Kwanini watanzania hatuna uchungu na nchi yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini watanzania hatuna uchungu na nchi yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kipisi, Jul 16, 2011.

 1. k

  kipisi Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 25
  Ndugu zangu wana jamii forums napenda kuuliza hii swali kwenu wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kwanini watanzania hatuna uchungu na nchi yetu? nimeuliza hivyo kwasababu hali ya nchi yetu kwa sasa ni tete, ukianzia na umeme ni rezo watu wanapoteza kazi hakuna uzalishaji, maduka yanafungwa vyakula kama vile nyama, samaki nk vinaharibika, watu wanapata hasara sana, vibaka ndiyo kwanza wanazidi kusumbua wananchi, imefika kipindi achacho everyone of us should stand up and fight for our country, tatizo la nchi ni viongozi wa nchi ambao ni wabovu na wananchi wengi tunawashabikia
   
 2. n

  ngarauo Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ninauchungu na nchi yangu
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nani kakuambia watu hawana uchungu na nchi yetu? Ukisoma mada nyingi hapa JF utaona jinsi tulivyo na uchungu na nchi yetu na jinsi tusivyoridhishwa na uongozi wa Kikwete na CCM yake.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,540
  Trophy Points: 280
  Naam Mkuu kuwa na uchungu wa nchi haina maana kuingia msituni....lakini watu wanasema sana lakini tatizo tuna wasanii ambao wameziba masikio yao ili kuendeleza ufisadi wao kabla ya kuachia ngazi. Utendaji wa hawa jamaa unastahili kabisa kuwafungulia mashtaka kwa kuhujumu uchumi wa nchi kwa miaka mingi sasa.
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Kusema kweli kama JKT inahusika na kutengeneza uzalendo basi ni bora ikarudishwa haraka sana iwezekanavyo kwa maana sahivi Tanzania ni zaidi ya jehanamu (tunaunguzwa na kuungulia kwenye nchi yetu tukiwa macho) haya mateso hatupigani vita kama somalia na afghanstan lakini hayatofautiana sana na wanayoyapata wasomali

  kuna njaa,kuna mauaji yasiyoelezeka,kuna rushwa ya hatari,mgao ndo usiseme,kuna maonevu kila kona ya nchi hii,on top,cha ajabu na cha kusikitisha ni ukimya unaoendelea kuoneshwa na watanzani,ni zaidi ya kondoo aliyefanyiwa castration,hawajali na wametulia wafe kimya m1 baada ya mwingine mpaka waishe...hivi ni kwa nini tumekuwa neglect kiasi hiki?hivi Tanzania ni nchi yetu kweli ama tulipandikizwa?mbona sasa hatuijali nchi yetu?kwa nini hatuna uchungu na nchi yetu?wakati mwingine namshukuru Mwl.Nyerere na wenzake wao waliweza kuipigania nchi yao toka kwa wakoloni sijuhi kama ndo ingelikuwa ni kazi ya sahv kama sie leo tungeiweza

  Tumekuwa wapole mno mpaka tunageuka wajinga,wapumbavu,mazuzu,mandondo,sisi?
   
 6. M

  MNYAKI MZALENDO Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swali lako c geni kichwani mwangu,labda niwafahamishe wana jf kwamba mbali na malaria,ukimwi na umaskini ugonjwa mwingine unaokula taifa ni KUKOSA UZALENDO.wadau wa elimu lazma tujenge mbinu za kukuza uzalendo ndani ya vichwa vvy watoto wetu ili wawe viongozi bora kesho.PAMOJA TUNAWEZA
   
 7. n

  nitasemaukweli Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa hii changamoto yako mkuu na kweli hapa unasema openly na transparent kama kweli tunataka tubadilishe hili taifa letu lazima to step up big time kwani tunaishia kuwaangalia hawa ccm na maafa walioyaleta na kila ninageuka nasikia jingine tena. when is these things going to stop? Juzi tu nimesikia uda nayo imeshakaangwa na tunapoteza kila aina ya biashara tanzania kutokana na wizi uliotokea wa umeme, kwanini sisi watanzania tusifanye maamuzi kwamba hatutaki hii serikali na kufanya uchaguzi wa ukweli ili tupate viongozi wanaojali taifa letu. Sioni sababu zozote kukaa na kusibiri kikwete arudi na ndege ya wananchi ili tusikie akitoa hotuba yake ya mwezi (wezi)?

  Uchungu wa wananchi kwa nchi yetu unaonekana wazi umepotea siku nyingi na wengi wanaonekana kutojali hali hii ambayo inakuwa mbaya kila tunapoamka asubuhi. Juzi tu nimezika mjomba na kama miezi miwili hivi nimezika mama mdogo na yote haya ni kutokana na ndugu kukata tamaa na maisha na wanapata magonjwa ya blood pressure na kisukari wanakuja kugundua dakika za mwisho na kukata tamaa na maisha kabisa. Hawa ndugu wanaojikuta na kusumbuliwa na magonjwa ya namna hii utasikia wanasema kwani kuna haja gani ya kuishi 'hali ya nyumbani inaonekana haitabailika hivyo hata wakipewa ushahuri na madaktari wanaacha kufuatilia na kama tunavyojua ukikata tamaa na maisha yako hata hizo dawa hazitafanya kazi tena. We are dying inside kutokana na haya matatizo ya inchi yalivyo makubwa, tufanyeni jitihada kuondoa hii serikali ya wahuni haraka sana tusiendelee kupoteza ndugu zetu.


   
 8. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Umefanya lipi kuudhihirisha huo uchungu
   
 9. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  kwahiyo kama wameziba masikio wewe umefanyaje iliyawafunguke extend your thinking capacity
   
 10. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Correct
   
 11. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  kwa maana ya greater thinker wewe kweli nakubali hoja yako big up
   
 12. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hatuhitaji chama kulikomboa hili taifa, hatuhitaji pesa kulikomboa hili taifa, hatuhitaki kengele kuambiwa sasa ni saa ya ukombozi!! Hakuna kiongozi hata mmoja wa chama au ngazi ya juu atakuja kutuambia sasa tuikomboe hii nchi kutoka kwa mkolono mweusi kwani hawa hawa viongozi wanakula sahani moja, wakati mwingine wanatukana kwenye majukwaa just to blind people lakini hawana tofauti.

  Huwezi kujiita kiongozi wa nchi wakati watu unaoongoza hawapati maji, umeme, hospitali kila siku watu zaidi ya 100 wanakufa ( total number nchi nzima), watu wanakula mlo mmoja tena kwa kubahatisha kiongozi umekaa kimya unategemea hawa watu wataishi vipi? Angalau toa hata morali (wape matumaini ya kuishi) siyo kukaa kimyaa wakati watu wanakufa njaa, wanakufa kwa kukosa dawa, wanakufa kwa kukosa umeme, viwanda vinafungwa kisa umeme wa magumashi hata viongozi wetu wamekaa kimyaa. Wananchi hawataki hotuba nzuri, ndefu na yenye maneno matamu bali ni end product. Viongozi wetu wanashindwa kuona kuwa wanatumiwa na watu wenye njaa kama watanzania wenzao waliowaweka madarakani.

  From now, lets start mobilizing the so called wazalendo, tuandamane lini kutoa hiki kilio. We don't need kibali, let them kill us imani yangu damu yetu itawaamsha wengi waliolala na kulikomboa taifa. TUTANGAZE MAANDAMANO YASIYO NA KIKOMO.
   
Loading...