GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,697
- 109,125
Hivi kunaweza kweli ndani ya ama Miezi Mitatu au Miwili kukafanyika ' Mabadiliko ' ya Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais ( PSU ) na TISS DG ambapo kabla yake Naibu wake ( TISS ) aliondolewa na kuwa RAS huko Tabora, halafu kusiwe na ama hali na wasiwasi / mashaka kabisa juu ya Usalama wa Mheshimiwa Rais wetu? Je hakuwezekani kwamba labda ndani huko Idarani ( Taasisini ) kuna ' Vuguvugu ' kubwa na pengine labda kuna Mipango ilikuwa inaendelea hivyo imezimwa ' Kiujasusi ' kupitia hizi Teuzi za hawa Watu muhimu Wawili ukiachilia mbali na Yule wa Jeshini?
Naomba ' Logically ' kabisa leo tulijadili hili ili tuwasaidie Wasaidizi wake kwani linashtua na linaogopesha pia. Ukiangalia matukio mengi ya Marais wengi ama Kupinduliwa au Kuuwawa kabisa huwa yanakuja ghafla baada ya Mabadilko katika Idara Nyeti hasa za Usalama na ile ya Jeshini pia.
Sisemi na sitaki Kuhalalisha kuwa labda Uzi huu nimeuanzisha nikiwa na maana ya kwamba Usalama wa Mheshmiwa Rais wetu uko Mashakani lakini katika hali ya kawaida na hasa ukilitumia Jicho Pevu la Ndege Tai haya Mabadiliko ya ghafla na hizi Teuzi za ghafla huko Usalama na Jeshini zinaweza kukupa Picha fulani kuwa pengine hali si Shwari ila Wananchi tunafichwa tu kwakuwa wenyewe wanasema kuwa kuna tunayoyajua na yale tusiyoyajua pia.
Karibuni katika Mjadala ambao nahitaji uwe ni wa Afya ( Tija ) zaidi na tuonyeshe kuwa kweli Sisi ni ' Great Thinkers ' wa JF.