Kwanini walimkataa Salim A. Salim?

Personally i think Salim is perfect but, But Znz is a big problem, Hawa jamaa ni wazushi sana
 
Leo nimemuona Salim Ahmed Salim akikabidhi tuzo ya Mo Ibrahim kwa mshindi wa tuzo hiyo Pedro Verona Pires, Rais Mstaafu wa visiwa vya Cape Verde. Kwa jinsi alivyokuwa anaongea na kujistahi nikajiuliza ilikuwaje mara mbili (1985 na 2005) wanachama wa chama chake walikataa asiwe mgombea wa chama chao kwenye nafasi ya Urais. Ina maana yeye sifa zake ni pungufu kuliko za Ally Hassani Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete?

Mapungufu ya Salim ni nini na ubora wao kina Mwinyi na Kikwete ni upi? Huyu jamaa kama taifa tunaweza kumtumia vipi kwani kwa inavyoelekea haiwezekani tena kwa yeye kugombea urais 2015.

Jamaa angeshika nchi huyu tungekuwa mbali sana
Angefanya kama anavyo fanya Satta
 
swali ana makundi ya kuiba nayo(MAFISADI)
Maana wengine waliingia kwenye mikataba ya ufisadi ndo maana wakapita kwenye uchaguzi.
 
Hivi nyinyi watanzania mtaondokana na ujinga/upumbavu huu lini? Kwanini mnafikilia RAIS lazima atoke CCM?! CCM imechoka tunahitaji kuipumzisha kama KANU, UNIP etc
Unamlinganishaje Salim na Slaa!! Huo nao ni ujinga mwingine kwamba vyama ni vyama na sio Personalities. Ni kweli kwamba CCM imechoka lakini hapa hatujadili kama CCM itoe rais mwaka 2015 bali ni kama taifa tutautumiaje ujuzi na uadilifu wa kutukuka wa Salim.

Hivi Slaa akijiunga na CCM atendelea kuwa msafi au chama kitakuwa kimemchafua. Na leo hii Lowassa akijiunga na CHADEMA ataendelea kuwa "fisadi" au CHADEMA itamtakasa?
 
Kwa Waislamu hakuna atakaye kuwa bora... watatafuta chochote kukukosoa Salim alikuwa anaelimu bora zaidi ya Kikwete, kazi bora serikalini na kwenye chama zaidi ya kikwete, alifanya kazi nje ya nchi kwahiyo alijua masuala mengi ya kimataifa wakati alisha kuwa raisi wa baraza la Umoja wa Mataifa na kuikubali China kuwa Mwanachama.

Lakini waislamu wanajajua jinsi ya kubaguana, wakapata namna ya kumbagua kwa rangi yake na bila Nyerere labda wangemuua wakati wa mapinduzi ya Zanzibar.

He!Haya sasa mapya!sasa hapo waislamu wanaingiaje mkuu?Ndugu yangu DK SALIM alikuwa "victim"wa sababu za kihistoria,aliponzwa na historia yake katika chama<alitokea hizbu> na hiyvo wana CCM mahafidhina wakawa wanamkataa kwa sababu ya ujinga wao!sasa hapo waislamu wameingiaje?Du!aisee kwa kweli kazi ipo!
 
He!Haya sasa mapya!sasa hapo waislamu wanaingiaje mkuu?Ndugu yangu DK SALIM alikuwa "victim"wa sababu za kihistoria,aliponzwa na historia yake katika chama<alitokea hizbu> na hiyvo wana CCM mahafidhina wakawa wanamkataa kwa sababu ya ujinga wao!sasa hapo waislamu wameingiaje?Du!aisee kwa kweli kazi ipo!
Sijui huu upofu wa kuchanganya Uislamu na ujinga utaisha lini humu JF?
 
Back
Top Bottom