Kwanini wasanii wa Bongo wabovu stejini?

Mastabenja

Member
Mar 23, 2012
25
6
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda utumbuizaji wa wasanii wetu stejini hasa wa bongo fleva na kwaya.kwa kweli wanaboa sana na kutia kinyaa _kinachofanyika ni ***** mtupu
1.wengi hawawezi kuimba live.diamond,rose muhando,jay,suma lee wote wachovu hawawezi kuimba live huishia kufanya maigizo tu .hii ni tofauti sana na wasanii wa nje na wasanii wa miaka ya nyuma
2.wengi hawaimbii huishia kuchezacheza na kusema piga kelele-yaani ***** mtupu
hii nitofauti sana na wasanii wa nje wao utaona wanaimba live kwa uwezo wa hali ya juu sana mpaka mtu unafurahia kuangalia
 
wameanza zamani,sisi tumeanza juzi sasa unategemea tutakua sawa,ONE STEP AT A TIME.
huwezi kuanza kukimbia wakati ata kutambaa bado
 
uaipende kulaumu tu bila sababu..af acha....... wako.ushacheki sho ya A.Y na mwanafa au johmakini wanapumzi na show nzuri na unavyofananisha na msanii wa nje toa mfano usigeneralize
 
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa muziki wa bongo utagundua kwamba wameanza kubadilila ama kupiga hatua na zaidi ya yote suala la kupiga live si kwamba wanashindwa kwani tumeshaona wengi wanapokuwa subjected kwenye mazingira ambayo wanapigiwa vyombo basi wanaimba vizuri sana ni suala la uwezo na muandaaji wa shoo.
 
Sasa mtu anaimba 'Playback' unategemea nini ?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kusema ukweli ukitaka muziki LIVE ni Twanga na Ngwasuma tu, hawa Bongo Fleva bado sijawahi kuona Show Live kama aliyoifanya Sugu pale kwenye viwanja vya Ustawi wa Jamii, sijui kama alipania sana au ndio viwango vyake.

Kwa mara ya kwanza nilimshuhudia msanii wa Bongo Fleva akiimba nyimo zake kavu kavu tena kwa ufasaha kabisa kama zilivyorekodiwa kwenye Cd's. kwakeli Sugu anastahili heshima kwenye hili, na kitu kingine ni nidhamu ya kazi, kwenye ile Show Sugu hakuruhusu msanii yeyote kunywa pombe mpaka wamalize Show.
 
mleta mada naungana na wewe ila ukweli ni kwamba yanahitajika maandalizi ya kutosha na mazoezi ya kutosha asikuambie mtu wasanii wa nchi zilizoendelea wanafanya sana mazoezi na pumzi ya kutosha ukiwa na muda uwe unanunua documentary zao uone wanavyopelekeshwa na ratiba zao wamepangiwa kabisa ratiba za mazoezi ya viungo, kuimba, kucheza, na hata chakula gani utumie,na kila kitu na hata kuongea na media wanafundishwa ukiulizwa swali la kijinga uwe unajibu hivi sisi wa bongo huwa tunawaona final pale tu kwenye TV hatujui huko nyuma process gani zimepitiwa mpka afike hapo kwenye kioo sasa msanii wa bongo fleva akiamka tu anasema nataka kuwa kama Jayz kitu ambacho hakipo duniani na vile vile nidhamu ni kitu cha maana sana kwenye sanaa haya masifa sifa kwenye magazeti ya makorokocho yanawatia kiburi sana sasa akifika kwenye stage siku moja tu akiimba watu weweeeeeeee!!!! kichwa kinamviiiimba anasahau hata kilichompeleka pale, bado wanahitaji ushauri pia ila tutafika siku moja watajafanya vizuri maana kuna wasanii wengine wanajitahidi ila hawajafikia bado kile kiwango kitakachowafurahisha baadhi ya washabiki wanaotaka show ichezwe na sio uimbe kwaya tu maana wimbo wako tunaujua sisi tunataka utuchezee hiyo show na kama hauchezwi create something else kitakacho tuvutia sisi tusiendelee kuwa bored. na bangi pia na madawa ya kulevya nayo yanachagia wenzetu wanatumia hivyo ila wanamaisha tayari. bongo unayatumia halafu unaenda kula ugali na maharage utapona kweli?? unatakiwa ule mlo kamili na kwa wakati, ona watumiaji wasanii wakibongo wanavyopuputika ni full skeleton,
 
tatizo lao ni hili: waliamua kuwa wasanii baada kukosa kazi zote duniani!
 
ww kuna ma artist wa zamani wa bongo walikuwa wakiimba live ww mwenyewe unasimama.mfano wakina Muheshimiwa SUGU,GWM na wengineo palikuwa hapatoshi
 
PUN'ZI ni tatizo kubwa kwa wasanii wetu. Vijana hawana PUN'ZI kabisa.. wakiimba dakika mbili tu wanaanza kuhema ka wanakata roho. We si unawaona walivyoota mavitambi? Mazoezi hamna, bia na vitimoto kwa sana, bange, unga n.k..
We ukienda kwene shoo tegemea makelele tuuu na kuona watu wanaotiririkwa majasho.. basi. Rubudani zero!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom