Kwanini wasomi wa Tanzania ni ngumu kufanikiwa kibiashara?

Wakinga wanatumia ndumba sana katika biashara ndiyo maana wako vizuri sana. Wengi wao hawana elimu ila biashara inawaendea vizuri sana. Waganga wao wapo Malawi.
Sio sababu nzito ya kwann wasomi hawafanikiwi kwenye biashara. Kama ni uchawi ndio sababu je wasomi sio wachawi? Kuna sababu nyingi sana kwenye hili na kubwa sana ni kwamba elimu yetu inatuandaa kuajiriwa na sio kujiajiri,hili ndio kubwa zaid hivyo hata mtu huyu afanye nn inahitaji wito na ari ya juu sana kuondokana na hiyo hali ya kuajiriwa. Kingine kuna mdau ameeleza hapo juu kwamba wasomi wanataka kuweka kila kitu kama walivyosoma darasan waweke kwenye mazingira ya biashara wakati huo huo tunasahau elimu nzima ya chuo imetengenezwa kureflect mazingira ya ulaya na amerika ambako ndio waandishi wa hivyo vitabu wanatoka sasa ukifanya aplication ya theory na principles zao huku itaka kwenye kahawa au mbarali kwenye mpunga lazima uangukie pua.
 
nadhani ni swala la priorities na muda.

wakati wewe unaanza kidato cha kwanza, mwenzako anaanza ujasiriamali wa kuuza karanga.

unamiliza kidato cha nne, mwenzako kaachana na biashara ya karanga kahamia kwenye biashara ya duka la jumla.

unaamaliza kidato cha sita mwenzako tayari kaongeza duka lingine la jumla la kuuza vifaa vya ujenzi.

unaanza chuo mwaka wa kwanza, mwenzako tayari ana maarifa na uzoefu mkubwa katika biashara yake, anajua risk zote za biashara anayoifanya na tayari ana network kubwa ya taasisi za kutoa mikopo hivo ni rahisi kwake kukopesheka.

unamiliza chuo mwaka wa tatu au wa nne, mwenzako tayari mtaji wake kibiashara ni mubwa mno. ana uwezo wa kuwa na vitega uchumi mbalimbali.

unamaliza chuo ukiwa mtaani bila kazi mwaka mzima ukitafakari utoke vipi kwa kupitia elimu yako, mwenzako mambo yake yanazidi kimnyokea kibiashara.

hayo ndio mazingira waliyopitia matajiri wengi wa kitanzania ambao hawana elimu. kubwa.
 
Kwa mfano; mr. kidude mwenye digrii moja ya uchumi ana mtaji wa milioni 5 anataka kufungua biashara lakini pia mr. Kituko mwenye elimu ya darasa la 4 ana mtaji wa milioni 5 na yeye anataka kufanya biashara,

mr. Kituko ambaye siyo msomi akaamua kuanza biashara ya chinga pale makoroboi ambapo hana pango la kulipia kwa kila mwezi bali ametengeneza tu kasehemu kakuuzia bidhaa zake, kwa mwaka anatozwa laki na nusu kwa kuuzia hapo bidhaa zake. Bado nyumba yake ya kuishi ni ya kawaida (tsh, elfu 30, 40 au 60 kwa mwezi), baada ya miaka 5 ana mtaji mkubwa hata anaweza kujipanua na kupanga chumba kikubwa cha biashara.

Lakini mr. Kidude yeye aliamua kufungua kampuni ya kibiashara, akatumia gharama kusajili kampuni, akatumia gharama kusajili jina la biashara, leseni ya biashara, kodi ya chumba cha biashara, kodi ya TRA kabla hajaanza biashara, kodi ya Tra baada ya kuanza biashara, gharama za umeme na maji, gharama za mlinzi, gharama za muendesha ofisi, gharama za nyumba anayoishi, kwa ujumla anajikuta anaumia kila mwezi maana biashara inatoa hela mfukoni kila siku ila haiingizi hela mfukoni.

Baada ya miaka 5 mr. Kituko aliyedharaulika kufanya uchinga ametajirika ila mr. Kidude aliyefungua kampuni kujenga jina mjini yuko hoi kabisa.

k
Asante sana chief. Umeeleza kwa mfano mdogo sana ila wenye maana kubwa sana ndani yake. Kama ni darasa wanafunzi wote wanafaulu kuenda kuenda kidato cha tano. Shida wasomi mbwembwe nyingi sana. Mtu ukimwambia biashara ya kuuza bidhaa za matumiz ya nyumban atakwambia box la sabani unajumua 7000/ unauza 8,000/ ukiuza mche mmoja moja unapata 10,000/ sasa msomi atakwambia unatoa 8,000-7,000/ baki 1,000/ ataweka na makorokoro mengine mwisho wa siku anakwambia profit analysis hapo inagoma kabisa wakat huo huo kuna jamaa mtaani huku wanajenga,wanasomesha nk na wengi wa hao wasomi wanapanga nyumba nzima zilizojengwa kwa faida ya hizo hizo biashara ndogo ndogo
 
Elimu yetu inatakiwa iwe zaidi ya vitendo kuliko maneno. Kama unasomea biashara at least wote wafungue vibiashara vidogo online au mtaani wajifunze hali halisi live, kama kilimo, wapewe eneo dogo kulima na kutafuta masoko.
 
Wakinga wanatumia ndumba sana katika biashara ndiyo maana wako vizuri sana. Wengi wao hawana elimu ila biashara inawaendea vizuri sana. Waganga wao wapo Malawi.
umeandika upuuzi mkubwa sana kama hujui kitu kaa kimya wakinga wana akili na nidhamu ya pesa ndio maana wanafanikiwa
 
nadhani ni swala la priorities na muda.

wakati wewe unaanza kidato cha kwanza, mwenzako anaanza ujasiriamali wa kuuza karanga.

unamiliza kidato cha nne, mwenzako kaachana na biashara ya karanga kahamia kwenye biashara ya duka la jumla.

unaamaliza kidato cha sita mwenzako tayari kaongeza duka lingine la jumla la kuuza vifaa vya ujenzi.

unaanza chuo mwaka wa kwanza, mwenzako tayari ana maarifa na uzoefu mkubwa katika biashara yake, anajua risk zote za biashara anayoifanya na tayari ana network kubwa ya taasisi za kutoa mikopo hivo ni rahisi kwake kukopesheka.

unamiliza chuo mwaka wa tatu au wa nne, mwenzako tayari mtaji wake kibiashara ni mubwa mno. ana uwezo wa kuwa na vitega uchumi mbalimbali.

unamaliza chuo ukiwa mtaani bila kazi mwaka mzima ukitafakari utoke vipi kwa kupitia elimu yako, mwenzako mambo yake yanazidi kimnyokea kibiashara.

hayo ndio mazingira waliyopitia matajiri wengi wa kitanzania ambao hawana elimu. kubwa.

Kweli mafanikio si mchezo mchezo
 
Lkn kwa matajiri WAKUBWA wa Tz, nadhani ni bakhresa tu ndo haja bukua.. I mean: Mo, Mengi, Ali mufuruki, Manji... wameenda shulen, wote hao wanazo degree.. Ila kwa kweli wasomi wengi hawafanikiwi, na hii ni kwa sababu kadhaa, mfano: Kupendelea ajira, kuchelewa kuanza biashara (biashara huanzishwa baada ya kuachishwa kaz au kustaafu), over analysis inayofanya karibu kila fursa ionekane haifai, kukosekana uzoefu wa ujasiriamali, pia hio imani ya kusafishwa cjui nyota hawawezi kuwa nayo, nk

OVER ANALYSIS hii point kubwa sana, wanachambua mno
 
Hizi mada zimewaandama wasomi sana kipindi hiki.

ila mimi niwaulize swali nyie mnaowaponda wasomi, "Ni kwa nini vichaa wanakula majalalani na vitu vichafu, hawaogi, wanalala pachafu na mengineyo ila hawaugui"?? Mbona nyie hamfanyi hayo??
 
Biashara inahitaj uvumilivu sana..hasa kama unaanza it need more time kutengemaa...biashara yoyote kubwa unayoiona mwanzo wake ukiambiwa ilivyoanza kimauzo huwez amin..watu ambao hawajasoma kwenye uvumilivu wapo vzur yaan anaweza akapata faida mia mbili mbili lkn akazitunza mpaka zikawa nyingi..wasomi wanakuwa na mategemeo makubwa sana wanapoanzisha biashara ndomana zinafeli...wakat biashara kama biashara inahitaj time ili watu wapozoee na uanze kuuza mfano kama hyo kuuza chips...kitu kingne ni huduma yaan mfano kwa kuuza chips kwa kuanza nmegundua ukiwa unawawekea wateja sahani kwa kuwajazia machips kibao...hii itafanya waambizane kwamba sehmu fulani anajaza kwel"..so ukiwa unawajazia mwanzo halaf ww ukawa unapata faida kidogo ndani ya mwezi au miezi miwili hapo utakuwa umewavuta kwa kiasi kubwa...then ukishaona wamevutika then unarudisha kama kawaida kwa kuweka sahni haijajaa sana...biashara inahitaj
1.lugha nzuri kwa wateja
2.uvumilivu
3.less money is more money..yaan kwa kuanza unaweza ukashusha bei ili kuwavuta wateja
4...................
5...................
6...................
Unaweza ukaongezea vya kwako
 
