Kwanini wanasiasa wengi hupenda kujiita vijana? Wakati umri umeenda?

gwavara

Member
Apr 5, 2012
37
5
Watanzania wenzangu naomba mnisaidie Ujana unaishia miaka mingapi kwani Watanzania wengi hususan Wanasiasa wamekuwa hawataki kutoka kwenye hili daraja na siku zote wanang'ang'ana kwenye Ujana.

JK mwaka 2005 akiwa anagombea Urais alijinadi kuwa ni Kijana wakati akiwa na miaka 55.Watu kama akina Zitto Kabwe na Filikunjombe,Bulaya na January wanajiita vijana wakati umri wao unazidi miaka 35.Nijuavyo mimi Ujana unaanzia miaka 18-35.Naomba mnisaidie katika hili sababu Watz wengi wanapenda kuonekana wadogo kiumri wakati siyo uhalisia wao.

Tumeona hata kwenye Uchaguzi wa Mwanasiasa Kijana humu JF kuna watu wa Makamo nao wanachaguliwa kama vijana wakati umri umeshapita.Naomba Watanzania wote tuelimishane maana ya Kijana sababu kuna Wazee wengine sababu ya mawazo yao mazuri nao wanapenda waonekane Vijana. Lakini Ki uhalisia Ujana ni umri.
 
Tumeona hata kwenye Uchaguzi wa Mwanasiasa Kijana humu JF kuna watu wa Makamo nao wanachaguliwa kama vijana wakati umri
una uhakika gani kama ni wazee una vielelezo vyovyote kusupport usemi wako.
 
tehe tehe ujana raha wadau! We acha tu, sasa mtu km wassira na yeye ajiite kijana si matusi sasa hayo
 
Uko sahihi kwamba ujana unatakiwa wishie miaka 35, basically half of the life expected and going chini ndio vijana, life expectancy was basically 70 years.

niaibu una mwaka 45, namtotowako amefikisha mwaka 21 wote mnaitwa vijana.
 
Limit ya Umri wa ujana inapangwa na watu, so, mtu yeyote anaweza akajiwekea limit yake ya ujana.
 
Kwani kuwa kijana unapangiwa na nani?. Mungu hajapanga ujana, mi nadhan ujana unaupanga mwenyewe. Na uzee unakuja wenyewe. Hiv km zito au nape tuwaite wazee?. Na mzee wa gombe ataitwaje?.
 
Back
Top Bottom