Kwanini Wasanii wanaishi kama mazombi?

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,825
3,664
Je unapenda kujua mazombi yanaishije?
Usipate taabu, angalia mifumo ya maisha ya wasanii wetu. Asilimia kubwa ya wasanii hao si rahisi kutenganisha mitindo ya maisha yao na mazombi, kimsingi wanaishi kama mazombi. Unadhani wanafanya kusudi? Huenda hata wao wanadhani wanafanya kusudi au wanatengeneza kiki ila hawa watu ni wagonjwa, ni wa kuonewa huruma, wanaumwa!

Chukua muda wako mfikirie Wema Sepetu, kisha yaangazie maisha ya Hamisa Mobetto halafu vuta taswira ya Rubby, mtazame Wolper, kisha rudi kwa Ray C kabla hujamfikiria Recho na dada machupi almaarufu kama Nandy, usisahau vitimbi vya Zamaradi wala majanga ya bi dada Diva the boss lady, hii orodha haijamsau Sheila (Irine Uwoya)

Turudi kiumeni sasa, mtazame Darasa, Chid Benzi na Young Dee na usiache kumuwaza Diamond na nduguze akina Rommy Jones, halafu turudi kwa Baraka da prince, TID na Q Chillah. Hawa na wengine wengi kiukweli wanaishi kama mizimu.

Wasanii wetu wanaweza wakafanya kitu hadi ukabaki kinywa wazi. Asubuhi atakuambia yeye ni dada mifweza a.k.a diva ze boss halafu jioni atatembeza bakuli la michango akatibiwe. Huyu ataiba mshono halafu akiulizwa atasema wanamuonea donge kisa yeye ni brand na wala tusijue kama aliiba kweli au hakuiba. Mwingine tutashirikiana nae leo kumzika mwenzake aliyekufa kutokana na athari za madawa ya kulevya halafu kesho tutaanza kumuuguza yeye kutokana na athari za madawa ya kulevya. Huyu atasema ana nyumba ya milioni 400 halafu kesho utasikia kanyang'anywa hiyo nyumba na hana pa kuishi. Huu kama sio uzombi tuuitaje?

Hawa ni wagonjwa, Wanaumwa Narcissistic personality disorder (NPD). Narcissistic personality disorder ni hali ya mtu kuwa na tabia ya ubinafsi uliopitiliza, kujihisi yeye ni wa muhimu kuliko wengine tofauti na uhalisia na kutokuwa na huruma. Dalili ya mtu mwenye Narcissistic personality disorder ni
-kujiona ana uwezo na mafanikio makubwa (kuliko uhalisia)
-kupenda sana attention, anataka kukubalika kila sehemu kukubalika kupenda kusifiwa.
-Kujiona yeye ni wa pekee na muhimu hivyo anatakiwa kuwa na watu kama yeye
-Kuwanyonya wengine ili afaidike yeye
-Anatakiwa kupata special treatment kila sehemu
-Kujihisi anapendwa na kila mtu

Mtu yeyote mwenye mitazamo kama hiyo hawezi kuuishi uhalisia, ni kama yupo njozini sababu anayoyataka hayawezekani katika mazingira ya kawaida. Wasanii wengi wanatamani kila wakati wawe vinywani mwa watu bahati mbaya si mara zote hili huwezekana. Kuna wakati kazi zao zinashindwa kuzua gumzo mtaani hivyo wanajikuta wanafanya mambo ambayo yatawafanya wawe gumzo kuna wakati wanafanya mambo ya hatari kweli. Wanahisi ni kiki, kwa hiyo atafanya kiki mara ya kwanza, atafanya tena kiki mwisho wa siku maisha yake yanakuwa kiki na hii hali iamleta tu athari mbaya kwao, ni kama addiction ikikukaa unaishi kwa shida.

Hakuna mtu anayekuwa juu milele, kuna wakati inafikia hata kiki inagoma, kila anachofanya hakimfanyi awe relevant mitaani hivyo anapata msongo wa mawazo. Anahisi kila mtu anamsema yeye, anakosa kujiamini, anashinda peke yake na haioni dhamani ya maisha. Alizoea maisha ya gharama sasa kazi zake haziuzi tena hivyo anafanya compensation wengine wanaingia kwenye ulevi, wanatumia madawa ya kulevya, wengine wanakuwa malaya wa kutupwa na uhovyo hovyo mwingine.

Kuna tofauti kati ya mtu mwenye Narcissistic personality traits na mtu mwenye Narcissistic personality disorder. Mfano watu wengi wanapokuwa katika umri wa balahe huwa wankuwa na Narcissistic personality traits ila huwa haizidi hadi kuwa Narcissistic personality disorder. Hawa wasanii wetu imezidi hadi wanaanza kuishi kama mazombi. Ni ishu ya kisaikolojia zaidi, wengi inahitaji msaada wa ushauri kupitia psychoanalysis. Hii ikifanyika wengi inatawasaidia. Inabidi waambiwe its okay not to be okay. Wao ni binaadamu tu wasijibebeshe madeni wasiyoweza kuyalipa (kuwa juu milele), wajue kutokuwa midomoni mwa watu kwa wakati fulani ni kawaida na wala sio dhambi.
Waambiwe kuwa hata wanapotaka kufanya compensation basi wafanye in a positive way.

Wasiishi kama mazombi.
 
Hizo sifa za NPD mbona watu kibao humu jf tunazo!!? Tusiwaseme wasanii peke yao
 
Ni wasanii wachache sana and possible asilimia 5% ya wasanii wenye NPD. NPD inatokana na malezi ya mtu akiwa utotoni..

Katika age ya 3 year ndipo personality ya mtu huwa inatengenezwa.. so kama wazaz walikuwa arogant, kumtenga mtoto..kuto kumjali ktk hiyo age wanatengeneza PD kwa mtoto wao. Akiwa mkubwa ndipo anaanza kusaka vile vitu ambavyo alikusoa utotoni kutoka kwa wazazii...

Ndio maana watu wenye NPD wanakuwa na tabia za watoto wenye miaka mitano. Hii usababishwa na sehem moja ya ubongo wao kutokukua.

Unaowaona hao wasanii wengi hawana NPD... wengi ni "flying monkeys" ana wapambe wa watu wenye NPD.
NPDs huwa wana recruit flying monkeys ili wawatetee, wawashabikie, wafunike maov yao pale wanapokosea.. in short ni waumini wao.
Ndio maana unaona kama wanafanana.. flani hiv.

And NPD inatokea sanasana kwa wanaume.. BPD inatokea sana sana kwa wanawake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa, waache kuishi kama mazombi, wanapaswa kuishi kama mashetani! huo ndio utaratibu tuliojiwekea.
Agenda.. hapo kuna master and puppet. Wengi ni puppet a.k.a waumini wa wasanii wenye NPDs.
Kitaalamu wanaitwa "flying monkeys", wako maalumu kuabudu, kumlamba miguu, kufunika maovu, kumtetea yule wanae ona ni superior wao(person with NPD)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom