavunjia miundombinu yao kama alivyofanya kwa freeman mbowe
 
Mito mingi ilikuwa haiko deep ndy ilikuwa inaanza hivyo maji Yalikuwa yanatapakaa sana wakati wa mvua.... Chukua mfano mto mdogo wa Msimbaz unavyoitesa Dar Je mto kama Ruvuma,Rufiji Pangani unaobeba maji kutoka Kenya, Kilimanjaro, Arusha na manyara utakuwa na hekaheka zipi mvua zikinyesha?
 
MTO kama rufiji,kilomboro,malagarasi ukajenge karibu,? Unawajua viboko wewe,unawajua mamba we we, unayajua mafuriko we we.Unawezaje kufananisha overpopulated India na Blessed Tanzania !!
 
Mzee bora bahari au maziwa lakini mito CHUNUSI wake sio wa dunia hiii hutalala utajikuta kila siku unaamkia mtoni
 
Sijawahi ona sehemu mzuli na mito inayo toa maji kama bukolwaa sasa walipo kuja geita gold mine nijangwa tu mito isiyo na mafuliko maji ya mapolomoko
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom