Kwanini wanandoa wakifumaniwa mwanamke hapigwi?

hahahahahahahaha uwiiii kujua ukweli baada ya kipondo jamani, si bora ufanye chunguzi kabla ya adhabu
nina hasira kali huwa siwezi kuvumilia ila nikivumilia ujue nimeweka kinyongo maana mimi sio mtu mzuri
 
Yesu aliwaambia wale jamaa waliokuwa wanataka kumpiga mawe yule mwanamke aliyefuniwa mpaka afe na asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe then jamaa wakamwacha. Soma Injili ya Yohana sura ya 8, aya ya 1 mpaka ya 11.
sawa mkuu haya maneno ninayakumbuka, kwa hiyo na wewe umepata/umejihakikishia sehemu ya kujitetea sio ili uwamege wake wa watu kisawasawa sio?
 
sawa mkuu haya maneno ninayakumbuka, kwa hiyo na wewe umepata/umejihakikishia sehemu ya kujitetea sio ili uwamege wake wa watu kisawasawa sio?

Hapana! Maana yangu ni kwamba kasumba hii ni ya siku nyingi sana mpaka kwenye vitabu imesemwa.
 
Ni ufinyu wa akili kupanga kabisa kuwa unaenda kufumania. Siko kwenye taasisi ya ndoa hivo sisemi sana............. ila iwapo ningekuwa kwenye ndoa whether mume wangu angekuwa anazini na kuwa na nyumba ndogo hata 20 hata siku moja nisingepanga kwenda kumfumania ati hotelini au guest au kwenye gari au kazini.

Sana sana ningekuwa busy kujifunza lugha mbali mbali za dunia hii mfano kireno, kispaniola, ki Italy, kifaransa, pia ningekuwa busy zaidi kujifunza lugha za makabila zaidi ya 30 ya Tanzania mfano kingoni, kiha, kisandawe, kimasai, kimakonde, kihaya. ... yaani ningekuwa boonge ya linguistic halafu hayo mawazo ya kufumania mume yangetoka wapi......

Hahahahahhaa crazy Kasie ndo maana sikupangiwa kuingia kwenye hiyo taasisi ya kufumaniana maana wangesema nimewehuka kwa jinsi ambavyo ninge behave.

Kasie.
SMART
 
kwa nini asipigwe nae si katenda kosa? mkuu na wasiwasi na uelewa wa ubongo wako. kwa hiyo hata binti yako akitenda makosa hutamchapa kisa nimwanamke?

Binti yangu na mtoto wangu! Mke hapigwi ... Zipo adhabu lakini sio kipigo.. Pwani sisi kama kupiga basi na kipande cha kanga wamrushia..
Utampigaje mtu mzima mwenzio?
 
Binti yangu na mtoto wangu! Mke hapigwi ... Zipo adhabu lakini sio kipigo.. Pwani sisi kama kupiga basi na kipande cha kanga wamrushia..
Utampigaje mtu mzima mwenzio?
mbona wewe unapigwa hapo kwenye fumanizi?
 
Back
Top Bottom