Kwanini wanababaika na historia ya African Association?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
KWA NINI WANABABAIKA NA HISTORIA YA AFRICAN ASSOCIATION ILHALI ILISHAANDIKWA?

Jana na ndiyo post yangu ya jana ipo hapo chini nilionyesha makosa ya yaliyopo katika historia ya African Association na kwa hakika ni makosa ambayo watendaji makosa hayo hawakubali kusahihishwa licha ya kuwa watafiti wengine ni wasomi wakubwa sana kwa hali yoyote ile.

Hebu soma hapo chini na fananisha na yaliyomo katika kitabu cha ''Muungano wa Tanganyika na Zanzibar:''
New Left Review 133 / 134 Jan Apr 2022

Issa Shivji, Saida Yahya-Othman and Ng’wanza Kamata,
Development as Rebellion: A Biography of Julius Nyerere
Mkuki na Nyota: Dar es Salaam 2020, £90, hardback
1208 pp, 978 9 9870 8411 1

''For the first twenty years of German colonial rule, ethnic groups waged guerrilla war, culminating in the ruthlessly extinguished Majimaji Uprising of 1905-07; the memory of the repression silenced political action for two decades.''

Katika kitabu cha Mwalimu Nyerere, ''A Biography of Julius Nyerere,'' mwandishi anasema kuwa katika miaka 20 ya utawala wa Wajerumani vikundi vya kikabila walianzisha vita vya msituni vilivyopelekea kuzimwa kikatili kwa Vita Vya Maji.

Kwa uandishi wa namna hii usiotaka muhali mwandishi anakwepa historia muhimu ya mashujaa wa Maji Maji kwa kuwapa nembo ndogo ya kabila (ethnic group) na kukwepa nembo kubwa na muhimu ya dini yao kuwa Wajerumani walipambana kwa silaha na Waislam.

Ushahidi wa ukweli huu utaupata kwenye minara na makaburi katika kumbukumbu za Maji Maji katika miji ya Kilwa na Songea.

Unachotakiwa kufanya ni kusoma majina katika minara hiyo ya kumbukumbu ingawa pamepitika juhudi ya kubadili majina ya Kiislam kama vile Abdulrauf Songea Mbano kuitwa Songea Mbano likaachwa jina la ''Abdulrauf'' na kukwepa jina la ''Khadija'' likatajwa ''Mkomanile,'' akawa anatambulika kwa jina moja tu la Mkomanile.

Haya ni kwa uchache.

Sasa soma hapo chini kuhusu kuundwa kwa African Association mwaka wa 1929:

''Reorganization slowly gathered pace: in 1929, a group of teachers and civil servants formed the African Association, the first in a line of organizations that would evolve into Nyerere’s political party, the Tanganyika African National Union (tanu).''

Mwandishi anasema kuwa African Association imeundwa na kundi la walimu na wafanyakazi wa serikali na anamalizia kwa kusema kuwa hii African Association ikamalizikia katika chama cha TANU cha Nyerere.

Kalamu ya mwandishi haitaki muhali imemuuzia Mwalimu Nyerere chama cha TANU kwa gharama ndogo sana baada ya kumuunganisha na African Association kimya kimya.

Lakini muasisi wa African Association Kleist Sykes kaacha mswada wa kitabu kabla hajafa anaeleza kwa kirefu kabisa vipi African Association iliundwa mwaka wa 1929 na kaweka majina ya waasisi wake: President Cecil Matola, Secretary Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Ukisoma kitabu hicho hapo chini utaipata historia yote ya African Association kwa uhakika na ukweli wake na vipi kutokana na African Association ikaundwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa 1933 President akiwa Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Sykes.

Bila ya kuijua historia hii huwezi kuandika kwa uhakika na ukweli wake historia ya Julius Nyerere na historia ya TANU.

(Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed) ''Modern Tanzanians,'' Nairobi, 1973, pp. 95-114).

PICHA: Kulia ni Kleist Sykes na Mzee bin Sudi.

1664252164714.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom