Nchi yetu ina makabila mengi sana na kwa uwingi huo unafanya nchi yetu kuvutia.Na inavutia zaidi hasa pale utakapowakuta watu kutoka maeneo mbalimbali wakizungumza kiswahili kwa lafudhi zao.
Lakini kabila la wamakonde wamekuwa wakidharauliwa kila wafikapo maeneo mengine.
Sijajua kwa lipi hasa lafudhi,makosa yao ya kisarufi,hulka zao au nini.Kama lafudhi binafs ya kiluguru,kinyakyusa hata kikurya zinachekesha zipo nyingne.Kama makosa yao ya kisarufi wapemba nao hawana m mimi binafsi kabila langu halina l pia wachaga hawana z,kama ni hulka zinafanana na upwani za umwinyi makabila meng kama wazaramo wanazo hizo.
Kwa sasa mkoa wao unaendelea kwa kasi asilimia 90 ya vitu vnavyohtajika vipo vyuo vya juu,vya kati,mahotel,mkoa wao upo vizur kimpangilio,fukwe ya kuvutia na hata barabara ya kwenda dar haiwetenganish mbal na dar masaa kama 6 au 7 tena kuna root za saa 2,4 na kuendelea.Wazawa wanasoma kwa uchungu.Kwa kweli nilipoenda kwa kazi zangu binafsi nimeshangazwa juu ya stori za uongo juu ya kabila na mkoa wao.
kihistoria wamakonde wanaonekana ni watu kutoka msumbiji na hata mkoa wa mtwara na lindi yote ilikua sehemu ya msumbiji, huenda hilo inaweza kuwa sababu ya kuadharau wamakonde.
mkuu funguka turekebishane
kuna dharau fulani inaambatana na hiyo.......ngoja nikupe mfanoMkapa ni mmakonde....hawadharauliwi ila wanataniwa....tofautisha utani na dharau
Kwani msumbiji ndio wadharauliwe? Sio sababu. Mimi nafikiri umaskini tu, kabila lolote likiambatana na uwezo wa pesa au sifa fulani nzuri hakuna cha lafudhi, maumbile wala majina kitadharauliwa. Aliyesema tabia za umwinyi kapatia kabisa, issue ni kuwa tofauti na wenzao wa pwani kama Tanga, Dar miundo mbinu iliiwezesha miji kukua kwa kujengwa viwanda hivyo ardhi yao ikawa ndo mkombozi wao maana nao hawana zao la kutegemea. Ardhi wanauza, wanapangisha wafanyakazi, wafanyabiashara imewawezesha kusoma, kuwekeza na kuinuka. Mtwara na Lindi barabara na hasa daraja ndo imejengwa juzi, sasa viwanda, bandari na madini vimegunduliwa. Sasa hivi wataanza kuuza ardhi, kupangisha na hivyo kukua haraka. Kama lafudhi au lugha ndio maendeleo tembelea kanda ya Ziwa ndani huko au umasaini uone Kiswahili chao au Pemba halafu uone kama wanadharauliwa. Maendeleo tu ndio yatatukomboa sio ukabila