mimi nikiwa mmoja wao wasomi wa degree 1+ sababu ni nyingi.

1. Miaka mingi inapotea masomoni huyu asiesoma anaanza kujifunza biashara toka umri wa miaka 13 na kuendelea wakati wa degree anaanza 25 na kuendelea huyu msomi anakuja kuanza moja huku asiesoma anaudhoefu wa miaka 12 wa mazingira harisi ya biashara yetu lazima amuache mbali sana huyu msomi.

2. Tunasoma vitabu vya waingereza huku tunafanyia biashara tz lazima uchemke usipojifunza kwa dalasa la saba mzoefu.

3. network yako ni ya waajiriwa huku network ya dalasa la 7 ni wahangaikaji pekee anajua nini akipate wapi? wakati network yako inajua kampuni gani imetangaza ajira.

4. degree holder anakuwa amejenga style ya maisha ambayo haihimili kipato cha biashara mpya. biashara mpya mara nyingi huwa na faida ndogo sana, bila faida na wakati mwingine inajiendesha kihasara wakati huo msomi anataka gari, nyumba nzima ya kuishi, mchumba wa dalaja lake (wigi 1m, ama saloon ya laki 2 kila wiki, bado disco au sinema mwisho wa wiki) wakati la saba hana mahitaji makubwa bado mtoto anakula nyumbani anaishi nyumbani, hana demu, hajui jumba la sinema wala club, hafikrii hata baiskeli lazima dalasa la saba akue hata kwa faida ya elfu 5 kwa siku

5. Degree holder uchambuzi mwiiiingi dalasa la saba anajirusha tu

6. Dalasa la saba akifeli atafanya vibarua ataanza tena hata mara 100 atafeli ataamuka tena but degree holder akifeli once ni for good ataanzia wapi tena hawezi kushika jembe alime avune aanze hawezi kukologa zege mwezi aanze na lk 3 tena.

Sababu ni nyingi sana lkn naamini degree holder akiachana na habari ya degree kwanza apige kazi kwa hali na misingi ya biashara ya hapa tz atafanya vizuri kuliko dalasa la 7
 
Ukichunguza kidogo utagundua kua biashara nyingi zinazofanikiwa ni za watu wakawaida kabisa ambao hata mambo ya biznes plan, demand and suply hawajui

Ukitoa yale makabila ambayo asili zao ni kutafta hela(Dr. Mengi) yaani wasomi wengi wenye kuanzia degree+ hata maprofesa hata wakianzisha biashara ya bagia ya mtaji wa 3000 huishia kuangukia pua.

Lakini ndugu zangu walioshia la 3 b hata mambo ya bissnes plan, strategies, sijui kusoma mavitabu ya 4 WAYS TO BE RICH hawayajui lakini ndio wanao run biashara za bongo kuanzia vijijini hadi mijini.

Na hapa ndipo hua nashangaa, inakuaje wasomi wetu huangukia pua? Japokua
wanamaarifa ya kila namna.

Nawasilisha
kufanya Biashara nayo ni kipaji au fani kama zilivyo nyingine. Kwa hiyo msomi mwenye kipaji atafanikiwa na pia asiye msomi ila ana kipaji nayeye atafanikiwa. Na kama hauna kipaji ni lazima ukubali kujifunza. Tatizo watu wanaamua kufanya biashara baada ya plan zao kufeli au kufuata mkumbo na bahati mbaya wanaingia wakiwa na expectations kubwa kuliko uhalisia. Na kila kitu unacho fanya ina bidi ujifunze n hii process ni ngumu na huweza kuwa ndefu kuliko inavyo tegemewa.
 
nadhani ni swala la priorities na muda.

wakati wewe unaanza kidato cha kwanza, mwenzako anaanza ujasiriamali wa kuuza karanga.

