Kwanini wanaCHADEMA wamekuwa hivi?

Nisifiche na wala nisiwe mnafiki! Mtu kama Tulia Akson namchukia sana tena sana! Sina jema naye hata moja.
Sasa unakuta mtu anakaa na kukwambia chadema wanaleta vurugu, tumeona bungeni kwa makusudi mtu anaambiwa hotuba yako mbadala ili isomwe lzm ifanyiwe edit, na tulia ndio kiongozi wa kuzuia hayo anafikia kuwa mtumwa kila siku eti atoki bungeni wala hawachii wenyeviti kuendesha bunge ili tu kuwadhibiti ukawa, vurugu zinaanzia bungeni alafu watu wananyimwa demokrasia ya kuwaambia watanzania ukweli, wanataka kuja huku kwa wananchi napo wanazuiwa kuongea na wanakamatwa. Alafu mtukufu ana sema siasa zimebakia bungeni sasa kama bungeni unafungwa gavana, na njee hakuna ruksa ya siasa utakwenda wapii
 
UKO PEKE YAKO KATI YA WATANZANIA ELFU 7 WANAOKUUNGA MKONO NI 7 JIULIZE KWA NINI
 
Ninatarajia kuona chama kinachotawala na kilichoshinda uchaguzi uliopita kwa kishido, kinakuwa chama cha watu wanaojiamini, na wanaoamini kwamba sera zao ni bora na ndiyo silaha pekee ya kuendelea kupata ushindi katika chaguzi zinazofuata. Tatizo letu sasa ni kwamba chama hiki ambacho kila siku kinatwambia kinashinda uchaguzi kwa kishindo, kimekuwa chama cha watu waoga kupita kiasi, wasiojiamini na wanaoogopa sana kukosolea na wasiopenda kukosolewa kabisa. Chama cha cha namna hii hugeuka kuwa tishio kwa kila mtu.... na chenyewe hutishwa na kila kitu!
 

Swali zuri...pamoja na kesi kuendelea mahakamani na zingine kuendelea kufunguliwa, maandamano yataendelea kwa sababu mikutano na kuandamana ni haki ya kikatiba. ni sawa na mtu anakukataza usinywe maji. sawa, unafungua kesi mahakamani kumpinga, lakini hata kama unajua kwamba utashinda tu kwa sababu ni haki yako kunywa maji, huwezi kusema usubiri mpaka kesi iamuliwe ndio uanze kunywa maji. vyama vya siasa vinapata uhai kwa kufanya siasa. bahati mbaya serikali ya awamu hii "imegundua" kwamba vyama vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria vikifanya shughuli zao tena kwa mujibu wa sheria, "vinazuia maendeleo". hii ni ajabu, maana tokea mfumo wa vyama vingi uanze enzi za Rais Mwinyi, pamoja na mizengwe ya hapa na pale kubana vyama vya siasa, lakini hawajawahi kuzuia moja kwa moja "mpaka 2020", kama ilivyo hivi sasa. huu ugunduzi wa serikali ya awamu hii unashangaza.

Polisi wakifanya kazi zao kwa weledi wa kipolisi, wala hakuna matatizo. tatizo linakuja pale Polisi wanapofanya kazi kwa maelekezo ya "wanasiasa" au "wakubwa". kuna wakati Lowasa alikuwa anakwenda msibani alipofariki Mzee Peter Kisumo, Agosti 13, 2015. Polisi wakamzuia wakasema hawahitaji msafara, wanaoruhusiwa ni watu wachache tu! Wakasema hayo ni maagizo toka kwa "wakubwa". sasa unashangaa, hivi jamani hata kwenda msibani tunapangiana mwende watu wangapi? wakati mwenye msiba wala hajakataza watu wasije msibani! yaani hiyo "intelijensia" ya Polisi huwa ina malengo yaliyojificha nyuma yake. siku zote wanaozuiliwa ni wapinzani tu. wengine aaahh,
 

Yaani hiki chama kweli ndio kilishinda uchaguzi? sidhani! mbona kinaogopa namna hii? kinatetemeka kwa hofu huku na kule. yaani Wallahi bila kuwa na joto la polisi hapa na pale, chama hiki wala hakifurukuti!!
 
Ngoja niongee kilugha kama baba Jesca aongeapo na watanzania, "Ndamko Ndalo Biswalo.... Ndendya Atukuzwe".
 
Taifa limepinda kwa sababu ya mawazo kama yako. Kama wewe ni kiongozi wa serikali au ccm kwa ngazi yoyote ile, ulitakiwa utuonyeshe hapa ili tuendelee kama taifa tunafanyaje. Itikadi ya ccm ni ujamaa na kujitegemea. Sera ya nchi ni soko huria. Huu mtanziko umetukwamisha kama nchi, ndiyo, viongozi wote, wametoka ccm, lakini kila mmoja anakuja na yake. Huyu wa sasa kaona slogani yake ya hapa kazi tu itamuumbua mapema, sasa anapozuia shughuli za siasa nchi inaendeshwa bila siasa? Akiwa Kahama amesema wajenga nchi ni wanaccm tu, kwa nini tenà anataka wasio wanaccm waitumikie slogan yake? Wewe mwenyewe unaamini kuwa watu wasio ccm hawana maana, kipi kinakufanya uanze kuanisha kutokuwa kwao na maana? Kwani wewe nani amekukataza kuwajibikia majukumu yako.? Kila mara mnahangaika na watu mliokwishà wahukumu, kwa sababu gani? Ni unafiki tuuuu....;;;;;;;;!!!!!!!!!!
 
mambo mengi unaandika kwa kupotosha ili kutibu hasira zako. Kahama mbele ya Lembeli alisema ''CCM ndiye bosi kwa sababu imechaguliwa kutekeleza ilani''...na chama kinachoshinda maana yake wananchi wamechagua mpago wake na kutupa mingine kutoka vyama vingine.
 
Kilazer.Magufuli.Com
 
Tukutane September 1 mlidhani tunatania... Sasa yanaanza kuwauma... Bado hata hatujaezeka
 
Unafiki sio mzuri hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…