mleta mada naungana na wewe ila ukweli ni kwamba yanahitajika maandalizi ya kutosha na mazoezi ya kutosha asikuambie mtu wasanii wa nchi zilizoendelea wanafanya sana mazoezi na pumzi ya kutosha ukiwa na muda uwe unanunua documentary zao uone wanavyopelekeshwa na ratiba zao wamepangiwa kabisa ratiba za mazoezi ya viungo, kuimba, kucheza, na hata chakula gani utumie,na kila kitu na hata kuongea na media wanafundishwa ukiulizwa swali la kijinga uwe unajibu hivi sisi wa bongo huwa tunawaona final pale tu kwenye TV hatujui huko nyuma process gani zimepitiwa mpka afike hapo kwenye kioo sasa msanii wa bongo fleva akiamka tu anasema nataka kuwa kama Jayz kitu ambacho hakipo duniani na vile vile nidhamu ni kitu cha maana sana kwenye sanaa haya masifa sifa kwenye magazeti ya makorokocho yanawatia kiburi sana sasa akifika kwenye stage siku moja tu akiimba watu weweeeeeeee!!!! kichwa kinamviiiimba anasahau hata kilichompeleka pale, bado wanahitaji ushauri pia ila tutafika siku moja watajafanya vizuri maana kuna wasanii wengine wanajitahidi ila hawajafikia bado kile kiwango kitakachowafurahisha baadhi ya washabiki wanaotaka show ichezwe na sio uimbe kwaya tu maana wimbo wako tunaujua sisi tunataka utuchezee hiyo show na kama hauchezwi create something else kitakacho tuvutia sisi tusiendelee kuwa bored. na bangi pia na madawa ya kulevya nayo yanachagia wenzetu wanatumia hivyo ila wanamaisha tayari. bongo unayatumia halafu unaenda kula ugali na maharage utapona kweli?? unatakiwa ule mlo kamili na kwa wakati, ona watumiaji wasanii wakibongo wanavyopuputika ni full skeleton,