unamiliza kidato cha nne, mwenzako kaachana na biashara ya karanga kahamia kwenye biashara ya duka la jumla.

unaamaliza kidato cha sita mwenzako tayari kaongeza duka lingine la jumla la kuuza vifaa vya ujenzi.

unaanza chuo mwaka wa kwanza, mwenzako tayari ana maarifa na uzoefu mkubwa katika biashara yake, anajua risk zote za biashara anayoifanya na tayari ana network kubwa ya taasisi za kutoa mikopo hivo ni rahisi kwake kukopesheka.

unamiliza chuo mwaka wa tatu au wa nne, mwenzako tayari mtaji wake kibiashara ni mubwa mno. ana uwezo wa kuwa na vitega uchumi mbalimbali.

unamaliza chuo ukiwa mtaani bila kazi mwaka mzima ukitafakari utoke vipi kwa kupitia elimu yako, mwenzako mambo yake yanazidi kimnyokea kibiashara.

hayo ndio mazingira waliyopitia matajiri wengi wa kitanzania ambao hawana elimu. kubwa.
Wewe umefika chuo kikuu? Umekuta na mtu uliyesoma naye amefikia mafanikio hayo unayosema hapa.

Kama hujafika chuo kukuu,je wewe umefikia mafanikio hayo?
 
hata nikiweka wazi kiwango changu cha elimu au mafanikio yangu kibiashara, bado haiondoi ukweli wa alichoandika mleta mada kwenye mada kuu kuhusu wasomi wa tanzania na masuala ya biashara.
 
mimi nikiwa mmoja wao wasomi wa degree 1+ sababu ni nyingi.

1. Miaka mingi inapotea masomoni huyu asiesoma anaanza kujifunza biashara toka umri wa miaka 13 na kuendelea wakati wa degree anaanza 25 na kuendelea huyu msomi anakuja kuanza moja huku asiesoma anaudhoefu wa miaka 12 wa mazingira harisi ya biashara yetu lazima amuache mbali sana huyu msomi.

2. Tunasoma vitabu vya waingereza huku tunafanyia biashara tz lazima uchemke usipojifunza kwa dalasa la saba mzoefu.

3. network yako ni ya waajiriwa huku network ya dalasa la 7 ni wahangaikaji pekee anajua nini akipate wapi? wakati network yako inajua kampuni gani imetangaza ajira.

4. degree holder anakuwa amejenga style ya maisha ambayo haihimili kipato cha biashara mpya. biashara mpya mara nyingi huwa na faida ndogo sana, bila faida na wakati mwingine inajiendesha kihasara wakati huo msomi anataka gari, nyumba nzima ya kuishi, mchumba wa dalaja lake (wigi 1m, ama saloon ya laki 2 kila wiki, bado disco au sinema mwisho wa wiki) wakati la saba hana mahitaji makubwa bado mtoto anakula nyumbani anaishi nyumbani, hana demu, hajui jumba la sinema wala club, hafikrii hata baiskeli lazima dalasa la saba akue hata kwa faida ya elfu 5 kwa siku

5. Degree holder uchambuzi mwiiiingi dalasa la saba anajirusha tu

6. Dalasa la saba akifeli atafanya vibarua ataanza tena hata mara 100 atafeli ataamuka tena but degree holder akifeli once ni for good ataanzia wapi tena hawezi kushika jembe alime avune aanze hawezi kukologa zege mwezi aanze na lk 3 tena.

Sababu ni nyingi sana lkn naamini degree holder akiachana na habari ya degree kwanza apige kazi kwa hali na misingi ya biashara ya hapa tz atafanya vizuri kuliko dalasa la 7
good analysis. spot on.
 
Wakinga wanatumia ndumba sana katika biashara ndiyo maana wako vizuri sana. Wengi wao hawana elimu ila biashara inawaendea vizuri sana. Waganga wao wapo Malawi.
Ikiwa kweli Wakinga wanatumia ndumba na wanafanikiwa basi ni bora hao kuliko wasomi ambao hawafanikiwi.

Ikiwa ni kweli na imethibitishwa kuwa mafanikio ya Wakinga yanaletewa na ndumba basi ni bora kutumia ndumba kuliko kufanya ujinga wa kusoma na ukashindwa kufanikiwa.
Hakika Wakinga wana maarifa makubwa kuliko hao wanaojiita wasomi.
 
Back
Top Bottom