Kwanini wanaume tunakuwa wazito kutoa Password za simu kwa wapenzi wetu?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,680
8,868
Mimi najiuliza kila kukicha sipati jibu unakuta unampenzi wako na unampenda sana tena unamfanyia kila kitu na unaonyesha upo muwazi kwake yeye anakuwa muwazi kwako hadi kadi za benki anakuoa Nywira zake(Password) za simu na kadi na kadi za Benk.

Ila sasa wewe Mwanamume tunakuwa wazito kumpa Password za simu zetu kwanini?

Nikwamba hatuwaamini au tunakuwa tuna makandokando bado?

Ni kwanini au sisi siyo waaminifu?

Mimi nimempa wangu kila kitu password zote Bank na Simu.
 
We si unasema umempa za benki na za simu? sasa kwamba wanaume hatuwapi password umeitoa wapi? au wewe siyo mwanaume!! mbona wanawake nao wanazo password kwenye simu zao?
 
Mie labda za bank ndo unipe, sasa password za simu za kazi gani..... Kujitia tu presha!!! Nipe za Bank mara moja moja niwe nakusaidia kwenda kutoa bhana
 
password ina maana kuwa kuna mambo fulani katika simu yako ambayo kwa sababu zako mwenyewe hutaki yajulikane na mwenzako..iwe conversations na michepuko au picha fulani..wakati mwingine kuna video za ngono na hivyo unahisi mwenzako akiziona huenda akakushangaa...ila mm password simpi mke wangu maana mara nyingi huwa natumia simu yangu kuhifadhia faili za kazini...
 
27c4e0ed16fcd30a87d8e05f2f660110.jpg
 
Wewe kwa kuwa unaaminiana na mke wako ndio umempa kila password ee..siku mambo yakigeuka ulete mrejesho huku
 
Kama mnaaminiana mipasswadi ya nini???lazima mjiamini mm na aweke wala simuulizi na hivo vikadi vyake vya benki na akae navyo sina haja
 
Mimi najiuliza kila kukicha sipati jibu unakuta unampenzi wako na unampenda sana tena unamfanyia kila kitu na unaonyesha upo muwazi kwake yeye anakuwa muwazi kwako hadi kadi za benki anakuoa Nywira zake(Password) za simu na kadi na kadi za Benk.

Ila sasa wewe Mwanamume tunakuwa wazito kumpa Password za simu zetu kwanini?

Nikwamba hatuwaamini au tunakuwa tuna makandokando bado?

Ni kwanini au sisi siyo waaminifu?

Mimi nimempa wangu kila kitu password zote Bank na Simu.
Kiongozi mbona kama akili yako imepiga uturn?
 
Back
Top Bottom