Kwanini Wanaume Werevu na Wasomi waliobobea huoa wanawake wenye Elimu ya wastani?

Hawataki maumivu ya kichwa..
Wanawake wasio na shule iliyopitiliza kumbe ni ma pain killer..... safi sana. Sikulijua hilo.
Kuna jamaa alioa bonge la sista duu, wakaenda nalo Mbeya, basi yule msichana akata aonyeshwe miti ya chips,
alipo onyeshwa viazi akauliza kwa hiyo hiii ndio michipschips? Ikiwa mikubwa inatoa matunda ya chips ehhh.
 
Wanawake wasio na shule iliyopitiliza kumbe ni ma pain killer..... safi sana. Sikulijua hilo.
Kuna jamaa alioa bonge la sista duu, wakaenda nalo Mbeya, basi yule msichana akata aonyeshwe miti ya chips,
alipo onyeshwa viazi akauliza kwa hiyo hiii ndio michipschips? Ikiwa mikubwa inatoa matunda ya chips ehhh.

huyo atakuwa alikuwa ana ugonjwa wa akili
 
Ni bahati mbaya sana kuona kuna idadi ya watu walio wengi kuwaheshimu wengine ili tu kutimiza matakwa yao, wakiweza kujitimizia wenyewe mahitaji yao Heshima na kusikilizana hamna tena. Ndio maana wahenga walisema ''Mwenye kutoa mahitaji huheshimiwa'' Ni bahati mbaya sana sana.

Ukitaka kulifahamu vizuri hili angalia MWAFRIKA aliyeinuka kiuchumi kutoka kwenye utegemezi awe mme awe mke, awe rafiki awe yeyote. Akiweza kuwa na unyenyekevu na heshima aliokuwa nayo kabla... ni moja kati ya kumi. Kwa nini? usiniulize tafadhali. Kuoanisha nilichokiandika hapa na mada husika, changanya na zakwako.

Pili: Ni uoga (Inferiority complex) na nadharia fulani fulani iliojengeka juu ya wanawake waliosoma sana au kuendelea sana... japo ina ukweli fulani kwa wengi wao, Wanapumbazwa sana na mali zao wakasahau nafasi ya Mwanaume katika maisha yao... maana wakimtaka mwanaume waweza kumhonga tu au vinginevyo wakajiridhisha. So ukiona ndoa nyingi za wenye mali, ni chache sana kati yao zenye ORDER.

Tatu: Kiburi cha mafanikio... Kama waweza kupata maziwa, kwa nini ufuge ng'ombe?

Nne: Nafasi ya mafanikio katika nafsi ya mtu, muda anaotumia kuyaendeleza, kuwekeza, muda na familia, etc etc.

Samahani sana nimewajibia MAPROFESA WAKATI sijawahi kuwa profesa.. Mimi nina kasetifiketi kangu tu hapa ka Elimu Dunia kama ndugu yangu Mbwiga mbwiguke.
 
mtoa mada unaongelea Jakaya kikwete na mama salma, pinda na mama tunu pinda au lowassa na regina lowassa???

Hawa wanasiasa sio wajinga kuoa walimu wakati wao walifika chuo kikuu enzi hizo. chuo kikuu si mchezo na ndoa zao zimedumu mpaka leo..
mkapa alijaribu kuoa msomi mwisho wa siku anaishi kibachelor katika uzee wake na mkewe wa ndoa yupo hai kazalishwa na wengine..


au unaongelea Mengi na K lyn / Luca Neghesti na Nancy sumari ????



mi nawapenda sana waislam. hata mwanamke awe na elimu vipi.. anavaa baibui lake na anamuheshimu mumewe bila mbwembwe...
 
uoga wao tu.

mwanamke akisoma anaogopwa na walioenda shule na wasio enda shule.
wanaume wamezoe kutawala wanawake, sasa kumtawala mtu alienda shule ni kimbembe, hapo ndio mnapoomba pooooo!
 
Ukweli ni kwamba sisi ambao tunafanya nao kazi tunawaona na pia twajua ukweli zaidi.

Hata mimi nataka kuoa mwanamke anayenizidi elimu na kipato japokuwa najua ukweli kuwa it will be hard to make order ina my family for real. Niko tayari kwa sababu ninaamini kwangu itakuwa tofauti.

Wanawake wenye elimu kubwa na kazi nzuri na mkawa level moja huwa ni vigumu kuishi nao. Wengi tunawasikia wakitamka na kuonesha vitendo kuwa mme wake wa kwanza ni hela alizo nazo au TGTS yake.

Ngoja na wenzangu waje waseme ila kuoa mwanamke mwenye uwezo sawa na mwanaume ni kukaribisha stress ndani ya maisha yako.
 
Ukitaka mambo yaende utakavyo ndani ya ndoa oa mwanamke asie na kisomo(au kisomo kikubwa) au kama unataka mambo yaendo sivyo ndivyo si kwa urahisi kwa nguvu tena kwa malumbano mengi pasua kichwa oa alieenda shule level za shahada ya kwanza kwenda mbele
 
Kwa ufupi mwanaume ama mwanamke yeyote anahitaji utulivu wa kutosha ndani ya familia bila kujali utulivu huo unaletwa na msomi ama asiye msomi,

Sina hakika na na tafiti zilizofanyika kama zimethibitisha hilo kuwa wasomi wengi hupenda kuoa/kuolewa na wanaowazidi sana kielimu lkn ujumla hii inatokana na ama wengi wao hujikuta wakikabiliwa na majukumu mengi ya shughuli zao hivyo huitaji mwenza mwenye kupata nafasi ama muda wa kutosha kuilea familia na kupata utulivu pindi anapohitaji utulivu huo,

Dhana ya uoga sidhani kama ni sahihi sana. Hivyo mtazamo wangu ni kwamba wasomi hasa hao maprofesor wanakimbilia huko ili kutafuta tulivu huo, lkn pia wako wachache wanaoishi na wanawake ama wanaume wasomi wenzao na wanaonekana maisha yao yako sawia kabisa
 
Maprofesor wanawake wanaoa na kuacha tena wanawaoa wale ambao ni maform iv leaver kwa ajili ya kuwapa starehe tu kama hutaki basi mimi sikuchapi
. Kuoa mwanamke aliyekuzidi elimu unatafuta stress they are not submissive to their husb.
 
Back
Top Bottom