Kwanini walimkataa Salim A. Salim?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,223
Leo nimemuona Salim Ahmed Salim akikabidhi tuzo ya Mo Ibrahim kwa mshindi wa tuzo hiyo Pedro Verona Pires, Rais Mstaafu wa visiwa vya Cape Verde. Kwa jinsi alivyokuwa anaongea na kujistahi nikajiuliza ilikuwaje mara mbili (1985 na 2005) wanachama wa chama chake walikataa asiwe mgombea wa chama chao kwenye nafasi ya Urais. Ina maana yeye sifa zake ni pungufu kuliko za Ally Hassani Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete?

Mapungufu ya Salim ni nini na ubora wao kina Mwinyi na Kikwete ni upi? Huyu jamaa kama taifa tunaweza kumtumia vipi kwani kwa inavyoelekea haiwezekani tena kwa yeye kugombea urais 2015.
 
Oct 5, 2011
63
16
kwa nini asigombee 2015 inawezekana labda mwenyewe akatae! na wasipo mteua basi tujiandae kuona taifa hili likipasuka vipande viwili kama ilivyotokea kwa sudani kaskazini na kusuni.katu wazanzibar hawatakubali safari ijayo rais atoke bara tena.kama ulifuatilia mjadala wa katiba mpiya uliofanyika zanziba hili lilikuwa wazi kabisa
 

Sniper

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,957
611
Umesahahu JK na timu yake ya majungu walivyomchafua Salim kwenye mbio za uraisi 2005? JK silaha yake kubwa ni 'Character Assasination', Alimchafua Salim, akamchafua Sumaye, akamchafua Kigoda, CUF akawasingizia ishu za visu na udini, dah this guy...
 

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,940
1,427
Ana umri gani sasa hivi ? Maana kwa Tanzani kwa wengine Pension yao ni Bungeni
 

Sniper

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,957
611
Salim angekuwa rais wa JMT badala ya mwinyi, lilikuwa ni chaguo la Mwalimu kwa wakati huo, lakini wa Zanzibari walimkataa, ndipo Mwinyi alipochaguliwa kugombea. 2005, madudu aliyoyafanya JK kumchafua Salim, wote mnayajua
 

peri

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,581
1,162
Tatizo siasa za bongo mkuu. Full usanii kuanzia chama tawala mpaka upinzani.
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Salim A Salim hana Makundi kama Kikwete na Mwinyi walivyo nanyo; hana ulafi kama Makamba na Kikwete walivyonavyo; he's a very clean politician akichagua mtu ni kwa sababu ya CV yake na sio baba yako au Mama yako

Wengi walimuogopa sababu ya hayo; angalia allivyoimudu Wizara ya Ulinzi wakati ule hata Wizara haina pesa...

He was the force for power...
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,878
3,725
Salim is the president that we never had; tukaambulia mafisadi mpaka wengine wanapoka migodi!! Have you ever wondered why Mkapa came out of retirement to campaign for Kafumu in Igunga? He facilitated the acquisition of the coal mine!!
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Kwa Waislamu hakuna atakaye kuwa bora... watatafuta chochote kukukosoa Salim alikuwa anaelimu bora zaidi ya Kikwete, kazi bora serikalini na kwenye chama zaidi ya kikwete, alifanya kazi nje ya nchi kwahiyo alijua masuala mengi ya kimataifa wakati alisha kuwa raisi wa baraza la Umoja wa Mataifa na kuikubali China kuwa Mwanachama.

Lakini waislamu wanajajua jinsi ya kubaguana, wakapata namna ya kumbagua kwa rangi yake na bila Nyerere labda wangemuua wakati wa mapinduzi ya Zanzibar.
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
225
Ni uhayawani tu wa Wazanzibari. Hebu fikiria kwa upande mdogo wa Muungano wetu, yaani Visiwani, kutoa Rais wa Jamhuri huwa ni fahari kubwa sana, kwa tafsiri yoyote ile. Lakini mwaka 2005 hao Wazanzibari walisema "Yakhe sisi huku hatuna moto sana wa kutoa Rais wa Jamhuri, endeleeni tu huko Bara kutoa Rais wa jamhuri, hatuna noma siye!"

Watu wa ajabu kabisa hawa.
 

Wayne

JF-Expert Member
May 27, 2009
660
199
kwa nini asigombee 2015 inawezekana labda mwenyewe akatae! na wasipo mteua basi tujiandae kuona taifa hili likipasuka vipande viwili kama ilivyotokea kwa sudani kaskazini na kusuni.katu wazanzibar hawatakubali safari ijayo rais atoke bara tena.kama ulifuatilia mjadala wa katiba mpiya uliofanyika zanziba hili lilikuwa wazi kabisa

Mkulu

Ni wazanzibar waliokuwa mstari wa mbele Salim asiwe presidential nominee wa CCM 2005, wakaleta mpaka ushahidi wa ku-support hoja zao za kumpinga.

Ni wakati huo ambapo ule utaratibu usiorasmi wa kubadilishana urais ulipovurugwa.

Hawana wa kumlaumu.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,153
19,112
seems clean,experienced but as long he holds that ccm card,...i really doubt him,..ukishakuwa hiki chama huwa hutabiliki,.who thought kikwete would turn to be monster???
 

BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,097
1,324
Kiukweli hakuna wa kuikomboa tz. Wanasiasa wa vyama vyote wapo kimaslahi zaidi labda tupate wajomba kama wale wa bengazi otherwise tutalalamika sana hapa jamvini.
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
3,262
Hivi nyinyi watanzania mtaondokana na ujinga/upumbavu huu lini? Kwanini mnafikilia RAIS lazima atoke CCM?! CCM imechoka tunahitaji kuipumzisha kama KANU, UNIP etc
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom