Kwanini wanasiasa hawafungwi?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Mpaka umri huu sijawahi kusikia au kuona mwanasiasa anafungwa yaani anahukumiwa kwenda jela halafu anatumikia kifungo hadi kinaisha,sijawahi!!!

Nimewahi kusikia wanasiasa wanashtakiwa na kuachiwa au wanahukumiwa ila wanaachiwa baada ya muda fulani bila kutumikia kifungo kikaisha

Wanasiasa ambao nimewahi kusikia wanafungwa na mpaka sasa wapo gerezani wengine ni level ya madiwani na wenyeviti vijiji/mtaa,ukifuatilia makosa yao ni uhujumu uchumi si zaidi ya milioni 50

Hizi sheria za kudhibiti uhalifu ni kwa watu masikini na wasiojulikana

Namhitaji DPP tubagain mdogo wangu yupo jela kifungo cha mwaka mmoja kwa kuiba kuku

No one is above the law,lakini wanasiasa wa ngazi za juu na watu maarufu wapo above the law tusidanyike!!!!!
 
Ukiwa CCM, halafU ukaenda gerezani wewe ni mzembe. Jamaa wanaendesha mambo watakavyo, na sio kwa misingi ya sheria
 
Ongea na mwanasheria wa Serikali anayemuwakilisha ndugu yako, kama ataweza kukubaliana na dpp.
 
Hawafungwi kwasababu wanaajili wanasheria au mawakili wazuri. Mdogo wako kafungwa kwakukosa utetezi wenye nguvu kisheria. Sometimes mahakamani Kuna option yakulipa pesa, kifungo au vyote kwapamoja. Sasa huyo mwizi wa kuku akiambiwa alipe faini ya laki tu mgogoro hivyo chaguo linalobaki ni kifungo.

Vile vile wanasiasa wanamahusiano mazuri na mahakimu kwahiyo yanafungwa mahusiano na sio mtu.
 
daniel yona na basil mramba walifungwa na wote waliwahi kushika nafasi za uwaziri katika wizara mbalimbali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom